MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Kwa habari nilizosoma kupitia ile post ya Mbunge wa Momba Davidi Silinde kwamba vijana wa CHASO Dodoma wamezuiwa kufanya mahafali yao Kwa madai ya kutokua na kibali cha polisi!
Wanasheria mnashauri nini au mnatoa ushauri gani juu ya hili? Imekaaje hii? Ina maana hata Sendof na harusi zitakua zinafanyika kwa kibali?
Wanasheria mnashauri nini au mnatoa ushauri gani juu ya hili? Imekaaje hii? Ina maana hata Sendof na harusi zitakua zinafanyika kwa kibali?
Na Faraja Simon
Unapoamua kuwa kiongozi ni muhimu kutambua kuwa wewe ni kiongozi wa wote. Si wa wanachama wa chama chako tu.
JPM ni muhimu zaidi kuheshimu uwepo wa hawa wenzetu, hoja kinzani ni muhimu sana katika kuijenga Tanzania. Lazima tufikiri tofauti katika kuijenga Tanzania yetu ili kuja na kitu bora zaidi. Kwa hili wanachaso mkoa wa Dodoma wameonewa sana.
Lakini polisi mbona shirikisho la vyuo vikuu (CCM) Walifanya mahafali yao na mgeni rasmi akiwa Rais mstaafu JK na walifanya bila tabu yoyote? Kuna tatizo gani kwa chaso kufanya mahafali yao? Bila shaka tatizo sio mahafali ya chaso ni mgeni rasmi.
Nadhani tatizo hapo haliwezi kuwa mahafali ya wanachadema, tatizo ni mgeni rasmi waliyemualika. Mgeni rasmi amekuwa mwiba katika kufanikisha mahafali yao kama wanachaso.
Ni kweli bado mgeni rasmi ana impact kubwa sana na pengine hofu ni Hotuba atakayoitoa ila ni kwa nini kuogopa? Uvccm si IPO kujibu mashambulizi kwa hoja?
Hii ni nidhamu ya uoga mnayowafundisha vijana wa CCM. Watazoea ubabe badala ya ukinzani wa hoja. Wenzetu wanafanya tafiti na wanajibu hoja za ccm kwa ufanisi mkubwa na maandiko yao yanaimpact sana. Sisi tuna endelea kujenga vijana wenye kuamini kulindwa kwa nguvu ya dola. Ni muhimu sana kuwajenga vijana katika mapambano ya kifikra kuliko mabavu au kutegemea mwamvuli wa nguvu ya dola. Hii itawasaidia sana.
-F.S