Hivi Rais Magufuli ni Mwafrika kweli?

Hivi Rais Magufuli ni Mwafrika kweli?

ndyo mwafrika angekuwa mzngu s ungemuona kila sku anakwenda udhunguni
 
Tuache utumwa wa fikra wasiopenda kwenda ulaya ni wengi mno. mimi binafsi huwa sipendi kutoka hata nje ya mkoa wangu huwa nahisi sina amani moyoni. hata kama nikisafiri nje ya mkoa,siku ninayorudi nikiingia ndani ya himaya ya mkoa wangu huwa nahisi joy ndani ya moyo wangu.
nina marafiki wengi majuu waokuja kazin kwetu ku- vulunteer kama kutoka shirika la pscop wakimaliza mikataba yao hunialika niende kwao kiukweli huwa nahisi moyo unaenda mbio kutoka nje ya TZ!.... Sijawahi kufikiri kabisa.
kiingereza kinapanda na mimi ndio huwapokea wazungu hao na kuwapa ushirikiano wa hali ya juu.wao hunipenda sana maana huwa siendekezi dhiki na hata tukisafiri pamoja huwa tuna-share cost almost in everything. mpaka baadhi ya ndugu zangu hunishang'aa eti nachezea bahati lol
 
Bado mgeni hujaelewa misemo chokonozi ya JF. Swali hilo ambalo linaulizwa na Mwandishi wa CNN limewekwa hivyo kwa kusudio maalum. Mjadala unavyoendelea utaelewa.
JF ; the home of great thinkers.
Huna lolote wewe! Kubali tu kua umejifanya mjuaji lakini mwisho wa siku umeumbuka tu, usitufanye sie ni watoto wenzako,

Siku nyingine usipende sana kukurupuka hii ndio JF au ulifikiri upo kwenye kile kijiwe chenu pale chini ya muembe?
 
Hata Mimi sipendi kwenda Uarabuni kwa vile lugha yao siijui.
Sasa JPM hata yeye kila akifikiri kuwa akifika kule kisha CNN, BBC, Skynews nk wakimshona kwa interview kutokana na nafasi yake itakuwa Shida kidogo.
Maana kuwajibu kila swali na HAPA KAZI TUU itakuwa kazi kwelikweli
Basi maraisi wote sio maana hata Lowasa alichapia kama mtoto wa Nursery alipohojiwa kwa kiingereza.

Lugha sio Kigezo,China,Comoro,Japan,Korea,Maraisi wao wengi wanatumai lugha zao nje ya Nchi

Ushamba unakuwa mzigo,siku hizi kuna mashine zinauzwa tena ndogo tu zina tafsiri bila kuwa na mtafsiri.Dunia inakupita kwa kasi sana mkuu
 
"Ili kuweza kupanda ndege usafiri masafa marefu yahitajika uwe na afya njema haswa moyo" alisisitiza daktari bingwa wa magonjwa ya moyo...mwisho wakunukuu
 
Marco Sata naye alikuwa hapendi mwisho alienda kutibiwa huko na mauti ikamkuta, siyo wote wanapenda kwenda Ulaya.
 
Marco Sata naye alikuwa hapendi mwisho alienda kutibiwa huko na mauti ikamkuta, siyo wote wanapenda kwenda Ulaya.


Lkn Raisi Sata aliishi Ulaya kabla ya kuwa Raisi hivyo namuelewa lkn Raisi Magufuli wetu hajawahi kuishi Ulaya na bado hapapatikii na hiyo ndiyo tofauti!
 
Binafsi Raisi Magufuli ananishangaza sana mpaka nafikia hatua ya kuhoji Uafrika wake!
Maishani mwangu sijawahi kukutana na Mwafrika asiyepapatikia kwenda Ulaya, (nchi za Wazungu), na hii huwa ni ndoto yetu watoto wa Kiafrika wkt tukuapo kwenda Ulaya!

