Uchaguzi 2020 Hivi Rais Magufuli kuwaahidi nafasi za uteuzi akina Andrew Chenge, siyo kutonesha kidonda kwa mamilioni ya vijana wasiokuwa na Ajira?

Kuna shida kubwa kwenye kampeni zake...hili la kuahidi vyeo kwa watu waliovimbiwa ukwasi na ambao umri umesonga ni kasoro kubwa sana
Cheo sio lazima iwe paid job, watu kama kina Anna ,Chenge na wabunge ambao umri umesonga wanaweza kupewa KAZI za kushauri,au watoto wao kuteuliwa na Rais kama ahsante au kifuta machozi..Refer Ile ahadi ya 50m kila kijiji..Rais alishasema pesa hiyo aliitoa indirectly kupitia miradi mbalimbali...SASA kama anaweza kutuliza kijiji kizima atashindwa kutuliza individuals kama kina Masele?!
 
Kwenye mitukano maana sio mikutano ya chadema viongozi wa chadema huwa wanamuita Lisu Rais mleta mada hujaliona hilo??

Nadhani mleta mada pia hafahamu umuhimu wa kuwa na wazee , wale Wana offer kitu kinaitwa experience, ni muhimu kuwa nao.

Nadhani umeona hasara za kutokuwa na watu wenye uzoefu huko Chadema ambako ni matusi tu na mihemko hakuna busara yeyote.
 
strubapost: 36720184 said:
Kwenye mitukano maana sio mikutano ya chadema viongozi wa chadema huwa wanamuita Lisu Rais mleta mada hujaliona hilo??
Kwani kuna ubaya gani kwa mashabiki wako kukuita Rais mgombea wao?
 
Magufuli ametudharau sisi Raia na wapiga kura. Anaelewa fika kuwa sisi ndiyo tumempa ajira na sasa anatunisha msuli wakati maombi yake ya kuongeza mkataba yako mezani na sisi ndiyo waamuzi.
La muhimu ni kuviweka sawa sawa vichinjio vyetu, ili ifikapo hapo Oktoba 28 mwaka huu, tukakamilishe zoezi la kumng'oa Jiwe, kwenye sanduku la kura!
 
Kwenye mitukano maana sio mikutano ya chadema viongozi wa chadema huwa wanamuita Lisu Rais mleta mada hujaliona hilo??

Nadhani mleta mada pia hafahamu umuhimu wa kuwa na wazee , wale Wana offer kitu kinaitwa experience, ni muhimu kuwa nao.

Nadhani umeona hasara za kutokuwa na watu wenye uzoefu huko Chadema ambako ni matusi tu na mihemko hakuna busara yeyote.
Wananchi wanakuja kusikiliza Sera nzuri kwenye mikutano ya Chadema.......

Siyo kama mikutano yenu ya chama, ambapo Mwenyekiti wenu kila anapofanya mkutano wa kampeni, anaendelea tu kuwasifu wanawake weupe!
 
Yaani huwa najaribu kuwaza, hivi huyu Magufuli anaelewa kweli kuwa yupo katika kampeni?

Utawezaje kuwaahidi vyeo watu, wakati huelewi kama utashinda uchaguzi huo au laa?

Kwanza huo mchakamchaka, anaoendeshwa na Lissu, siyo wa kawaida!

Mathalani tuchukulie, ameshindwa kwenye uchaguzi huu, hivi hivyo vyeo anavyowaahidi kina Chenge, atawapa akina Chenge, atakapokuwa Chato, akiwa Rais mstaafu?

Hii ni sawasawa na ule msemo wa wahenga, unaosema USIMTUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO
Sentensi yako ya Pili apo ndo ujue sasa something fishy is good to come well planned
 
Nilimshangaa kupita maelezo, nikasema huyu mtu ni heartless or clueless of peoples condition, hajali au hajui hali ya watu wa nchi hii.

kwa saabu hata kibinadamu tu, unahutubia mbele ya maelefu na maelfu ya wasio na kazi, wakulima na wafanya biashara ndogondogo, waendesha bodaboda ambao wengine wana na madgree, unawaeleza habari ya kina Chenge wasigombane "vyeo viko vingi sana...."

Vyeo viko vingi unawaambia ulio nao jukwaani, na hawa halaiki walio mbele yako, wasijikieje ????

Wananchi wanaokuja kumsikiliza mikoani huko yani yeye anawaona interest zao ni kujengewa vyoo vya stendi, wasifukuzwe na mgambo wanapouza ndizi, kuchimbiwa visima vya vijijini na kero ya kulipishwa michango ya primary school....

Maana hawezi kwenda sehemu bila kusema "hapa sijaona mmebeba masinia ya viazi vya kuchemsha mnauza"! Uzeni karanga, uzeni mahindi ya kuchemsha! Anawadharau sana Watanzania, anachojua yeye kazi nzuri ni kwa akina Chenge na Tibaijuka. Anajua Chenge na Tibaijuka wameshashiba lakini anawahonga ma vyeo ili wamsaidie ku control chama na madaraka yake! Very selfish guy!
 
Aisee kuna mziki unachezwa kimyakimya.midundo inatokea mbaaaaali kupitia clips.maana ambako angeona disko live amewafokea.

Polepole alitwambia wote kuwa,kampeni za mwaka huu wanazifanya kidikitali.kumbe ni mwendo wa YOUTUBE WHASAP n.k

Kwa hiyo acha ajipe moto maana ni yeye tu atakae weka rekod ambayo hakuna rais atakaeivunja kwa kurud chato kwa kuongoza 5yrs only.

Na ajiandae kisaikolojia ambapo katiba itabadirishwa na aombe mungu asije juta.

Ngoja nikanywe MBEGE kwa Mama D.loading........
 
Huyu jamaa hatoondoka Ikulu kwa sanduku la kura. NEC yenyewe imejaa maafisa usalama ambao bila shaka yoyote wanareport na kupokea maagizo kutoka Gogoni kabla ya kutangaza chochote
 
Tulimsikia alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni, huko Bariadi akimuahidi Mzee Andrew Chenge, ambaye alishinda kura za maoni jimboni kwake, kuwa atampa nafasi "nzuri" ya uteuzi, miongoni ya nafasi zake nyingi za uteuzi, kwa sharti tu la kumwuunga mkono mgombea "wao" wa vikao vya juu vya Central Committee!

Aliamua kumuahidi nafasi hiyo ya uteuzi, kama afanyavyo Mwalimu anapoamua kumzawadia pipi, mtoto wa shule ya chekechea!

Alifanya vivyo hivyo alipofika Shinyanga mjini, ambapo alimuahidi Stephen Masele, nafasi ya uteuzi, kwa kuwa amegundua kuwa jimbo hilo, kuna hatari kubwa sana, ya kulipoteza na kwenda upinzani, baada ya vikao vya juu vya chama cha CCM "kupindua" maamuzi ya wajumbe, kwa kumteua Petrobas Katambi, ambaye aliachwa mbali sana, katika kura hizo za maoni.

Wananchi wamekuwa wakijiuliza, ikiwa Rais Magufuli anaamini kuwa ana nafasi nyingi za uteuzi, ni kwanini asitumie nafasi hizo, kumteua "kipenzi" chake Katambi?

Vivyo vivyo alipofika Biharamulo, akamuahidi Anna Tibaijuka, ambaye alitangaza mwenyewe kuwa kutokana na umri wake kuwa mkubwa, anastaafu siasa, na kuamua kuanza kula pensheni yake.

Lakini cha ajabu Rais Magufuli akaamua "kumlazimisha" huyo mama wa "vijisenti vya mboga" kuwa eti bado a anamuhitaji, kwa hiyo ataendelea kumtumia kwenye nafasi nyingine.

Kwanza mimweleze Rais Magufuli kuwa hivi sasa yeye ni mgombea, kama walivyo wagombea wengine, kwa hiyo siyo vyema kuamua kuahidi kutoa vyeo wakati akijua yupo kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi, ambapo anaweza kushinda, lakini vile vile wananchi wanaweza wasimpe kura za kutosha na hivyo anaweza kung'olewa kwenye nafasi hiyo ya Urais, na asiwe Rais wa awamu ya sita na atakuwa Rais mstaafu.

Hivi nimuulize Rais Magufuli, hivi akishindwa kwenye uchaguzi huu wa mwaka huu, hivyo vyeo anavyowaahidi hao "wakereketwa" wa chama chake, atawazawadia akiwa Chato kwake, akiwa Rais mstaafu?

