Hivi pantoni ni Meli au si meli?

Pantoni ni kivuko - ‘moving bridge’ kinachotumika umbali mfupi kuvusha vitu/watu. Ni daraja linalotembea (mara nyingi kinatembea mbele au nyuma, hakihitaji kugeuka)

Meli ni kwa ajili ya masafa marefu na huwa ina ‘mbele’ na ‘nyuma’

Nifahamuvyo mimi, wataalamu wanaweza kufafanua zaidi
 
Kwa wanaojua ningependa kufafanuliwa kuhusu hii Mada maana tumebishana Sana na Wana mbeya wenzangu ambao hata pantoni hatujawahi kupanda🤣🤣 kwa upande wangu niliwajibu kuwa pantoni ni Meli basi kila mtu akawa anasema lake..... Ufafanuzi kwa wanaofahamu pantoni ni nini jamani nipate kuwaeleimisha Hawa wananzengo wenzangu.
Hilo ni Daraja la kuvukia linaloelea.Panton na meli ni vitu viwili tofauti
 
Hata hizi tunazoziita meli kuanzia ziwa victoria hadi kule bahari ya hindi nyingi ni FERRYBOAT.
Tanzania Cruise ship, merchant ship na warship ni chache mno hata vidole vya mkono wa kushoto ni vingi.
Ile tuliokuwa tunaita meli ya spice na skygic nilipoangalia CNN na al jazeera waliripoti ni TRAGEDY OF FERRYBOAT IN TANZANIA.
eti unakuta unaambiwa meli imebeba watu 500,meli!!!!

mazafantaz.
moja likaja kushusha gari za dangote karibia gari 300,nikatamani niite watu waje waone meli sasa.
 
eti unakuta unaambiwa meli imebeba watu 500,meli!!!!

mazafantaz.
moja likaja kushusha gari za dangote karibia gari 300,nikatamani niite watu waje waone meli sasa.
Ukisikia kitu inaitwa MELI either ni cruiseship, au ni warship au ni merchatship humo ndani unasafiri toka sehemu moja kwenda nyingine kwa LIFT, escalator au bodaboda au baiskeli.
Cruiseship ni kama ile ya Titanic ile ndo meli tena kwa ukubwa ile TITANIC ni moja wapo ya meli ndogo zipo kubwa kushinda TITANIC.
Ndani ya TITANIC kutoka sehemu moja kwenda nyingine baiskeli ilikuwa inatumika.
Sasa mjinga mmoja anatuambia hata zile AZAM FAST FERRIES eti zile ni meli.....
Hapa bongo meli ni chache sana. Labla za akina MAERSK zile ni merchant ship meli za mizigo.
 
Back
Top Bottom