Mada yako haina mvuto! Ila kuna vimiji vingine Bongo vimepewa hadhi ya jiji kwa sababu za kisiasa! Mfano Mbeya, yaani mji watu wanalala saa 10 jioni, hamna hata klabu ya usiku ya maana eti nalo ni jiji! Phew!!!
Hivi Arusha na Mbeya wapi pana staili kuwa JIJI?
bora arusha! Pako laivu zaidi na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa!
Je mnafahamu kuwa na Moshi iko mbioni kuwa jiji? Uongozi wa Manispaa katika malengo yake ya miaka 10 ijayo ni kuwa Moshi ipate hadhi ya jiji, ukifika ofisi za manispaa pale Moshi kuna bango kubwa limeandikwa malengo yao. Na kwa kweli, kwa waliofika Moshi zamani, wakienda sasa hivi kuna tofauti kubwa
1. Mji wa Moshi toka zamani ulipangika vizuri, una mitaa ya kueleweka, alternative routes kibao
2. Mji ni msafi
3. Huduma za jamii za kueleweka: maji (ni nadra sana usikie eti eneo fulani Moshi halina huduma ya maji), barabara sasa hivi kwa kiasi kikubwa ni lami safi, ile tabia ya mji kwenda kulala baada ya saa 11 haipo tena, sehemu za starehe kwa wingi (kinachosubiriwa sasa ni jumba la sinema ambalo nimesikia linafunguliwa siku za karibuni) nk
4. Vyuo kwa wingi: KCMC, MUCCoBS, Mwenge, Mweka, Sebastian Moshi etc... hivi vimechangia sana kuongeza idadi ya wakaazi na kuuchangamsha mji, pia magari (not necessarily an indicator of progress/ development) yameongezeka na sasa hivi si tu zile 504 na pickup zilizozoeleka zamani
Kilichobaki sasa ni viwanda vingi vilivyokuwepo zamani kufufuliwa baada ya kufa katika ka-mchezo fulani ka kuwaadhibu wenyeji baada ya kusapoti upinzani!!
Injinia ni MOSHI kuwa jiji au KILIMANJARO kuwa jiji???
Kwa jumla miji inayo stahili kuwa na sifa ya jiji Tanzania ni DAR, Mwanza na Arusha tu.
Ha ha!! Ni Moshi bwana. Mi sijui kuhusu Kilimanjaro nje ya Moshi. Kwa nini umeuliza hivyo? Nilidhani nilichoandika ni kuhusu mji wenyewe wa Moshi
Hapo natofautiana na wewe Magezi. Arusha!! Ile vurugu nayo ni jiji? Ni kwamba tu ina vitu vichache vinavyotakiwa katika jiji lakini the main thing kwa mfano lay-out ya mji (it was originally planned as a small hunting town), huduma ya maji safi na maji taka (you might argue kwamba mbona Dar ni jiji).
Usidanganyike na majengo machache marefu, wingi wa watu (tena wenye hela), uzuri wa magari, viwanja vya starehe nk. Jiulize, je UNICTR wakiondoka Arusha leo, mzunguko wa pesa utakuwa sustained?
Arusha kuwa jiji bila UNICTR inawezekana mkuu, UN-ICTR ni kigezo cha sehemu tu ya mzunguko wa mapesa A-city Mkuu
kwani kuna jiji tanzania basi kama ndo ivo ukilinganisha na majiji kama new york,tokyo n.k
acha madhereu weye, MBEYA haiwezi linganishwa na kahama. Mbeya ina uchumi mkubwa kuliko kahama==kama umekosa mji wa kulinganisha na Mbeya, sema. Unalinganisha na Kahama ambako kuna njaa toka asubuhi mpaka jioni... hili ni moja tu ninayo mengi sana tatizo muda wa kukukuambiahuwa wanatumia vigezo gani maana nimefika mbeya mji hauna hata chembe moja ya kuwa jiji unazidiwa hata na wilaya ya kahama jamani