Hivi rais Magufuli amemtendea nini masikini mpaka sasa?

Watanzania wanatabia kama za wanywaji pombe kwani kila bar mpya ikifunguliwa huamia huko kwa kutegemea kutakuwa na huduma mpya na tofauti lkn loooo baada ya siku 3 utawasikia wakilalama
 
Ivi ushuru kwa mitandao simu (mobile money transactions) umekua kiasi gan vile ??
 
JMP anatengeneza mfumo ambao utasaidia kuwawezesha mtanzania yoyote kupata haki yake na kufanikiwa bila kujali kipato chake. Mfano: Elimu bure, Afya access kwa bima na wazee bure, Kubana matumizi kwa ajili hizo helazitumike kupeleka maji vijijini navitu vingi tu. Tunatakiwa kukumbuka tulipotoka kwani watu walikuwa wanapewa huduma kutokana na surname zao.
Unakosea hapo kwenye neno mfumo, wewe sema magufuli anapambana pekee yake habari za mfumo hapo umechemka sana
 
Genghis Khan mfumo Ni sheria, Sheria Ni Katiba!, Katiba bora Ni ile itokanayo Na maoni ya wananchi (rejea rasimu ya Warioba inayowapa wananchi nguvu ya kikatiba kuwajibisha wawakilishi wao iwapo watazingua), Katiba bora ni ile inayolipa bunge mamlaka kamili ya kuisimamia serikali, Ni wapi uncle Magu amethubutu kushawishi wananchi/bunge viwe Na nguvu ya kuhoji/kuisimamia serikali?, Kama hakuna basi Ni mfumo gani anaoujenga ambao mwenzetu umeuona?, hakuna na haijawahi kutokea duniani mfumo wa mtu mmoja Tu kufanya Kila kitu kwa ajili ya watu wote Na akafanikiwa!. Tunahitaji mfumo wa kitaasisi ambao msingi wake ni demokrasia ya kweli inayompa mwanachi wa kawaida haki ya kupongeza, kukosoa, kuhoji, Na kusikilizwa katika misingi ya kisheria. Tofauti na hayo tutaishia kila siku kufanya tendo la kijinga la kumuombea mtu kwa Mungu wakati Mungu huyohuyo katupa akili ya kujua mema na mabaya ili tuweze kufanya maamuzi sahihi!.
 
Kuna sarakasi nyingi zinaendelea hapa tanzania nadhani zimezidi hata zile kungfu wanazocheza kina jakchang na kina donen kwa watazamaji wa move za kichina na kikorea wananelewa sana.

kwa wewe usiyefurahisha macho kwa kuangalia move za aina hii kwasababu ya kile unachokiita ubize wa kazi acha nikudokeze kidogo tabia ya move hizi; hizi move kama hujui kazi ya computer unaweza kusema kile unachokiona ndo ukweli kabisa maana kwa kweli hazina chembe ya uigizaji kwa kuzitazama japo ni uigizaji zinafanana na ukweli mtupu. utajua tu ni za uongo pale utakapoona kwenye move donen kafa lakini kwenye uhalisia yuko hai!

Wengi hapa wanalalama ndani ya mioyo yao kwani huyu muandishi anataka kusema nini? mbona mara atuletee mabo jackchang mara Don En kwanini Jamii forum ni jukwaa la move za kichina? la hasha! nataka tu uelewe kwamba wapo waigizaji nguli ambao maigizo yao ni kama ukweli unapoyatazama na hayatii shaka kuyaamini.

Sasa nataka turudi Tanzania yenye mahakama ya mafisadi, viwanda, kila mwalimu laptop, million hamsini na mengine mengi. Ni juzi tu hapa tumeambiwa nchi imevunja record ya tangu uhuru wake kwa kukusanya mapato makubwa kwa mwezi January-February......Sasa nakuuliza wewe uliyeko hapa mjini tu Goba je maji yamekufikia? sitaki kumuuliza wa Mdimba maana naweza kumuamshia machungu anayojaribu kusahaulishwa.

Ni hivi majuzi tu tumeambiwa watoto wa vigogo wamerithishana BOT naukuuliza Mr Don En the master himself umewachukulia hatua gani?

Tuliambiwa serikali iliyopita mafisadi walikua wanakamatwa alafu wanacheleweshwa kuhukumiwa! nakuuliza Master Don En wale wa nyumba sabini ni muda gani tangu utuonyeshe kwenye fimbo yako ya mkono wa kulia (vyombo vya habari) hawajachukuliwa hatua na tayari tunasahaulishwa?

