Hivi sisi tukoje?

hapa naona kuna vitu viwili.. kwanza wanachi kujichukulia sheria mkononi na la pili kituo cha television kuonyesha tukio lile.. kitendo cha kujichukulia sheria mkononi hakina excuse naomba tukubaliane hilo.. kama tunatambua kuna sheria na vyombo vya sheria basi hatupaswi kuchukua sheria mikononi mwetu.. hii dhana ya kusema tukiwapeleka wahalifu polisi wanarudi ni dhana iliokosa mashiko kwa sababu wengi wetu tunaamini ukishamkamata mhalifu na kumpeleka polisi basi umemaliza.. unataka polisi ndio ampeleke mahakamani na polisi huyo atoe ushahidi.. ni wangapi tumefuatilia kuona haki inatendeka kwa kuhudhuria mahakamani na kuona haki imetendeka..? kwamba tumetoa ushahidi dhidi ya mhalifu..? hakuna.. tumegeuka kuwa mabingwa wa kutoa lawama kwa polisi na kusahau sie ndo tunaosababisha hawa wahalifu wengi wawepo uraini.. tunawasema polisi wanachukua rushwa sawa wanachukua.. ila ci tunawasaidia kwa kutohudhuria mahakamani..! halafu ukitaka kujua kama sisi ni wanafiki.. miongoni mwetu tunao ndugu zetu ambao ni wahalifu.. mara ngapi tunachanga hela za kwenda kuwahonga polisi ili ndugu zetu watoke..? unapata ujaciri gani leo kuhonga hela ndugu yako muhalifu aachiwe.. kesho unaenda kumchoma moto mhalifu mwingine..???
na kuna mistake identity.. kama mnakumbuka juzijuzi hapa kule ukonga.. wananchi wamemuua askari wa magereza kwa kudhania ni mwizi..!!
suala la kituo cha television kuonyesha habari na picha ile kwangu mie naona sio vibaya kama walitoa tahadhari mapema..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom