Kuna sarakasi nyingi zinaendelea hapa tanzania nadhani zimezidi hata zile kungfu wanazocheza kina jakchang na kina donen kwa watazamaji wa move za kichina na kikorea wananelewa sana.
kwa wewe usiyefurahisha macho kwa kuangalia move za aina hii kwasababu ya kile unachokiita ubize wa kazi acha nikudokeze kidogo tabia ya move hizi; hizi move kama hujui kazi ya computer unaweza kusema kile unachokiona ndo ukweli kabisa maana kwa kweli hazina chembe ya uigizaji kwa kuzitazama japo ni uigizaji zinafanana na ukweli mtupu. utajua tu ni za uongo pale utakapoona kwenye move donen kafa lakini kwenye uhalisia yuko hai!
Wengi hapa wanalalama ndani ya mioyo yao kwani huyu muandishi anataka kusema nini? mbona mara atuletee mabo jackchang mara Don En kwanini Jamii forum ni jukwaa la move za kichina? la hasha! nataka tu uelewe kwamba wapo waigizaji nguli ambao maigizo yao ni kama ukweli unapoyatazama na hayatii shaka kuyaamini.
Sasa nataka turudi Tanzania yenye mahakama ya mafisadi, viwanda, kila mwalimu laptop, million hamsini na mengine mengi. Ni juzi tu hapa tumeambiwa nchi imevunja record ya tangu uhuru wake kwa kukusanya mapato makubwa kwa mwezi January-February......Sasa nakuuliza wewe uliyeko hapa mjini tu Goba je maji yamekufikia? sitaki kumuuliza wa Mdimba maana naweza kumuamshia machungu anayojaribu kusahaulishwa.
Ni hivi majuzi tu tumeambiwa watoto wa vigogo wamerithishana BOT naukuuliza Mr Don En the master himself umewachukulia hatua gani?
Tuliambiwa serikali iliyopita mafisadi walikua wanakamatwa alafu wanacheleweshwa kuhukumiwa! nakuuliza Master Don En wale wa nyumba sabini ni muda gani tangu utuonyeshe kwenye fimbo yako ya mkono wa kulia (vyombo vya habari) hawajachukuliwa hatua na tayari tunasahaulishwa?
Mdanganyika amka kabla panya buku hawajamaliza kula mguu wako huku wakikupuliza usisikie maumivu. tuliambiwa mama ntilie na bodaboda watatengenezewa mazingira mazuri ya kufanya kazi zao bila bugudha jamani mama ntilie na bodaboda nijibuni mko salama?
Sitaki kuzungumzia ya dada Jesca nisije nikaonekana nashupalia, lakini najiuliza hivi kuna Cinema bora iliyotoka mwaka 2016 kuliko hii? yaani kwa ujasiri namuita Juma bumbuazi kilaza kumbe Salma wangu ni hamna kitu! kwakweli hiki ni kiwango kikubwa sana cha uigizaji, watu wa aina hii walipaswa kwa hapa kwetu kufidia nafasi ya Kanumba Mungu "ampuumzishe kwa amani"
Najiuliza, hivi koki ilipofunguliwa kwa amri ya waziri nani aliwajibishwa na kwasababu gani wakati Don the legend himself alisema siangalii mtu uson ukifanya uzembe unakwenda utupishe tuchape kazi?mhhh hapa nabaki nikiguna tu na kusema usipostaajabia ya musa subiri uyaone ya firauni..
Lakini mdanganyika mimi kuna saa najiuliza hivi ni kweli nina akili finyu kiasi chakuchezewa move zoote hizi alafu sishtuki? saa nyingine najiuliza au nimepuliziwa dawa ya usingizi?
Ee Mungu nisaidie niamke nianze kuwaza upya.