Hivi ni sahihi mitandao ya simu kuingiza tena sokoni namba ya simu ambayo haijatumika kwa muda fulani?

man dunga

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
3,216
5,566
Unanunua line na kusajili lakini kutokana na sababu mbalimbali, unakuta hujaitumia hiyo line kwa muda fulani. Cha kushangaza mitandao ya simu inaaamua kuiingiza tena sokoni hiyo namba ili inunuliwe na kusajiliwa na mtu mwingine.

Kitu kimeuzwa na kusajiliwa sasa kwa nini kisimilikiwe daima na aliyekinunua? Mbaya zaidi ukomo wa hiyo line kuwa hewani kabla hawajaingiza tena sokoni unakuta ni miezi mitatu yaani hawajafikiria hata suala la mtu kuumwa n.k.

Huu usajili mpya ufutilie mbali kabisa uwezekano wa line moja kuja kusajiliwa zaidi ya mara moja.
 
Watajuaje Kama we we unaumwa na je Kama umekufa? Kinachofanyika hapo ni maelekezo kutoka tcra wanataka kujua ni laini ngapi zinatumika
Line ikiingizwa tena sokoni inaweza kukaa hata mwaka au miaka bado haijanunuliwa na mtu mwingine, sasa sababu hasa ya tcra(kama ulivyosema) kuhimiza line zisizotumika kwa muda fulani kuingizwa tena sokoni ni nini?
 
Policy za kampuni nyingi ni miezi 6 ( siku 180).

Msidanganye watu.
Unanunua line na kusajili lakini kutokana na sababu mbalimbali unakuta hujaitumia hiyo line kwa muda fulani. Cha kushangaza mitandao ya simu inaaamua kuiingiza tena sokoni hiyo namba ili inunuliwe na kusajiliwa na mtu mwingine.

Kitu kimeuzwa na kusajiliwa sasa kwa nini kisimilikiwe daima na aliyekinunua? Mbaya zaidi ukomo wa hiyo line kuwa hewani kabla hawajaingiza tena sokoni unakuta ni miezi mitatu yaani hawajafikiria hata suala la mtu kuumwa n.k.

Huu usajili mpya ufutilie mbali kabisa uwezekano wa line moja kuja kusajiliwa zaidi ya mara moja.
 
Airtel wamenipigia ikifika 31 Dec 2019 sijasajili alama za vidole line itafungwa.
Sijui wanataka kunifanyia mnachosema?
Mimi niko kitandani nimepooza miguu japo naongea na kuandika watakuwa hawajanitendea haki waje hapa kitandani wachukue alama zao.Mimi ni mteja wao toka wanaitwa Celtel-Zain-Airtel au lugha nyepesi toka waje nchi hii nimewachangia mno.
 
Pole sana mkuu
 
Acha kupotosha, line ikifungwa kwa sababu yoyote ikiwemo kutotumika kwa muda mrefu, ujue hiyo namba HAIRUDI HEWANI tena.
 
Back
Top Bottom