Hivi Rais Magufuli ni Mwafrika kweli?

Hivi Rais Magufuli ni Mwafrika kweli?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,838
Binafsi Raisi Magufuli ananishangaza sana mpaka nafikia hatua ya kuhoji Uafrika wake!
Maishani mwangu sijawahi kukutana na Mwafrika asiyepapatikia kwenda Ulaya, (nchi za Wazungu), na hii huwa ni ndoto yetu watoto wa Kiafrika wkt tukuapo kwenda Ulaya!

Sasa hapa kuna Mwafrika aliyezaliwa na kukulia Afrika ingawaje ana uwezo wa kwenda Ulaya muda wowote kama akiamua na kufikia Hoteli yoyote ya gharama yoyote ile na kwenda shopping ya kufa mtu, pmj na haya yote bado hafagilii kwenda Ulaya?

Hili limenistaajabisha sana, Mwafrika asipende kwenda Ulaya pmj na kuwa na huo uwezo?
Yaani Mwafrika akatae kwenda kutibiwa Ulaya kwenye Hospitali ya Mzungu?
Mwafrika mwenye uwezo amuamini Mwafrika kumtibu?
Mwafrika mwenye uwezo asile chakula cha Kizungu badala yake Mke wake ndiyo ampikie?

Hapana Mimi nafikiri Raisi Magufuli siyo Mwafrika labda tumefichwa tu!
 
Binafsi Raisi Magufuli ananishangaza sana mpaka nafikia hatua ya kuhoji Uafrika wake!
Maishani mwangu sijawahi kukutana na Mwafrika asiyepapatikia kwenda Ulaya, (nchi za Wazungu), na hii huwa ni ndoto yetu watoto wa Kiafrika wkt tukuapo kwenda Ulaya!

Sasa hapa kuna Mwafrika aliyezaliwa na kukulia Afrika ingawaje ana uwezo wa kwenda Ulaya muda wowote kama akiamua na kufikia Hoteli yoyote ya gharama yoyote ile na kwenda shopping ya kufa mtu, pmj na haya yote bado hafagilii kwenda Ulaya?

Hili limenistaajabisha sana, Mwafrika asipende kwenda Ulaya pmj na kuwa na huo uwezo?

NCHI HAINA HERA SASA AKIAMUA KWENDA ULAYA WAKATI MWAKAHUU TUNATAKIWA KULIPA TRILLION 8 ZA MADENI YALIYOIVA NA WAKATI MISHAHARA YA SERIKILI NI TRILLION 7.2 UNADHANI MAMBO YATAENDA KWELI
 
pmj ndio nani mkuu...naona umeghafilika...ulishasikia putin kuzuruzuru marekani au Africa???

Magufuli is Pure Pan Africanist..May GOD bless his vision....

viva Thomas Sankara; Samora Machel; Amilcar Cabral; Patrice Lumumba; Mwalimu Nyerere; Steve Biko...

Now Africa has Magu the great...
 
Hata Mimi sipendi kwenda Uarabuni kwa vile lugha yao siijui.
Sasa JPM hata yeye kila akifikiri kuwa akifika kule kisha CNN, BBC, Skynews nk wakimshona kwa interview kutokana na nafasi yake itakuwa Shida kidogo.
Maana kuwajibu kila swali na HAPA KAZI TUU itakuwa kazi kwelikweli
 
Kuna tofauti kubwa sana hapa, kwenda Uarabuni siyo ndoto ya Mwafrika, ila Ulaya binafsi ni mara ya kwanza kuona Mwafrika wa hivi, ndiyo maana siamini kama kweli ni Muafrika!
 
Mtamsema na kumkashifu saana!. Lkn ukweli utabaki palepale...., Magu iz da President....
 
