Hivi Rombo, Same na Mwanga ni Moshi?

kikahe

JF-Expert Member
May 23, 2009
1,351
1,500
Watu wengi wakienda kwao Rombo, same, Mwanga hata Hai utawasikia wanasema tunaenda MOSHI. Mbona hizo ni Wilaya tofauti na Moshi?
Jamani nisaidieni kwa hili.
Nawasilisha
 

Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
831
0
Rombo Same na Mwanga zote ni Wilaya ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro huku Moshi ikiwa Manispaa na pia Moshi ukiwa mji mkuu wa Kilimanjaro.
 

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
9,283
2,000
watu wengi hutumia jina la moshi akimaanisha kilimanjaro ndio maana mtu akienda moja ya hizo wilaya ulizotaja husema anaenda moshi
 

NEW NOEL

JF-Expert Member
May 21, 2011
859
500
Yawezekana wana sababu zao,pengine wanahisi wakitaja kuwa wanatokea maeneo kama ya Same,au Mwanga na Rombo wataonekana wanatokea vijijini kivile. Unajua Mwanga,Same na Rombo ni wilaya ambazo hazina maendeleo sana ukilinganisha na wilaya nyingine za Kilimanjaro.
Lakini pia jina la Moshi limezoeleka sana kuliko Kilimanjaro.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
40,629
2,000
Moshi ni wilaya na ni makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro na si vinginevyo. Mwanga huwezi kuita ni Moshi wala Rombo wala Hai wala Same kwa namna yoyote ile.
Kuna mikoa wilaya zao ambapo ndipo zilipo makao makuu ya mikoa yao imekuwa maarufukuliko mikoa yenyewe, mfano Musoma, Songea n;k.
 

Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
831
0
Pia Moshi nikimaanisha Kilimanjaro ingekuwa nchi kama siyo udhalimu na wivu wa Julius Kambarage Nyerere.
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,571
2,000
Ni kweli babaangu watu wanachanga?? wanachanganya kweli.....hivi uru ipo sehemu gani kati ya hizo wilaya?
 

Kyalow

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,288
2,000
uru ipo moshi...kuanzia stendi kuu na kuendelea hadi KCMC na katika yale mashamba ya kahawa ya USAGARA
 

zumbemkuu

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
10,141
2,000
mtu anatokea huko igunga ndani ndani yuko hapa mjini ukimwambia unaenda SAME au MWANGA au ROMBO atakuelewa kweli? nikiwa Mbeya simwambii mtu naenda Lushoto, jibu ni Tanga ili kupunguza maswali.
 

Baba_Enock

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
6,972
2,000
Makao Makuu ya Mkoa ndiyo ufahamika kama jina wakilishi la Mkoa:-

Kwa mfano unapotoka Bukoba kuja Temeke, unaaga kuwa unakwenda Dar es Salaam na siyo Temeke!

Dar-Moshi
Dar-Bukoba
Dar-Musoma
Dar-Sumbawanga
Dar-Songea
Dar-Mbeya
Dar-Singida
 

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,339
2,000
Rombo ni Jamhuri! Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Rombo. Lol...!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom