Hivi ni nini kinaendelea Clouds Tv?

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,095
22,705
Habari ndugu watanzania wenzangu na wazalendo wote mnaopenda maendeleo ya taifa letu teule.

Dhumuni la uzi huu ni kuhoji mwenendo unaoonekana katika kituo cha televisheni cha Clouds TV hasa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadan.
Kiukweli nashangazwa kama sio kupigwa butwaa na mwenendo wa vipindi ambavyo kwa masaa yote vimekuwa vishabihi maudhui ya kipindi hiki cha wanaimani wenzetu. Yaani tokea asubuhi hadi jioni imekuwa ni matangazo......kampeni na vipindi ambavyo ni vinavyohusu imani ya kiustadhi tu kiasi kwamba najiuliza hivi hii stesheni ni ya kihafidhina au ni nini.
Hivi ruge na kujifanya mjuaji kote ameshindwa kujua kuwa clouds inapatikana katika vingamuzi ambavyo vinaifanya kutazamwa na mamilioni ya watanzania bara ambao si wote wanashea imani ya kiislam........
Sikatai kama kituo cha televisheni wanaweza watakia mfungo mwema watazamaji wao ambao wanafunga wakati huu lakini isiwe too much kama wanavyofanya kile si kituo cha dini fulani hadi wakae wakituonyesha mawaidha......mara hadi maigizo yote yanaakisi dini ya kiislam.......watangazaji wote ni asalam aleikum muda wote kwani mliambiwa wapi kuwa inapofika ramadhani tanzania nzima tunafunga?! Mbona hizo mbwe mbwe hatukuziona kipindi cha kwaresma kama nyie ni kweli kituo ambacho mnaheshimu imani za wengine.....?!
Hebu acheni unafiki uongozi wa clouds mnachofanya si jambo la kistaarabu ni unafiki wa kujifanya ni media mnayojali imani kumbe mna masilahi yenu ya kimasoko ya kuwashika akili watu kwa kutumia dini.
Dini ya kiislam wanazo stesheni zao za redio na televisheni ambazo mwezi huu watapata hayo mawaidha na hata ibada wakitaka.
Sasa ninashangaa sana mnapojiita televisheni ya watu au redio ya watu halafu mnafanya unafiki huo wa kujifanya mnajua sana kushabikia imani ya dini fulani na kuitumia kama karata ya kuwashika ili watazame stesheni yenu.......je mnadhani na wasio katika imani hiyo wanafurahia kuaangalia hicho mlicho kazana nacho?!
Hii stesheni m'meanza kufulia vipindi hadi mnaanza kutumia udini kama gia ya kuvutia watazamaji kitu ambacho si kizuri kwa taifa. Mbona wenzenu I.T.V......chanel ten......star tv.......na nyenginezo hawana hayo mashauzi........?!
Huo ni unafiki na muuache mara moja .......kama mnaona vipi basi nendeni mkabadili usajiri wa matangazo ili msajiriwe kama kituo cha matangazo ya dini ya kiislam ila sio kutuonyesha vipindi vyenye maudhui ya dini moja na mkijua wazi hili taifa lina mchanganyiko wa imani........na zipo stesheni maalumu kwa kila imani husika .....wale ambao wanataka hizo vitu waende kutazama huko na sio nyie kuwa wanafiki kwa kuwachota watu akili mkitumia dini yao ili muonekane nyie ni baab kubwa wanafiki wakubwa nyie.
Na kuanzia leo nimeacha rasmi kuwafuatilia vipindi vyenu maana nimeona dhahiri kuwa ninyi si kituo cha watu kama mnavyojiita ila ni watu wavinafsi na haya mnayoyafanya wanatufanya wenye imani tofauti kujihisi kutothaminiwa kabisa na wapanga vipindi wenu.
Bakini na mavipindi yenu ya kinafiki na mjue kuwa kila siku zinapokwenda mnapoteza watazamaji na wasikilizaji m'moja baada ya mwingine. Bora nisikilize radio Tanzania kulikoni Clouds......wamekuwa na mambo ya ajabu sana.
Kusaka you should fire ruge he is not a creative person anymore.......
 
Ufinyu wa mawazo unaweza kukusababishia kifo sasa yy analalamikia clouzds bila kujua vipi vyote vile ninalipiwa kama hata angali chanel nyingine usiwe mvivu wa kufikiri utadhindwa kuishi maisha salam
 
Ohh butthurt people hawakosekani,alafu kwanini kila siku clouds kwani hamna chaneli nyingine?huu ndo mfungo wa ramadhan upo powerfull sana bro wala usijisumbue maana unajipiga promo wenyewe mpaka magazeti hua yanatenga kinafasi yanaatuhisabia siku ya ngapi leo katika mfungo..
 
