Hivi Sheria za Barabarani haziwahusu Madereva wa Serikali?

Master Legendary

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
550
786
Nimesikia Meneja wa MSD kafariki kwa ajali leo nimeumia sana, ila nimeangalia picha ya ajali ni kama Dereva alimhamishia ajali upande wake kujiokoa yeye madereva watanielewa.

Ila kinachonikera kila siku nawafuatilia hawa Madereva wa Serikali wanavyoendesha bila kufuata uataratibu na Sheria za Barabarani, yani wamejisahau wana viburi na dharau wanaona hizi Sheria haziwahusu kabisa,na kibaya Matrafiki wanawaona na wanawachekelea tu sijui kwasababu wakiwakamata hawapati chochote au wanawaogopa tu kwavile wanadhani wamebeba Mabosi.

Ni kawaida sasa kupita kwenye taa nyekundu,kupita kwenye Maeneo yasiyoruhusiwa,kuoverspeed kwenye speedlimit,kuovertake pasiporuhusiwa na Matrafiki wanawaona hawachukui hatua zozote.

Hii imefikia stage mbaya kiasi Madereva hawa hawaoni kama sheria za Barabarani zinawahusu kiasi cha kusababisha ajali,ulemavu na vifo kwa wasio na hatia.

Niwakumbushe tu Matrafiki Sheria ni Msumeno,hili mnalotengeneza ni bomu hamjui litamkuta nani kuna siku watasababisha ajali itakayopoteza Familia yako ndiyo mtaona Uchungu.

Wenzenu wanapozika na kuuguza endeleeni kujiona tu hamhusiki


Ni tahadhari tu kabla ya jahazi kuzama.
 
Meneja wa MSD unafariki kipindi cha ulaji,daaah! R.I.P
 
Mimi naomba mchango nitakaoutoa hapa uwafikie LATRA, Traffic police, Mkuu wa mkoa na serikali za mitaa.

Kumekuwa na kero kubwa na isiyoisha ya foleni za kijinga zinazosababishwa na vituo vya daladala punde mabasi yanapotega abiria, kupanda au kushusha abiria mfano Mwananyamala A, Studio, Tandika mwisho, Mwembeyanga, Kawe ukwamani, Tegeta kwa ndevu, Bunju B.

Tunaomba anayehusika atoe adhabu kali kwa daladala zinazosababisha foleni barabara kuu bila sababu ya msingi kisa kutega mingo za abiria. Vituo nilivyotaja vingi ni vya kupanda na kushusha lakini mabasi huwa yanageuza ndio mwisho wa stendi na kuzuia njia nzima. Foleni za ajabu huwa zinatokea mfano Tegeta kwa ndevu. Ni wakati wa kuchukua hatua na kukamata mabasi yote yanayosimama hovyo na kupaki njiani.
 
Back
Top Bottom