Hivi nitajuaje kama nimelogwa?

Wana JF hebu msaidieni mwenzenu, msimdhihaki. Kitendo cha yeye kuuliza atajuaje amelogwa ni wazi kinaonyesha kuna kitu amekihisi kama labda kalogwa. Mtoa mada nakushauri uende kwa wale waombaji wa ukweli (sio wale wanaoringia upako). Ukiombewa kwa Jina la Yesu, na kama umelogwa, mapepo yatajidhihirisha yatatolewa. Usiende kwa mganga kamwe. Unaweza kwenda kwa mganga akakueleza vitu vya siri vya undani kabisa ambavyo hakuna hata mtu mwingine yeyote anavijua ila wewe. Lakini hili halimaanishi kwamba atakuponya. Mganga kama huyo ana roho ya utambuzi ya hali ya juu. Lakini yuko chini ya shetani huyo huyo aliyemeta mchawi aliyekuloga. Anayeweza kukuondolea uchawi uliovikwa ni Yesu Kristo peke yake. Haijalishi kama wewe ni dini ingine au huna dini kabisa. Yesu Kristo anawaponya WOTE walio na nia ya kuponywa, na wanaomwamini kwamba ana uwezo wa kuponya.
 
Back
Top Bottom