Hivi Rastam Aziz ni nani Tanzania na ndani ya CCM?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,955
543
Kila tetesi tunazosikia kumuhusu Rostam zinatimia ina maana ana nguvu gani hata M/kiti wa CCM hapingi na CC ya CCM wanafuata maamuzi yake.Huyu mtu ni nani hasa kwani maamuzi ya CCM na Serikali yanaonekana kuwa na shinikizo lake,sasa uchaguzi wa nini?
 
Kila tetesi tunazosikia kumuhusu Rostam zinatimia ina maana ana nguvu gani hata M/kiti wa CCM hapingi na CC ya CCM wanafuata maamuzi yake.Huyu mtu ni nani hasa kwani maamuzi ya CCM na Serikali yanaonekana kuwa na shinikizo lake,sasa uchaguzi wa nini?... RA alias Kingmaker, alitaka ZM alias Zakia Meghji ateuliwe mgombea mwenza wakati uleeee...wazee wakaja juu..... iweje President RA (JK) na Mke (Mkwewe) awe VP. Jamaa alikuja juu sana, kama mnakumbuka alijifungia pahala na hatimaye kujitokeza nadhani 30 minutes later kutangaza jina la Nuclear Physicist kuwa mgombea mwenza.

Inafurahisha sana hii...yule Waziri wa Pesa alokiri eti kaindizwa mjini na Gavana (RIP???) sasa huyooo...
 
Kila tetesi tunazosikia kumuhusu Rostam zinatimia ina maana ana nguvu gani hata M/kiti wa CCM hapingi na CC ya CCM wanafuata maamuzi yake.Huyu mtu ni nani hasa kwani maamuzi ya CCM na Serikali yanaonekana kuwa na shinikizo lake,sasa uchaguzi wa nini?

CCM kila mtu anasharubu kama kambale. Mweneyekiti mwenyewe wa chama anazidiwa msimamo na mkewe na mtoto wake unatarajia atayaweza haya majitu ndani ya CCM??? Hawa ndio kila kitu CCM na ndio wenyewe hawa bana. ILA MIE NAWASHUKURU MAANA WANAHARAKISHA KUANGUSHWA KWA CCM MAPEMA ZAIDI. BIG UP ROSTAM
 
Rostam Aziz ni Managing Director wa CCM, na ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna anaye bisha?
 
Kama hujui Rostam ni nani, soma habari hii iliyoandikwa humu humu JF:

"Ukweli kuhusu Rostam Azizi

Ukurasa mpya wa nchi ulifunuliwa baada ya kifo cha baba wa Taifa mwalimu Nyerere kwa kuingiliwa kijanja na taifa la nje ambalo linafanya maamuzi ya kiungozi bila watanzania wenyewe kufahamu kwa kujipenyeza kwenye uongozi wa chama cha mapinduzi CCM watu ambao kabla ya kifo cha mwalimu Nyerere haikuwezekana kushika nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Mambo haya yanawezekanaje ?
Ikumbukwe kwamba wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere Nchi ya Irani ilikuja Tanzania kujenga mradi wa barabara ya Lindi –Kibiti lakini muda mfupi mwalimu Nyerere alisitisha ujenzi huo baada ya kugundua kuwa nchi hiyo ilikuwa na wazo la kuitawala Tanzania nasio kutekekeleza mradi huo . Kwa wale wasio jua kipindi hiki, ilikuwa ni miaka ya themenini kabla mwalimu Nyerere hajag'atuka uongozi.

Iran baada ya kutimuliwa kwenye mradi huo ,ilimkabidhi Rostam Azizi mitambo yote ya ujenzi ambayo ingetumika kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo,ingawa hakuna anyejua walifahamiana vipi na Rostam Azizi.

Watu wanaomfahamu Rostam Azizi wanasema yeye ni miongoni mwa wa Irani waliopo Tanzania ambaye kwa sasa makazi yake yako Igunga mkoani Tabora , ndugu zake wakaribu wengi wao wanapatikana katika maeneo Mwisi ,Sungwizi , Ndembezi,Bukene ,Mwamala na Itobo mkoani humo ,huku wengine wakiishi Lujewa mjini , mbarali mkoani Mbeya wakilima mpunga.

Nini uhusiano kati ya Rostam Azizi na Iran na zana za ujenzi alizokabidhiwa ,kampuni ya ujenzi wa Caspian construction Tanzania ilianzishwa kwa mtaji wa vifaa hiyo alivyokabidhiwa na Iran,kampuni ambayo pia imefahamika baadaye kuwa ni moja ya matawi ya kampuni mama ya Caspian.

Mitambo hiyo tangu wakati huo inaendelea kutumika kuchimba madini kwenye migodi yote hapa nchini .

Caspian Tanzania haichukui tenda za kuchimba madini moja kwa moja ila kwa mara ya kwanza ilipita kwenye kampuni iliyojenga hospitali ya Rufaa ya Mbeya mitambo yake ambayo ilikuwa ikihifadhiwa eneo la Pugu Road Daresalam baada ya kumaliza ujenzi wa hospitali . kampuni hiyo ilitoweka katika mazingira tata.