Mdanganyika amka kabla panya buku hawajamaliza kula mguu wako huku wakikupuliza usisikie maumivu. tuliambiwa mama ntilie na bodaboda watatengenezewa mazingira mazuri ya kufanya kazi zao bila bugudha jamani mama ntilie na bodaboda nijibuni mko salama?

Sitaki kuzungumzia ya dada Jesca nisije nikaonekana nashupalia, lakini najiuliza hivi kuna Cinema bora iliyotoka mwaka 2016 kuliko hii? yaani kwa ujasiri namuita Juma bumbuazi kilaza kumbe Salma wangu ni hamna kitu! kwakweli hiki ni kiwango kikubwa sana cha uigizaji, watu wa aina hii walipaswa kwa hapa kwetu kufidia nafasi ya Kanumba Mungu "ampuumzishe kwa amani"

Najiuliza, hivi koki ilipofunguliwa kwa amri ya waziri nani aliwajibishwa na kwasababu gani wakati Don the legend himself alisema siangalii mtu uson ukifanya uzembe unakwenda utupishe tuchape kazi?mhhh hapa nabaki nikiguna tu na kusema usipostaajabia ya musa subiri uyaone ya firauni..

Lakini mdanganyika mimi kuna saa najiuliza hivi ni kweli nina akili finyu kiasi chakuchezewa move zoote hizi alafu sishtuki? saa nyingine najiuliza au nimepuliziwa dawa ya usingizi?

Ee Mungu nisaidie niamke nianze kuwaza upya.
Acha porojo urais ni miaka mitano, sasa unatoa hukumu hata mwaka haujaisha
 
natamani Baba Jesca angepitia na huku siku moja asome vilio vya waliomuweka ikulu. Abadili mfumo ,badala ya Clouds 360 ambapo wanamsifu tu apite na huku napo aone. Inawezekana bado ana nia njema ambayo hatujaiona bado maana haijawahi tokea mtu aliepokelewa kwa shangwe kubwa kulalamikiwa kiasi hiki chini ya mwaka mmoja tu wa utawala.
 
Kuna watu wanaishi kama malaika nataka waishi kama mashetani.Badala ya kuwapa masikini (mashetani) uwezo wa kuishi kama malaika (matajiri) unawafanya na matajiri ma wao wawe masikini.
 
Hizo ni kati ya maneno mapya kwenye matumizi ya lugha ya kila siku kwa watanzania
 
Na huyo aliyemaliza miaka 10 amemtendea nini masikini mbona huulizi hilo
 
Genghis Khan mfumo Ni sheria, Sheria Ni Katiba!, Katiba bora Ni ile itokanayo Na maoni ya wananchi (rejea rasimu ya Warioba inayowapa wananchi nguvu ya kikatiba kuwajibisha wawakilishi wao iwapo watazingua), Katiba bora ni ile inayolipa bunge mamlaka kamili ya kuisimamia serikali, Ni wapi uncle Magu amethubutu kushawishi wananchi/bunge viwe Na nguvu ya kuhoji/kuisimamia serikali?, Kama hakuna basi Ni mfumo gani anaoujenga ambao mwenzetu umeuona?, hakuna na haijawahi kutokea duniani mfumo wa mtu mmoja Tu kufanya Kila kitu kwa ajili ya watu wote Na akafanikiwa!. Tunahitaji mfumo wa kitaasisi ambao msingi wake ni demokrasia ya kweli inayompa mwanachi wa kawaida haki ya kupongeza, kukosoa, kuhoji, Na kusikilizwa katika misingi ya kisheria. Tofauti na hayo tutaishia kila siku kufanya tendo la kijinga la kumuombea mtu kwa Mungu wakati Mungu huyohuyo katupa akili ya kujua mema na mabaya ili tuweze kufanya maamuzi sahihi!.
Upo sawa kuwa mfumo ni sheria lakin sheria zizopo tumeshindwa kusimamia leo hii unaweka sheria nyingine tutaweza kuzisimamia kweli. Leo wabunge wetu wengi wanajali maslahi yao wenye kwanza bila kujali wananchi waliowachagua, kutojali watoto wa majimboni kwano wanasoma chini ya miti au kukaa chini. Nilitegea kuona wabunge wanajitolea kutengeneza madawati na kuhasisha watu julitolea kuchangia vitanda mahospitaline. Lakini ukija uchangauzi wabunge ni wakwanza kutume email na msg kuomba mchango kwa ajili za kampeni zao.
 