Nchi hii ina mbulula na mbumbu wengi sana. Sasa ndio umeandika nini??
wewe ndiye mbulula na mbumbumbu kabisa usiyejua nini hakipo sawa.......na unaonekana ni product ya BRN maana hata hauwezi kujua madhara ya kinachoendelea........pengine ruge ni shemeji yako ndio maana unatetea.
Ila kaa ukijua wanachofanya kinaweza kuwa kina kupendeza wewe machoni pako kwasababu unashea imani ila kama ungetizama kwa jicho la tatu ungeona kuwa si jambo la busara kwa stesheni ambayo inatazamwa na halaiki hata kama ni ya binafsi kuwa inafanya ushabiki au kukazia matukio ya kidini kitu ambacho si kizuri........ila nahisi bado haujakomaa kiakili kuyaona hayo ni waliopevuka tu ndio wanaweza kuona.
 
Mtoa mada naona mmmmh iko shida kwake
We kama unaona hupendezwi si unabadilisha channel tu
hiyo sio suluhu .......cha muhimu ni ujumbe uwafikie wahusika ili wajue wanachofanya si sahihi
 
Ufinyu wa mawazo unaweza kukusababishia kifo sasa yy analalamikia clouzds bila kujua vipi vyote vile ninalipiwa kama hata angali chanel nyingine usiwe mvivu wa kufikiri utadhindwa kuishi maisha salam
Wewe ndiye uliye na ufinyu wa mawazo unayeongea bila kuelewa unasema nini.........kwahiyo akitokea mtu na pesa zake akalipia clouds ionyeshe picha za utupu mchana watakuwa sahihi kukubali kisa wamelipwa..... .?!
Tumia akili wewe sometimes media inatakiwa kuwa makini katika kuchagua vipindi........maswala ya kidini au imani huwa inatakiwa waishie kwenye kutoa salaam tu tena kipindi cha sikukuu ndio utamaduni wetu kama haujui........sasa kutuweka masaa 24 vipindi vya mambo ambayo imani moja ndio inahusika si jambo la busara sana.
Na kama haujajua tu ile hawafanyi kwasababu ni wanamapenzi na imani husika ni njia yao ya kiboya ya kujifanya wanajua imani zingine wakati mwaka mzima huwa hii channel inaonyesha vituko vya hii dunia. Sasa kama wewe ni mpenda imani yako sana ubadilishe chanel utazame channel ambazo zina maudhui ya imani yako sio kujifanya unaelewa sana mambo ya media wakati ni zero brain plus BRN product ........zumbukuku punguwani wahed kabisa.
 
Ohh butthurt people hawakosekani,alafu kwanini kila siku clouds kwani hamna chaneli nyingine?huu ndo mfungo wa ramadhan upo powerfull sana bro wala usijisumbue maana unajipiga promo wenyewe mpaka magazeti hua yanatenga kinafasi yanaatuhisabia siku ya ngapi leo katika mfungo..
True that my friend. Ila nilikuwa nawapa tu alert kuwa wamepitiliza na program zao maana too much ya chochote huwa inaboa sana......... yaani si tu maswala ya kiimani hata ingekuwa ni jambo lolote lingine unapokazania kuonyesha kitu fulani cha msimu wa kipindi fulani kwa kulenga watu fulani tu hiyo si mzuri maana kuna wengine unachokionyesha hakiwapi msisimko wowote zaidi ya kuwakera so why not tusiwaambie.

Mfano mambo ya siasa ukitaka sana unakwenda TBC .........kama kumsifu bwana unajua kuna tv tumaini na redio tumaini.....efata.....atn etc.........kama ni kupata dua na mawaidha kuna imani radio na tv......kuna africa tv etc........sasa stesheni kama clouds wanatakiwa wafocus zaidi kwenye program za kawaida maana wakumbuke kuwa si kila mtu ni wa imani moja wengine wanaimani tofauti kuwawekea vitu vya imani isiyowahusu masaa yote na vipindi vyote inakuwa haiko poa labda tu kama wana malengo yao amambayo mimi nadhani si mazuri kama wanatumia imani ya watu fulani kuyafikia.
 
Kama redio mimi nimasikiliza Wapo Radio. Tv sina!
Umeongea vizuri jirani........yaani kama ni swala la imani yako .....unatafuta kituo cha tv ama redio kinachorusha matangazo yanayohusiana na hiyo kitu yako........sasa nashangaa kuna baadhi yetu hapa ambao hawajaelewa ni kitu gani kibaya kinafanyika kwa kurusha matangazo yenye uhusiano na imani fulani tu masaa yote.
Ni bora wangeamua basi kubadili maudhui ya hiyo channel iwe ya imani hiyo kabisa kulikoni kuwa wanafiki hivi.
 
Shemegi yetu ni mzenji... Kwani hujui nguvu ya wabeijingi?
Hata me nimeshaanza kuona kuwa kuna akili ndogo inapelekesha akili kubwa .......na akiendelea kupelekeshwa vile ajue ipo siku atakuja kufanya vitu vya ajabu sana na ndio maana chanel inapwaya siku hizi.......watangazaji wazuri wanakimbia........maamuzi ya ajabu ajabu yanapitishwa........what a waste kwakweli.
 
Back
Top Bottom