Sasa hapa kuna Mwafrika aliyezaliwa na kukulia Afrika ingawaje ana uwezo wa kwenda Ulaya muda wowote kama akiamua na kufikia Hoteli yoyote ya gharama yoyote ile na kwenda shopping ya kufa mtu, pmj na haya yote bado hafagilii kwenda Ulaya?

Hili limenistaajabisha sana, Mwafrika asipende kwenda Ulaya pmj na kuwa na huo uwezo?
Yaani Mwafrika akatae kwenda kutibiwa Ulaya kwenye Hospitali ya Mzungu?
Mwafrika mwenye uwezo amuamini Mwafrika kumtibu?
Mwafrika mwenye uwezo asile chakula cha Kizungu badala yake Mke wake ndiyo ampikie?

Hapana Mimi nafikiri Raisi Magufuli siyo Mwafrika labda tumefichwa tu!


Tanzania tumepata rais mzalendo na mwenye mapenzi ya ukweli na watanzania wenzake si wale waliopita. Kuna rais mmoja hivi nakumbuka yeye kila safari isiyo ya lazima kwake kwenda alikuwa anakwenda na kundi la watu wasio muhimu ili mradi tu kawapeleka kutoa ushamba.
 
Hata Mimi sipendi kwenda Uarabuni kwa vile lugha yao siijui.
Sasa JPM hata yeye kila akifikiri kuwa akifika kule kisha CNN, BBC, Skynews nk wakimshona kwa interview kutokana na nafasi yake itakuwa Shida kidogo.
Maana kuwajibu kila swali na HAPA KAZI TUU itakuwa kazi kwelikweli
I have never seen such an uninformed comment. When Ji xipin, Putin, Franco hollande and many other leaders whose countries do not use english go to Europe, what language do they use? Have you witnessed AU or UN assemblies in session? What happens concerning language? IDIOT.
 
Hivi wewe unadhani Rais akienda ulaya anafaidi nini ambacho anakikosa akiwa hapo Magogoni?
Mimi au wewe tukienda ulaya tunafaidi zaidi kwani tuna Uhuru wa kwenda popote, club, michezoni, madanguro ,casino nk mradi hela yako tuu.
Viongozi wanaokimbilia huko huwa wanafuata kuangalia vitega uchumi vyao huyu hana bado
Mbona mkwere alikuwa ana paa sana,na hatuna kitega uchumi chochote cha maana?
 
Kwa hili la kutulia nyumbani na kushughulikia matatizo ya ndani kwa dhati kabisa namsifu sana (pamoja na kuwepo kwa makosa/changamote za hapa na pale). Kwa mfano, approach yake kwenye uchumi (hasa macro) inabidi aitizame kwa makini (anahitaji washauri).

Binafsi naamini mojawapo ya sababu za mtangulizi wake kuboronga ilikuwa ni safari za nje. Kwa namna alivyokuwa anasafiri kwenda nje, ilikuwa ni vigumu kwake kuona matatizo ya ndani. Lakini kubwa ambalo lilikuwa linanikera ni pamoja na kwenda kote huko nje haonekani kama alikuwa anapata "wivu" wa kuleta nyumbani hayo mazuri anayoyaona huko nje.
 
Lugha mkuu
Wewe ni kilaza kweli, kwani akienda na kuongea kiswahili kuna tatizo?? Hivi unajua marais wa France, Russia, China, Japan etc hawajui kiingereza na hawamind na wakienda popote pale wanaongea lugha zao?? Jiongeze ndg yangu.lugha sio tatizo kabisa,.
 
I have never seen such an uninformed comment. When Ji xipin, Putin, Franco hollande and many other leaders whose countries do not use english go to Europe, what language do they use? Have you witnessed AU or UN assemblies in session? What happens concerning language? IDIOT.

Hivi wewe huwa unasoma na comments zingine au unarukia moja tuu? Hizo lugha za kwao hao wanazotumia hata shule wamesomea hizo, huyu kasomea lugha gani? Mbona wazito wa kuelewa nyinyi kinachojadiliwa?
 
Back
Top Bottom