Uchaguzi 2020 Hivi Rais Magufuli kuwaahidi nafasi za uteuzi akina Andrew Chenge, siyo kutonesha kidonda kwa mamilioni ya vijana wasiokuwa na Ajira?

Sasa ulitaka nani ahaidi ni kweli hata iweje magufuli ndio rais ajaye ana haki ya kuahidi hata asipopata wataelewa
 
Kuna shida kubwa kwenye kampeni zake...hili la kuahidi vyeo kwa watu waliovimbiwa ukwasi na ambao umri umesonga ni kasoro kubwa sana
Cheo sio lazima iwe paid job, watu kama kina Anna ,Chenge na wabunge ambao umri umesonga wanaweza kupewa KAZI za kushauri,au watoto wao kuteuliwa na Rais kama ahsante au kifuta machozi..Refer Ile ahadi ya 50m kila kijiji..Rais alishasema pesa hiyo aliitoa indirectly kupitia miradi mbalimbali...SASA kama anaweza kutuliza kijiji kizima atashindwa kutuliza individuals kama kina Masele?!
 
Kwenye mitukano maana sio mikutano ya chadema viongozi wa chadema huwa wanamuita Lisu Rais mleta mada hujaliona hilo??

Nadhani mleta mada pia hafahamu umuhimu wa kuwa na wazee , wale Wana offer kitu kinaitwa experience, ni muhimu kuwa nao.

Nadhani umeona hasara za kutokuwa na watu wenye uzoefu huko Chadema ambako ni matusi tu na mihemko hakuna busara yeyote.
 
strubapost: 36720184 said:
Kwenye mitukano maana sio mikutano ya chadema viongozi wa chadema huwa wanamuita Lisu Rais mleta mada hujaliona hilo??
Kwani kuna ubaya gani kwa mashabiki wako kukuita Rais mgombea wao?
 
Magufuli ametudharau sisi Raia na wapiga kura. Anaelewa fika kuwa sisi ndiyo tumempa ajira na sasa anatunisha msuli wakati maombi yake ya kuongeza mkataba yako mezani na sisi ndiyo waamuzi.
La muhimu ni kuviweka sawa sawa vichinjio vyetu, ili ifikapo hapo Oktoba 28 mwaka huu, tukakamilishe zoezi la kumng'oa Jiwe, kwenye sanduku la kura!
 
Wananchi wanakuja kusikiliza Sera nzuri kwenye mikutano ya Chadema.......

Siyo kama mikutano yenu ya chama, ambapo Mwenyekiti wenu kila anapofanya mkutano wa kampeni, anaendelea tu kuwasifu wanawake weupe!
 
Sentensi yako ya Pili apo ndo ujue sasa something fishy is good to come well planned
 
Nilimshangaa kupita maelezo, nikasema huyu mtu ni heartless or clueless of peoples condition, hajali au hajui hali ya watu wa nchi hii.

kwa saabu hata kibinadamu tu, unahutubia mbele ya maelefu na maelfu ya wasio na kazi, wakulima na wafanya biashara ndogondogo, waendesha bodaboda ambao wengine wana na madgree, unawaeleza habari ya kina Chenge wasigombane "vyeo viko vingi sana...."

Vyeo viko vingi unawaambia ulio nao jukwaani, na hawa halaiki walio mbele yako, wasijikieje ????

Wananchi wanaokuja kumsikiliza mikoani huko yani yeye anawaona interest zao ni kujengewa vyoo vya stendi, wasifukuzwe na mgambo wanapouza ndizi, kuchimbiwa visima vya vijijini na kero ya kulipishwa michango ya primary school....

Maana hawezi kwenda sehemu bila kusema "hapa sijaona mmebeba masinia ya viazi vya kuchemsha mnauza"! Uzeni karanga, uzeni mahindi ya kuchemsha! Anawadharau sana Watanzania, anachojua yeye kazi nzuri ni kwa akina Chenge na Tibaijuka. Anajua Chenge na Tibaijuka wameshashiba lakini anawahonga ma vyeo ili wamsaidie ku control chama na madaraka yake! Very selfish guy!
 
Aisee kuna mziki unachezwa kimyakimya.midundo inatokea mbaaaaali kupitia clips.maana ambako angeona disko live amewafokea.

Polepole alitwambia wote kuwa,kampeni za mwaka huu wanazifanya kidikitali.kumbe ni mwendo wa YOUTUBE WHASAP n.k

Kwa hiyo acha ajipe moto maana ni yeye tu atakae weka rekod ambayo hakuna rais atakaeivunja kwa kurud chato kwa kuongoza 5yrs only.

Na ajiandae kisaikolojia ambapo katiba itabadirishwa na aombe mungu asije juta.

Ngoja nikanywe MBEGE kwa Mama D.loading........
 
Huyu jamaa hatoondoka Ikulu kwa sanduku la kura. NEC yenyewe imejaa maafisa usalama ambao bila shaka yoyote wanareport na kupokea maagizo kutoka Gogoni kabla ya kutangaza chochote
 
Toka uandike maada hii umekuwa mzee zaidi ya ulivyokuwa ulipofikiria kuandika-POLE SANA- kama unaamini katika ubaguzi kwa misingi ya umri
 
Hata hao kina Chenge ni dharau tu inayotokana na kuamini anaweza kumnunua mtu yoyote.
 
Inaweza ikawa sio sawa kufanya hivyo lakini na wewe jifunze kutofautisha kati ya teuzi za kisiasa na ajira za utumishi wa umma.
Usiwe kama wale wanaona mtu mwenye umri ambao kweli ni mkubwa kateuliwa kuwa balozi nje, wao wanasema kwanini wasipewe vijana waliomaliza vyuo lakini hawana ajira.
 
Magu lazima amalize awamu zake zote, hapa tunasumbuana na kutafuta ahueni ya maon ya watu tu, au Tanzania sisi ni wageni, Magu ni rais na ataendelea, ingewezekana kusingekuwa na election tu, haya maneno utayakumbuka mwenye uzi wakat ukifika bado sio parefu.
 
Elimu yetu inatutengeneza ukimaliza chuo uajiriwe, na taasisi, serikal au mtu flan, huu utegemez mbaya sana..ndo unaotuletea shida, kipind hik cha Magu kimefundisha sana watu, kwamba acha kwenda shule ukitegemea kuja kuajiriwa na serikal, utakufa na pressure, Be ur self, utachukia watu sana na wasiokuwa na hatia.
 
Hajachaguliwa ila anaahidi watu vyeo, anaona kazi za serikali ni za kuhongana kishamba hivyo.
Kweli naamini kauli ya Nape jamaa ni Mshamba sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…