Binafsi Raisi Magufuli ananishangaza sana mpaka nafikia hatua ya kuhoji Uafrika wake!
Maishani mwangu sijawahi kukutana na Mwafrika asiyepapatikia kwenda Ulaya, (nchi za Wazungu), na hii huwa ni ndoto yetu watoto wa Kiafrika wkt tukuapo kwenda Ulaya!

Sasa hapa kuna Mwafrika aliyezaliwa na kukulia Afrika ingawaje ana uwezo wa kwenda Ulaya muda wowote kama akiamua na kufikia Hoteli yoyote ya gharama yoyote ile na kwenda shopping ya kufa mtu, pmj na haya yote bado hafagilii kwenda Ulaya?

Hili limenistaajabisha sana, Mwafrika asipende kwenda Ulaya pmj na kuwa na huo uwezo?
Mkuu Baribaro, JPM ni Pan Africanist na nadhani alilia Ghadafi alipouliwa na wale ma imperialists !.

Tuko wengi na JPM peke yake ila sisi wengine angalau tulijaribu, kwa upande wangu nilianzia UK kisha nikaenda US na kuamua kurudi nyumbani by choice, ila kutokana na ule Uafrika wa mambo yetu yale, kote nimeacha familia, hivyo kuwajibika kwenda sio kwa sababu ya kushobokea ulaya, bali kutimiza tuu wajibu wa kutembelea familia.

Pasco
 
Duh! Kweli mkuu ni mmajumui wa kiafrika yaani hata Londoni hapataki?

Mwanzoni nlijua ni zuga za siasa lakini mwaka sasa umekatika. Loh!
 
Kuna tofauti kubwa sana hapa, kwenda Uarabuni siyo ndoto ya Mwafrika, ila Ulaya binafsi ni mara ya kwanza kuona Mwafrika wa hivi, ndiyo maana siamini kama kweli ni Muafrika!
Hivi wewe unadhani Rais akienda ulaya anafaidi nini ambacho anakikosa akiwa hapo Magogoni?
Mimi au wewe tukienda ulaya tunafaidi zaidi kwani tuna Uhuru wa kwenda popote, club, michezoni, madanguro ,casino nk mradi hela yako tuu.
Viongozi wanaokimbilia huko huwa wanafuata kuangalia vitega uchumi vyao huyu hana bado
 
Hakuna shida. Fanya utafiti kuhusu asili yake kisha utuhabarishe.
 
Hata Mimi sipendi kwenda Uarabuni kwa vile lugha yao siijui.
Sasa JPM hata yeye kila akifikiri kuwa akifika kule kisha CNN, BBC, Skynews nk wakimshona kwa interview kutokana na nafasi yake itakuwa Shida kidogo.
Maana kuwajibu kila swali na HAPA KAZI TUU itakuwa kazi kwelikweli
Unaona mbali sana….
 
Hivi wewe unadhani Rais akienda ulaya anafaidi nini ambacho anakikosa akiwa hapo Magogoni?
Mimi au wewe tukienda ulaya tunafaidi zaidi kwani tuna Uhuru wa kwenda popote, club, michezoni, madanguro ,casino nk mradi hela yako tuu.
Viongozi wanaokimbilia huko huwa wanafuata kuangalia vitega uchumi vyao huyu hana bado

Lkn hayo unayajua baada ya kujaribu, yaani ningeelewa kama Raisi Magufuli kabla ya kuwa Raisi angekuwa keshaimaliza Ulaya na raha zake tuziaminizo Waafrika, lkn ukiangalia Historia ile tuijuayo hajawahi kuishi huko, sasa hili kwa Mwafrika wa kawaida ni ngumu kuamini!

Kumbuka wengine mpaka wanafungiwa na Wazungu kwenda huko kama Mugabe lkn anazuga na kuibukia UN New York, ndiyo maana nasema Raisi Magufuli amenishangaza sana kwani Mwafrika wa hivi sijawahi kuona!
 
Hata mm nashangaa hawa watakuwa viongozi wa ajibu sijawahi kusikia mfalme wa Saudi Arabia akija afrika, rais wa Finland, Norway, Pakistan, Brazil Uzbekistan wakuja africa wakati wakijua wazi Afrika ni shamba la bibi!
 
Hata Mimi sipendi kwenda Uarabuni kwa vile lugha yao siijui.
Sasa JPM hata yeye kila akifikiri kuwa akifika kule kisha CNN, BBC, Skynews nk wakimshona kwa interview kutokana na nafasi yake itakuwa Shida kidogo.
Maana kuwajibu kila swali na HAPA KAZI TUU itakuwa kazi kwelikweli
Upo dunia ya kale mkuu. Rais wa China akienda hizo nchi anaojiwa kwa lugha gani? Anaweza kwenda kule na akafanya mahojiano kwa lugha yake, hao wanaomuhoji watatafuta mkalimani na yeye anakuwa na wa kwake. Kwa nafasi yake anaweza kufanya chochote, anaweza kujibu kwa kisukuma na hakuna shida. Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa UK anajifunza kiswahili darasani huku wewe unakidharau ni utumwa tu unatusumbua.
 
Lkn hayo unayajua baada ya kujaribu, yaani ningeelewa kama Raisi Magufuli kabla ya kuwa Raisi angekuwa keshaimaliza Ulaya na raha zake tuziaminizo Waafrika, lkn ukiangalia Historia ile tuijuayo hajawahi kuishi huko, sasa hili kwa Mwafrika wa kawaida ni ngumu kuamini!

Kumbuka wengine mpaka wanafungiwa na Wazungu kwenda huko kama Mugabe lkn anazuga na kuibukia UN New York, ndiyo maana nasema Raisi Magufuli amenishangaza sana kwani Mwafrika wa hivi sijawahi kuona!
Ila wewe Barbarosa unawatafutia watu Kisutu bure! Kuna mtu atakuja kutiririka hapa kuhusu ule uvumi wa sijui moyo, mara mashine, mara safari ndefu za ndege na ngurumo yake, sijui ugonjwa na, aah basi bwana mie simo kwaheri! hata mie mgonjwa ndio maana napenda sana kusafiri na gari mpaka dharula ndio naenda angani tena safari isiyozidi saa 2
 
Tuongelee hoja zamsingi bana.sio eti Mara jpm haendi ulaya, mara jpm hajui inglish,huo ni ufinyu wamawazo wandugu.mtoa hoja mwenyewe hata kuliandika jina la rais lenyewe hajui.sasa ndo kitugani hicho kama sio ujinga,kwanza wewe unadhani leo ukipanda pipa na kwenda ulaya utakapo rudi bongo utakuwa umebadilika kitu chochote?rahasha utabaki kuwa vilevile tu.acha ushamba tuulize tulie enda tukuambie.na hii tabia ya kumwongelea jpm kwenye mada za upuuzi kama hii nakemea kabisa.
 
Upo dunia ya kale mkuu. Rais wa China akienda hizo nchi anaojiwa kwa lugha gani? Anaweza kwenda kule na akafanya mahojiano kwa lugha yake, hao wanaomuhoji watatafuta mkalimani na yeye anakuwa na wa kwake. Kwa nafasi yake anaweza kufanya chochote, anaweza kujibu kwa kisukuma na hakuna shida. Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa UK anajifunza kiswahili darasani huku wewe unakidharau ni utumwa tu unatusumbua.
OK mie wa kale, hivi huyo wa CNN akimuuliza "your exellency, how come you learn to the level of doctorate (Phd) with english language then you cant use it?" Atajibuje kwa kiswahili au kisukuma?
Huyo wa China umsemaye kasoma kwa kichina.
Hata hapa kwetu tukimpa cheo hicho Lusinde akienda huko ataongea na kujibu kiswahili na hakuna atakayeshangaa kutokujua lugha hiyo kwa vile hajasomea.
Umeipata mantiki ya hoja?
 
Back
Top Bottom