Kazi ya uchimbaji madini kwenye migodi yote nchini tangu mwanzo inaonekana kufanywa na mitambo ya kampuni ya Caspian construction ya afrika kusini lakini ukweli ni kwamba kampuni ya Caspian Tanzania ambayo mmliki wake ni Rostam Azizi ndiyo inayojishugulisha na kazi hiyo kwa kivuli cha Caspian ya Afrika kusini.


Tunataka Dunia ijue kuwa Tanzania imevamiwa na Iran na kila anayeiunga mkono Tanzania anaiunga mkono Iran kwa sababu ,mitambo ya Caspian construction Company Tanzania ambayo inamilikiwa na Rostam Azizi ndiyo inayochimba madini kwenye migodi yote hapa nchini ,sehemu ya madini hayo yanapelekwa ulaya ,lakini sehemu kubwa ya madini yote yanakwenda Iran kupitia Caspian construction company.

Kampuni hiyo pia ndiyo inayoamua mchanga kutoka mgodi upi upelekwe nje ya Tanzania ,Ni kampuni hii ambayo pia inapeleka ulaya Sehemu ndogo ya madini hayo kuwapumbaza watanzania wasijue Irani inavyowaibia madin yao.

Vianzo huru vinaweka bayana kuwa asilima 3 ya marahaba inayopata Tanzania inatokana na kiasi cha madini yake yanayokwenda ulaya,wakati sehemu yote ya madini yanayopelekwa Iran hayatozwi chochote ukiachilia mbali mchanga ambao pia unauzwa Dubai kwa ajili ya kujengea hoteli za kifahari na kunakshi mazingira ya hoteli hizo.

Mbali na Tanzania kuibiwa madini yake ,Marekani ambalo ni Taifa kubwa duniani kwa miaka mingi linapambana na ugaidi duniani , vyanzo vya uhakika vinathibitisha kuwa haliwezi kutimiza jukumu hilo bila kwanza kukata mizizi ya Iran iliyojikita nchini Tanzania ambako inachukua bure mdini ya uranium kupitia kampuni ya Caspian construction Tanzania .

Kwa hiyo Rais wa marekani Baraka Obama kuendelea kuumbatia utawala wa Jakaya kikwete ni kuiunga mkono Iran, iwe inajua au haijui huo ndiyo ukweli na ndiyo maana hadi sasa Iran inakiburi katika kutekeleza vikwazo vya kimataifa dhidi ya urutubishaji wa madini ya uranium kwa kuwa ina hazina kubwa ya madini hayo kutoka Tanzania na kwamba Marekani bila kujijua iko nyuma yake.

Kupitia makala haya tunamwonesha marekani,washirika wake katika vita dhidi ya ugaidi na watanzania kuwa wakala wa moja kwa moja wa shirika la jasusi la Iran hapa Tanzania ni Rostam Azizi na namna anavyoendesha shughuli zake za kijasusi kwa ajili ya Iran.

Rostam Azizi ana vituo vikuu viwili Afrika kusini na Ujerumani ambako hukutana na maafisa wa shirika hilo la ujasusi la Iran wanaompangia kazi ingawa kituo chake kikubwa ni ujerumani .Mara zote anapoondoka hapa nchini anaaga kwa visingizio tofauti ikiwemo kupelaka mgonjwa.

Hajawahi hata mara moja kwenda Iran na kama amewahi kufanya hivyo ni kwa siri na kupitia nchi nyingine ,hii ina maanisha nini ?anawaghiribu wa Tanzania wasifahamu ujasusi wake na hivyo amefanikiwa kuikwepa idara ya ujasusi ya Tanzania ambayo kwa miaka mingi imejigamba kuwa na uwezo mkubwa wa kazi. Kama sivyo Jasusi huyu amefanikiwa kuinunua Idara hiyo.

Iran inafahamu kwamba kikwete anafahamu ujasusi wa Irani hapa nchini ,lakini anaogopa kuchukua hatua dhidi yao akihofia kuhatarisha maisha yake ,kwani amejipeleka mno kwao hata ameozwa mtoto wa Megheji na mtoto wa Asas ambaye harusi yake ilifanyikia kwenye hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika mkoa wa Iringa, wote hawa ni wa Iran.

Ndiyo maana ubadhilifu wote unaofanywa na Rostam Azizi kikwete anashindwa hata kuukemea sembuse kuchukua hutua za kisheria? Kwa hiyo kitendo cha Jakaya kikwete alipokuwa igumga wakati wa kampeni zake za Urais kumunadi Rostam Azizi kuwa ni mtu safi hazikuwa za kubahatisha na zinatoa picha kuwa bila Rostam Azizi kikwete hawezi kuongoza nchi.

Inaendelea-------------- "
 
Mmoja wa wapigakura wa jimbo la igunga aliwahi kumuuliza RA kwanini katika kipindi chake chote kilichopita kama mbuge wao hakuwahi kuiuliza serikali swali lolote kupitia Bunge? Mh. RA alijibu mipango yote ya serikali anaijua na anashiriki katika kuipanga kwahiyo kuiliza maswali bungeni ni sawa na mwalimu kutunga mtihani na kisha kuujibu mwenyewe. Huyu sasa nizaidi ya mbuge! huyu ndiye aliyeshikilia roho za watanzania zaidi ya milioni 43.:A S angry:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom