Hivi nini hasa suluhu ya ukosefu wa ajira? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi nini hasa suluhu ya ukosefu wa ajira?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Scolari, Mar 8, 2011.

 1. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Ukiangalia post lukuki zinasanifu hali halisi ya ukosefu wa ajira inayozidi kumea Tanzania. Ni kweli hata nchi nyingine zinakumbwa na tatizo hili, lakini je hapa kwetu nini haswa tufanye kuwa mwarobaini?

  Mchango kwa mapana na wahusika wote; yaani kama serikali, je kijana mwenyewe naye afanyaje?

   
 2. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 280
  Hivi hd mtu uajiriwe ndo ujue unafanya kazi? Kujiari ndo suluhu.
   
 3. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Babaubaya:

  Ni kweli unaweza kusema hivyo yaani "kujiajiri" ndilo suluhu la kudumu. Ingawa hakika si rahisi kama kubyofa keyboard. Kwa upana wake tuangalie namna ya kukabili fursa za kuzalisha pato. Maana hata kujiajiri vijana wengi wanalalama kuwa na changamoto lukuki hivyo wanashindwa na kuishia kukaa majumbani wakiwa na shahada zao, hali ni mbaya sasa hata kwa wale wenye shahada za pili za biashara "MBA" hakuna kujiajiri wala biashara
   
 4. G

  Godwine JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mapinduzi
   
 5. K

  Koola Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo la ajira ni la ulimwengu Mzima.Wakati wa mdororo wa uchumi Kampuni ya ndege ya Uingereza ilipunguza wafanyakazi zaidi ya 500 na kufunga safari sisizo na faida.Hata Amerika imetokea na Obama anahangaika na kufufua uchumi na makapuni ya magari yalishapewa fedha za kuyasaidia yasife(stimulus package).Suluhisho ni sisi Watz kufungua makampuni kwa kutumia fulsa zilizopo hapa nchini nakuto ogopa kufeli kibiashara. Wageni wamekuja na kufungua makampuni kama ya usaili na wanaula ile mbaya.Tukubali kuiba ujuzi wa wenzetu tunapoajiriwa nao ili tuanzishe vya kweli.Unakuta Mtu yupo kwenye ajira miaka 30 ameridhika.Tufanye kazi kwa muda mfupi na kuwaachia vijana wanaochipukia ili tuwaajiri kwenye makampuni yetu.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ndiyo maana wakaja na kilimo kwanza!!!!???????
   
 7. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Koola:

  Ni kweli ni la ulimwengu mzima. Lakini mwenzetu wanajitahidi hakika kulishughulikia au kulijadili tofauti na hapa Tanzania
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hili ni suala sugu ulimwenguni kote, lakini kwa TZ ni kubwa zaidi kutokana na mfumo wetuwa elimu. Elimu inayotolewa, mfumo wa kusoma-kufundisha unalenga zaidi katika kupasi mitihani kuliko kuwa wabunifu. Pia tunatoka katika mfumo wa kutegemea zaidi ajira za sekta ya umma kuliko sekta binafsi.

  Suluhisho ni kujiajiri, lakini hili nalo lina ugumu wake, kukosa mtaji na ujuzi. La kufanya ni kwa vijana wenye ujuzi mbali mbali kujikusanya na kubuni miradi. Umoja ni nguvu.
   
 9. E

  Edo JF-Expert Member

  #9
  Mar 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Juzijuzi Mh Rais Kateua Katibu Mkuu mpya Wizara ya "ajira" . Alipohojiwa wakati wa kuapishwa nilimsikia anakiri changamoto hii ya ajira ilivyo kubwa japo naye amegundua tatizo ni mfumo wa elimu, Naamaini atakuja na mkakati endelevu wa suluhisho, tumpe ushirikiano katika hili ili tujipange upya katika vyuo vyetu, si kazi ya leo wala kesho, Lakini LAZIMA Tuanze!
   
 10. A

  ANNASTACIA Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kujiajiri ndio suluhisho ila inahitaji someone to overcome fear kwanza maana wengi wetu tunaogopa mwanzo zile challenges zinakuwa nyingi sana hadi watu tunaishia kwenda huku na huku kutafuta kuingia kwenye pay roll ya mtu wakati tungetuliza vichwa na kuanza vya kwetu na sisi tungeajiri wenzetu badala ya kuafiriwa tu! utasikia hata tulioko kwenye ajira tunalala mshahara hautoshi ila hatuchukui zile opportunity tunazoziona mbele yetu na kuzifanyia kazi za kutuongizia kipato cha zaidi badala tu ya kutegemea mshahara tu kila mwisho wa mwezi
   
Loading...