Hivi nini kigezo cha mji kuwa na hadhi ya Jiji?

Kama suala ndo hilo basi mji wa Njombe umejengeka kwa ramani kuliko Dar. Kwa hiyo Dar haina hadhi ya jiji bali Njombe. Msiwe mapungu.ani kupima hadhi ya mji kwa macho. Mbeya ni jiji kwa kuwa linastahili. Sasa mnaiponda Mbeya badala ya kuponda jiji lenye makazi ya ovyo kama kwa Mtogole, na miundombinu mibovu kama Sinza na eneo chafu kama Kariakoo.
Kama ndivyo mwasema hata Dar siyo jiji. Lakini kama mwatumia vigezo, tazama vigezo alotoa Green City ndo utaijua Mbeya siyo ya kuipimia.
Halafu tuheshimiane kuilinganisha Mbeya na mikusanyiko ya makazi ya Kahama na Singida.
 
Ni kweli kwa mtazamo wako haswa kama vigezo vya mahala kuwa mji, wilaya au jiji ingetokana na test/ utashi fulani wa mtu basi hata haya unayoyasema ingekuwa hivyo. ndugu yangu nimeona wengi wamechangia sana lakini kwa kuongeza vigezo ni pamoja na idadi ya watu, makusanyo ktk halmashauri husika, lakini pia sikukatalii sana kwa nchi kama zetu kipo pia kigezo cha utashi wa wanasiasa wetu. kwa jiji la mbeya ni vigumu sana kwa mtu anaeingia kwa mara kwanza kuona picha halisi, na wengi wamekuwa mara kadhaa na mtazamo wa kwako kwani wamekuwa tu wakiamini mbeya ni kijiji kikubwa na wala sio jiji, mfano ni kutokana na kuzagaa hovyo hovyo kwa wamachinga, usafi kufanyika ktk njia moja tu ya highway kiasi cha maeneo mengi mfano kata kama ya ilemi, nzovwe na hata iyela kuwa ktk hali mbaya. pia lipo tatizo la watu wenyewe kuwa wenyeji zaidi (too local) kitu kinachowapelekea kushindwa kutumia fursa zilizopo vizuri zaidi kuhakikisha wanatoa hudumu ya kutosha, mfano ikifika saa moja huwezi kuta huduma ya hotel popote zaid ya baa, na zenyewe ni chache.
 
QUOTE]Quote from fakenology
Ukweli mi kwamba mbeya sio jiji.
wamebambikwa jina hilo ili wenyeji wasihame uko kuja kwenye majiji kamili.
Kiufupi wamezugwa.
Halafu wenyeji wake cio wote ila wengi wao wanahitilafu kichwani cmaanish ni vichaa ila wanamatatizo kichwani kidogo, fuatilia kwa umakini utaligundua hilo.
Naipongeza serikali kwa kuliona hilo maana mtaani kwetu wapo w3 ni shida kwelkwel je wangekua 10 c tungehama mtaa.
Bila kusahau rangi zao, ni bora wakae hukohuko.
Eti mby jj. Haina radio wal tv inayobrodcast country wide.[/QUOTE]
Quote from luhala
Nakubaliana nawe katika moja tu, kwamba uamuzi wa kuufanya mji wa Mbeya jiji ulikuwa wa kisiasa zaidi kuliko uhalisia wenyewe. Kwamba wana hitilafu kichwani sijui wala sielewi umetumia kipimo gani kuligundua hilo kwani mimi nawaona miongoni mwao wako walio makini kuliko wewe na wenzako wenye mawazo yanayofanana nawe. Kama wapo humu walioshiriki katika mchakato wa kuufanya mji wa Mbeya jiji kabla ya Tanga, Iringa, Dodoma na hata Morogoro wajitokeze watueleze vigezo walivyotumia. Inashangaza kwelikweli kuona jiji halina hata hoteli moja ya 5 Stars, kiwanja cha ndege hakikuwepo wakati linatangazwa, hakuna hata kituo kimoja cha Televisheni wala redio kinachotangaza kitaifa, na hata baadhi ya huduma za kibenki ni lazima uende Dar kuzikamilisha!
UNISOME KWA MAKINI HAPA:
1.Population: Mbeya ni ya tatu baada ya mwanza na dsm.
Kwa hilo sina takwimu, sina hoja.
2. Huduma za afya: mbeya(rufaa) inahudumia mikoa ya iringa, rukwa, songea
Moshi pia ipewe hadhi ya jiji kwa vile ipo hospitali ya rufaa kwa ajili ya kanda nzima ya kaskazini (KCMC)?
3. huduma za fedha: mbeya ni kati ya mikoa 5 yenye B.O.T tangu awamu ya pili.
Bado sijaunganisha uhusiano wa BOT na uteuzi wa mahala kuwa jiji
4. Transportation: mbeya ina aina zote za usafiri kama reli, barabara, maji kwa ziwa nyasa na rukwa, ndege n.K.
Sikuwa nafahamu kwamba jiji la Mbeya lina usafiri wa aina zote; yaani barabara, maji, reli na ndege!
5. Financial inst: mbeya ina zaid ya aina 15 za mabenk.
Dodoma kuna Financial Inst. zaidi ya hizo, ipewe hadhi ya jiji?
6. Elimu: mbeya ni ya 2 kwa wingi wa shule za a-level. Na ya 3 kwa o-level.
Kwa hili pia sina takwimu, lakini ninavyoamini hesabu yako inajumuisha shule zilizoko wilayani!
7. Biashara: mbeya inamiliki bourder kubwa kuliko zote tanzania.
Nashindwa kuelewa ni mkoa au mji wa Mbeya unaomiliki bourders hizo?
8. Mapato: T.R.A Mkoa wa mbeya imekuwa ikivuka malengo ya ukusanyaji kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
Kama mapato ni kigezo, basi maeneo ya Ilala, Temeke na Kinondoni yapewe hadhi za majiji kwa vile
yanachangia sehemu kubwa ya mapato kitaifa.

9. Nyakyusa: ni kabila la nne kwa ukubwa baada ya sukuma, chaga, na haya.
Kigezo hiki ni cha ovyo kabisa na hakihusiani na uteuzi wa jiji. Isitoshe ninavyofahamu wanyakyusa
hawatoki Mbeya bali Tukuyu!

10. Urban area: mbya mjini ina makazi ya kudumu mengi ikifuatia kwa mwanza baada ya dsm.
Hili pia sina takwimu, inawezekana.
11. Chakula: mbeya is the greatest food producer in tanzania.
If so the our next cities shall be Sumbawanga, Iringa and Songea!
 
acha ukilaza! Mwza au arusha au Dar ilipopewa sifa ya jiji ni hotel gan ilikuwa 5star?
Kuna redio gan ya kitaifa pale tanga au arusha hadi kuwa jiji?
Ni huduma gani ya benk uliyokosa mbeya ukaifuata dar?
Kwa iyo mikoa mingne ulotaja ndo ina cfa za kuwa jiji?
Amka wewe, fungua TAMISEMI ujue vigezo nilivyotaja ktk post ya juu vinavyotumika.

Hapa ndio nimeona ushabiki wako kuliko ukweli.Arusha imekuwa na hotel zenye hadhi kubwa sambamba na Dar es salaam kabla Arusha haijawa jiji.Kihalisia miji mingi imepewa hadhi ya jiji kisiasa tu.

Majiji yenye hadhi hiyo hapa Tanzania (pamoja na mapungufu mengi ya miji hiyo) ni Arusha na Mwanza tu (ukitoa Dar ).Arusha na Mwanza zimezidiana ukubwa na population lakini huduma nyingi ni sawa ingawa upande wa barabara upanuzi uliofanyika Mwanza umebadili kabisa sura ya jiji hilo.

Leo miji yenye uwezo wa ku accomodate ugeni wowote mkubwa bila kuelemewa ni Dar na Arusha tu!leo mechi ya Simba na Yanga ikichezwa Mbeya au Tanga utasikia mpaka guest zimefurika hakuna nafasi! kuna jiji hapo! Dodoma wabunge tu hawatoshi! Miji kama Tanga,Mbeya haina sifa za kuwa jiji hata kibongo bongo na hii haiitaji takwimu bali macho tu ukifika ktk miji hiyo.
Mwanza na Arusha ndio miji yenye unafuu kwa huduma nyingi na Arusha kutopewa hadhi ya jiji mapema ni changamoto tu kulifanya liwe na hadhi inayostahili sababu ya nafasi ya jiji hilo ktk huduma za kimataifa na si sababu Mbeya na Tanga ni zaidi ya Arusha loh!
 
QUOTE]Quote from fakenology
Ukweli mi kwamba mbeya sio jiji.
wamebambikwa jina hilo ili wenyeji wasihame uko kuja kwenye majiji kamili.
Kiufupi wamezugwa.
Halafu wenyeji wake cio wote ila wengi wao wanahitilafu kichwani cmaanish ni vichaa ila wanamatatizo kichwani kidogo, fuatilia kwa umakini utaligundua hilo.
Naipongeza serikali kwa kuliona hilo maana mtaani kwetu wapo w3 ni shida kwelkwel je wangekua 10 c tungehama mtaa.
Bila kusahau rangi zao, ni bora wakae hukohuko.
Eti mby jj. Haina radio wal tv inayobrodcast country wide.
[/QUOTE]

kaka usichukulie kigezo kimoja kimoja bali muunganiko wa vingi!
Na c kila kigezo kiwe ndan ya manispaa hucka, uwepo wa vigezo vya kiuchumi wilayani ndio mapato ya mkoa mzima, hivyo makao makuu huweza kupewa hadhi kubwa.
Unadhan kwanin wilaya za dsm zinajenga jiji moja? Bla shaka ni vigezo vilivyogo ktk wilayj hucka.
 
Ni kweli kwa mtazamo wako haswa kama vigezo vya mahala kuwa mji, wilaya au jiji ingetokana na test/ utashi fulani wa mtu basi hata haya unayoyasema ingekuwa hivyo. ndugu yangu nimeona wengi wamechangia sana lakini kwa kuongeza vigezo ni pamoja na idadi ya watu, makusanyo ktk halmashauri husika, lakini pia sikukatalii sana kwa nchi kama zetu kipo pia kigezo cha utashi wa wanasiasa wetu. kwa jiji la mbeya ni vigumu sana kwa mtu anaeingia kwa mara kwanza kuona picha halisi, na wengi wamekuwa mara kadhaa na mtazamo wa kwako kwani wamekuwa tu wakiamini mbeya ni kijiji kikubwa na wala sio jiji, mfano ni kutokana na kuzagaa hovyo hovyo kwa wamachinga, usafi kufanyika ktk njia moja tu ya highway kiasi cha maeneo mengi mfano kata kama ya ilemi, nzovwe na hata iyela kuwa ktk hali mbaya. pia lipo tatizo la watu wenyewe kuwa wenyeji zaidi (too local) kitu kinachowapelekea kushindwa kutumia fursa zilizopo vizuri zaidi kuhakikisha wanatoa hudumu ya kutosha, mfano ikifika saa moja huwezi kuta huduma ya hotel popote zaid ya baa, na zenyewe ni chache.

hata ukifikia jijin dar maeneo ya tandale, manzese, na maeneo ya kigogo utasema dar sio jiji, vivyo ukiwa jijin arusha maeneo ya mbauda, ngusero, matejoo nk, utasema arusha ni kijiji.
Mwanza cjafika!
 
Hapa ndio nimeona ushabiki wako kuliko ukweli.Arusha imekuwa na hotel zenye hadhi kubwa sambamba na Dar es salaam kabla Arusha haijawa jiji.Kihalisia miji mingi imepewa hadhi ya jiji kisiasa tu.

Majiji yenye hadhi hiyo hapa Tanzania (pamoja na mapungufu mengi ya miji hiyo) ni Arusha na Mwanza tu (ukitoa Dar ).Arusha na Mwanza zimezidiana ukubwa na population lakini huduma nyingi ni sawa ingawa upande wa barabara upanuzi uliofanyika Mwanza umebadili kabisa sura ya jiji hilo.

Leo miji yenye uwezo wa ku accomodate ugeni wowote mkubwa bila kuelemewa ni Dar na Arusha tu!leo mechi ya Simba na Yanga ikichezwa Mbeya au Tanga utasikia mpaka guest zimefurika hakuna nafasi! kuna jiji hapo! Dodoma wabunge tu hawatoshi! Miji kama Tanga,Mbeya haina sifa za kuwa jiji hata kibongo bongo na hii haiitaji takwimu bali macho tu ukifika ktk miji hiyo.
Mwanza na Arusha ndio miji yenye unafuu kwa huduma nyingi na Arusha kutopewa hadhi ya jiji mapema ni changamoto tu kulifanya liwe na hadhi inayostahili sababu ya nafasi ya jiji hilo ktk huduma za kimataifa na si sababu Mbeya na Tanga ni zaidi ya Arusha loh!

hata ukifikia jijin dar maeneo ya tandale, manzese, na maeneo ya kigogo utasema dar sio jiji, vivyo ukiwa jijin arusha maeneo ya mbauda, ngusero, matejoo nk, utasema arusha ni kijiji.
Mwanza cjafika!
 
Tatizo la wengine wakiambiwa jiji wanajenga picha ya Dar es Salaam vichwani mwao. Hata hawajui wakati hiyo Dar ikipewa hadhi ya jiji ilikuwa inafananaje! Ni sawa na kufananisha chuo kikuu kilichoanza kabla ya mwaka 1980 na kilichoanza baada ya mwaka 2000.
Nadhani vigezo na masharti vilizingatiwa.
Arusha ilipewa hadhi hiyo then ikanyang'anywa kutokana na uchafu wa jiji. Waliambiwa warekebishe then wanarudishiwa hadhi yao.
 
MAJIJI YA TANZANIA NI 1.DAR , 2. MWANZA, 3. ARUSHA, 4. MBEYA, 5.TANGA. Inawezekana wengi humu ni vijana wa juzijuzi au hamjatembea miji mingi ya Tanzania hivyo inakuwa ngumu kuelewa mambo. kwa wanaokumbuka Mwanza ilipewa hadhi ya jiji wakati barabara zake nyingi ni za vumbi,na pia haikuwa na hotel yeyote ya maana, Vigezo vilivyotumika kuipa hadhi ya jiji vilikuwa ni idadi ya watu,mtawanyiko wa makazi ya kudumu,na pato(makusanyo ya mji) vyote hivyo vitatu mji wa Mwanza ulikuwa wa pili nyuma ya Dar. barabara nzuri na Mahotel mazuri na Majengo mazuri yaliyopo sasa mjini Mwanza vimekuja baadaye sana. baada ya Mwanza kupewa hadhi ya jiji miaka kadhaa baadaye Mbeya,arusha na Tanga nazo ziliomba kupewa hadhi hiyo,waombaji wa mikoa hii kuwa jiji pamoja na mambo mengine walibase kwenye vigezo vilevile vilivyotumika kuipa Mwanza hadhi hiyo, yaani Idadi ya watu kwenye miji hiyo,mtawanyiko wa makazi,na pato, baada ya serikali kuchambua kwa umakini vigezo hivyo iliguandua kwamba,baada ya Dar na Mwanza miji uliokuwa unafuatia kwa vigezo hivyo ni Mby na Tanga hivyo ikaitangaza Mby na Tanga kuwa Majiji,Arusha ilinyimwa sababu haikukidhi kegezo cha idadi ya watu mjini na mtawanyiko wa makazi kuwa mdogo.(kwa wanaofuatilia mambo hata mji wa moshi mwaka jana uliomba kupewa hadhi hiyo ya jiji lkn ukanyimwa kwa kigezo hichohicho kilichoibania Arusha kipindi hicho).
NB. Inawezekana kabisa kwamba kwa sasa kuna miji mingine ambayo haikupewa hadhi ya kuwa jiji lkn kwa sasa tayari ina vigezo vyote vya kupewa,kama we ni mkazi wa mji huo na unahisi mji huo unakidhi vigezo usisite kuwashauri wahusika wapeleke maombi ya kupewa hadhi ya jiji.
 
Nafikiri kila nchi labda ina vigezo vyake
Ukienda uganda ukiacha kampala majiji mengine ni aibu
Ila kwa macho tu mbeya haioni ndani kwa dodoma na moshi
kigezo kikubwa kwa mbeya ni wingi wa watu,
umri wa mji sio kigezo mwanza ina umri mkubwa kushinda nairobi lakini angalia tofauti
kinachoifanya mbeya ionekane kama kijiji nyumba za watu nyingi ni za tope, hakuna majengo
makubwa ya kuvutia. Kahama si ya kudharau ni wilaya inayokua kwa kasi tatizo la miji mingi ya
kanda ya ziwa watu wake hukimbilia kujenga na kustarehe mwanza.
 
tunataka tujue idadi ya watu wanaotakiwa kwa namba kwa sababu mwanza imepewa hadhi ya jiji ikiwa na watu kati ya laki sita na nane. mbeya mpaka sasa haina idadi hiyo ya watu, sipingi mbeya kuwa jiji ila nataka kujua idadi kiasi gani inatakiwa ili mji uwe jiji?
Kwa taarifa tu arusha sio jiji kwa sababu ya kigezo cha eneo wakitatua hilo mambo yatakuwa poa, walipewa halafu baadaye wakanyang'anywa kimya kimya wengi hawajui hilo, sasa hapa napo sijui zinahitajika km ngapi za mraba ili mji uwe jiji tufahamishane,
 
UNISOME KWA MAKINI HAPA:
1.Population: Mbeya ni ya tatu baada ya mwanza na dsm.
hapa unazungumzia halmashauri ya mji wa mbeya au unazungumzia mkoa wa mbeya maana unaonekana wewe hata hujui hata tofauti ya mkoa na mji
2. Huduma za afya: mbeya(rufaa) inahudumia mikoa ya iringa, rukwa, songea
hlo ni zuga kama ingekuwa kuna hospitali ya rufaa na muhimbili huwa wanakuja wagonjwa toka huko kufanyaje
3. huduma za fedha: mbeya ni kati ya mikoa 5 yenye B.O.T tangu awamu ya pili.
kutokana mamgawanyiko wa kanda hakukuwa na namna zaidi ya kuiweka huko ili kusaidia mzunguko na mtawanyiko wa fedha
4. Transportation: mbeya ina aina zote za usafiri kama reli, barabara, maji kwa ziwa nyasa na rukwa, ndege n.K.
ndege gani inayotua mbeya bora hata shinyanga precision inatuwa mbeya vinatua vile vindege vya watu 12 napo utasema kuna usafiri wa ndege wanazidiwa hata na kigoma
5. Financial inst: mbeya ina zaid ya aina 15 za mabenk.
ukujumlisha na saccos sawa
6. Elimu: mbeya ni ya 2 kwa wingi wa shule za a-level. Na ya 3 kwa o-level.
hapa unazungumzia jiji la mbeya au mkoa wa mbeya maana inaonekana wewe kwako ukisikia jiji basi unajua ni mkoaludi darasa la 4 kasome tena uraia
7. Biashara: mbeya inamiliki bourder kubwa kuliko zote tanzania.
hapa sina uhakika
8. Mapato: T.R.A Mkoa wa mbeya imekuwa ikivuka malengo ya ukusanyaji kwa zaidi ya miaka 10 sasa.
mimi nazungumzia jiji sio mkoa
9. Nyakyusa: ni kabila la nne kwa ukubwa baada ya sukuma, chaga, na haya.
nyamwezi je?,hehe je?
10. Urban area: mbya mjini ina makazi ya kudumu mengi ikifuatia kwa mwanza baada ya dsm.
nyumba zenyewe ndio hizo za tope?
11. Chakula: mbeya is the greatest food producer in tanzania
pale mjini sijaona mashamba.
jiji gani halina hata hotel ya 3 stars
 
Nimejiuliza hili baada ya kuona hapa kwetu Tanzania Majiji yanaongezeka kila uchao,ni jambo zuri ila sijajua huwa duniani kuna kigezo kipi huwa kinapandisha hadhi ya mji kwenda kua jiji,je ni ukubwa Wa mji?majengo,?barabara?au huduma za jamii?

Masikio yangu yamezoea kusikia maneno kama Jiji la Tokyo, Washington DC,Berlin, Johannesburg, Paris,Singapore, London,Nairobi,Dar es salaam,Kampala nk

Lakini pia niliwahi kuishi Bahrain na Mji wa Muscat Oman ambapo si pakubwa saana lakini ni miji iliyosheheni mambo mengi ya hadhi ya kimataifa maana kule gulf wanasema wao wapo second world kimiundo mbinu ni Mji msafi wenye barabara bora zenye interchange na flyovers zaidi ya 20 lakini bado sikuwahi kusikia wakiita City/Jiji...hii imenichabganya na kutaka kujua kigezo ni nini?
 
Majiji hata kuwa uchochoro wa London hayana hiyo sifa yaan afriza taabu kwl kwl
 
Vizuri sikuwahi kujua kama Uzi kama huu uliwahi kuja hapa
 
Back
Top Bottom