Kuna sarakasi nyingi zinaendelea hapa tanzania nadhani zimezidi hata zile kungfu wanazocheza kina jakchang na kina donen kwa watazamaji wa move za kichina na kikorea wananelewa sana.

kwa wewe usiyefurahisha macho kwa kuangalia move za aina hii kwasababu ya kile unachokiita ubize wa kazi acha nikudokeze kidogo tabia ya move hizi; hizi move kama hujui kazi ya computer unaweza kusema kile unachokiona ndo ukweli kabisa maana kwa kweli hazina chembe ya uigizaji kwa kuzitazama japo ni uigizaji zinafanana na ukweli mtupu. utajua tu ni za uongo pale utakapoona kwenye move donen kafa lakini kwenye uhalisia yuko hai!

Wengi hapa wanalalama ndani ya mioyo yao kwani huyu muandishi anataka kusema nini? mbona mara atuletee mabo jackchang mara Don En kwanini Jamii forum ni jukwaa la move za kichina? la hasha! nataka tu uelewe kwamba wapo waigizaji nguli ambao maigizo yao ni kama ukweli unapoyatazama na hayatii shaka kuyaamini.

Sasa nataka turudi Tanzania yenye mahakama ya mafisadi, viwanda, kila mwalimu laptop, million hamsini na mengine mengi. Ni juzi tu hapa tumeambiwa nchi imevunja record ya tangu uhuru wake kwa kukusanya mapato makubwa kwa mwezi January-February......Sasa nakuuliza wewe uliyeko hapa mjini tu Goba je maji yamekufikia? sitaki kumuuliza wa Mdimba maana naweza kumuamshia machungu anayojaribu kusahaulishwa.

Ni hivi majuzi tu tumeambiwa watoto wa vigogo wamerithishana BOT naukuuliza Mr Don En the master himself umewachukulia hatua gani?

Tuliambiwa serikali iliyopita mafisadi walikua wanakamatwa alafu wanacheleweshwa kuhukumiwa! nakuuliza Master Don En wale wa nyumba sabini ni muda gani tangu utuonyeshe kwenye fimbo yako ya mkono wa kulia (vyombo vya habari) hawajachukuliwa hatua na tayari tunasahaulishwa?

Mdanganyika amka kabla panya buku hawajamaliza kula mguu wako huku wakikupuliza usisikie maumivu. tuliambiwa mama ntilie na bodaboda watatengenezewa mazingira mazuri ya kufanya kazi zao bila bugudha jamani mama ntilie na bodaboda nijibuni mko salama?

Sitaki kuzungumzia ya dada Jesca nisije nikaonekana nashupalia, lakini najiuliza hivi kuna Cinema bora iliyotoka mwaka 2016 kuliko hii? yaani kwa ujasiri namuita Juma bumbuazi kilaza kumbe Salma wangu ni hamna kitu! kwakweli hiki ni kiwango kikubwa sana cha uigizaji, watu wa aina hii walipaswa kwa hapa kwetu kufidia nafasi ya Kanumba Mungu "ampuumzishe kwa amani"

Najiuliza, hivi koki ilipofunguliwa kwa amri ya waziri nani aliwajibishwa na kwasababu gani wakati Don the legend himself alisema siangalii mtu uson ukifanya uzembe unakwenda utupishe tuchape kazi?mhhh hapa nabaki nikiguna tu na kusema usipostaajabia ya musa subiri uyaone ya firauni..

Lakini mdanganyika mimi kuna saa najiuliza hivi ni kweli nina akili finyu kiasi chakuchezewa move zoote hizi alafu sishtuki? saa nyingine najiuliza au nimepuliziwa dawa ya usingizi?

Ee Mungu nisaidie niamke nianze kuwaza upya.
Wewe kalia kutaka kutendewa mwisho utatendwa wewe
 
Unakosea hapo kwenye neno mfumo, wewe sema magufuli anapambana pekee yake habari za mfumo hapo umechemka sana
Nitakwambia mm binafsi nilijaribu kuomba kurenew passport ilinichukuwa week mbili, nenda rudi. Leo hii asante kwa JMP wafanyakazi wale wale nimeweza kupata hudumu zote kwa masaa matatu tu. Hii inaonyesha mfumo upo lakin watu walikuwa hawatekelezi wajibu wao. Tumpe muda na ushirikiano, Utaona hata wazee wetu huko vijijini ukienda kuwatembelea hawakuombe tena hela ya kupombe badala yake watakuwa wanakupa offer ww uliyotoka mjini.
 
Mkuu unaongelea kilo moja ya chumvi kwenye bahari ya hindi, hapa tanzania tuna mahitaji mengi sana tena muhimu kuliko hiyo pasipoti unayo ipigia vigeregere
 
Wewe kalia kutaka kutendewa mwisho utatendwa wewe
Ndiyo tatizo lenu wana-CCM yaani mtu akikosoa utendaji wenu basi mnamuona ni kituko wakati huo ugumu wa maisha tunaupata wote
 
Back
Top Bottom