Kwa vile huu ni uchaguzi, kuna kushinda na kushindwa, iweje yeye akiwa mgombea kama walivyo wagombea wengine, akina Tundu Lissu, ajihakikishie uhakika wa asilimia 100, wa kushinda uchaguzi huu?

Au yeye Rais Magufuli anaamini kuwa ni lazima atashinda, hata kama kura hazitatosha, kwa kuwa Tume ya uchaguzi itakayotangaza matokeo hayo ni "yake" aliyoiteua?

Vile vile kuna hoja nyingine kubwa, kama yeye Rais Magufuli anafahamu kuwa idadi ya vijana wanaomaliza vyuo vikuu na kupata degree zao ni kwa maelfu, ambao hawana kazi, iweje sasa, awaahidi nafasi za kuteuliwa hao "wazee" waliostaafu na kuanza kula pensheni zao, wakati akiwaacha "solemba" vijana hao, ambao kutwa kucha wanazunguka na CV zao bila mafanikio yoyote?

Hivi unawezaje kumhakikishia nafasi ya uteuzi Mzee Andrew Chenge, ambaye amekuwa akifanya kazi, tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, wakati kuna vijana wengi kwa maelfu."wakisota" wakiwa hawana ajira zozote?

Hivi hii hali ya Rais Magufuli, kuahidi kutoa nafasi ya kuwateua hao makada wa CCM, kama siyo mazingira ya utoaji rushwa wakati wa uchaguzi, tuiite nini?
Toka uandike maada hii umekuwa mzee zaidi ya ulivyokuwa ulipofikiria kuandika-POLE SANA- kama unaamini katika ubaguzi kwa misingi ya umri
 
Nilimshangaa kupita maelezo, nikasema huyu mtu ni heartless or clueless of peoples condition, hajali au hajui hali ya watu wa nchi hii.

kwa saabu hata kibinadamu tu, unahutubia mbele ya maelefu na maelfu ya wasio na kazi, wakulima na wafanya biashara ndogondogo, waendesha bodaboda ambao wengine wana na madgree, unawaeleza habari ya kina Chenge wasigombane "vyeo viko vingi sana...."

Vyeo viko vingi unawaambia ulio nao jukwaani, na hawa halaiki walio mbele yako, wasijikieje ????

Wananchi wanaokuja kumsikiliza mikoani huko yani yeye anawaona interest zao ni vyoo vya stendi, kufukuzwa na mgambo wanapouza ndizi, visima vya vijiji na kulipishwa michango ya primary school....

Maana hawezi kwenda sehemu bila kusema hapa sijaona mmebeba masinia ya viazi vya kuchemsha mnauza! Uzeni! Anawadharau sana Watanzania, anachojua yeye kazi nzuri ni kwa akina Chenge na Tibaijuka. Anajua Chenge na Tibaijuka wameshashiba lakini anawahonga ma vyeo ili wamsaidie ku control chama na madaraka yake! Very selfish guy!
Hata hao kina Chenge ni dharau tu inayotokana na kuamini anaweza kumnunua mtu yoyote.
 
Inaweza ikawa sio sawa kufanya hivyo lakini na wewe jifunze kutofautisha kati ya teuzi za kisiasa na ajira za utumishi wa umma.
Usiwe kama wale wanaona mtu mwenye umri ambao kweli ni mkubwa kateuliwa kuwa balozi nje, wao wanasema kwanini wasipewe vijana waliomaliza vyuo lakini hawana ajira.
 
Magu lazima amalize awamu zake zote, hapa tunasumbuana na kutafuta ahueni ya maon ya watu tu, au Tanzania sisi ni wageni, Magu ni rais na ataendelea, ingewezekana kusingekuwa na election tu, haya maneno utayakumbuka mwenye uzi wakat ukifika bado sio parefu.
 
Elimu yetu inatutengeneza ukimaliza chuo uajiriwe, na taasisi, serikal au mtu flan, huu utegemez mbaya sana..ndo unaotuletea shida, kipind hik cha Magu kimefundisha sana watu, kwamba acha kwenda shule ukitegemea kuja kuajiriwa na serikal, utakufa na pressure, Be ur self, utachukia watu sana na wasiokuwa na hatia.
 
Hajachaguliwa ila anaahidi watu vyeo, anaona kazi za serikali ni za kuhongana kishamba hivyo.
Kweli naamini kauli ya Nape jamaa ni Mshamba sana.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom