Hivi ni mimi tu ndo nashangaa au kuna mwingine huko ?!

Hivi ni mimi tu ndo nashangaa au kuna mwingine huko ?!

Andie

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
712
Reaction score
1,643
Ukizungumza na wanawake wenye kujitahidi katika masomo ngazi tofauti tofauti za elimu lengo lao HASA sio kusaidia familia zao hapana, wala kuendeleza ndoa zao badae hapana lengo kuu ni "sitaki kunyanyaswa na mwanaume" yani hili ndo limewakaa vema kwenye ubongo wao na kwa kweli linawapa msukumo wa kutosha kujitahidi sana sana kwao kwa nia thabiti ya "kujikomboa" toka kwetu "makatili"(wanaume)

Sasa ninaposhangazwa ni hapa, hivi karibuni aise kweli wanawake wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa "kujikomboa" wasomi wanawake wameongezeka sana madaktari, walimu, wanasheria nk sasa nilitegemea wafurahie si ndio jamani...?

ila hapana wanalalamika, wanahangaika sio kwa waganga tu mpaka makanisani watumishi wa Mungu wengine wameanzisha "programu maalumu" ya kuwaombea maombi maalumu kwa mfano Rwakatale na upepo wake wa kuleta waume "kimiujiza" pastor Mwamposa na Mitimingi na "upako" wa kuolewa. Manabii nao hawajabaki nyuma nao wamepata ulaji wanawake wasomi na mahela yao wanatozwa hela ndefu ya kupanda mbegu iote kua mume.

Jamani hawa si ndo wanasoma kwa usongo na gadhabu kuu ili "kujikomboa" toka kwa wanaume, sasa wameshajikomboa si waishi kivyao sasa na maelimu yao, na mataaluma yao na mahela yao wanahangaika nini kujirudisha tena kutaka companionship na wanaume ??!!

Wanaume si makatili sasa kwanini wanataka waolewe nao ??!

Unajua nimekuja kugundua wanawake ni viumbe wa ajabu na hauwezi kuwaelewa, anaeweza kumuelewa mwanamke ni mwanamke mwenzake na wanachukiana balaa waana wanajuana hasa.

Hujawahi kusikia mwanamke akisema "mimi sina urafiki na wanawake marafiki zangu wengi ni wanaume" afu huyo huyo utamsikia "wanawake tusome tujikomboe na hawa wanaume" unabaki unajiuliza huyu kashiba maharage gani na hupati jibu.

Nimalize kwa kusema, feminism didnt come to save women, it came to tarnish and victimize them. Mwanamke yeyote mwenye busara hawezi kushadadia haki sawa. Na hili wimbi la women enpowerment ni mpango unaofanikiwa SANA kuibomoa jamii.

Peace be with you all.
 
Imeandikwa "kichwa cha mwanamke ni mwanaume"
Na hata wao ndani ya mioyo yao wanalitambua hilo ila wanakua na ujinga wa kutosha kuamini mifumo ya usawa.
 
Mwanzo wakati wa ku- struggle huwa hawajui kama wanapotea ila baada ya kupata walichopata ndipo hugundua umuhimu wa wanaume kwenye maisha yao.

Kuna wawili ambao nawafahamu vizuri, wamefanikiwa kimaisha vizuri saana kabisa ila wanalilia kupata waume.
 
Kuna mwenye njaa humu??

Ndoa sio wanawake tu ndo wanazitaman hata wanaume
So, nimaujanja yako tu yakutafuta yatakusaidia.
Nawasubiri waje wameshiba maharage yao.
 
SK2016,
Na mbaya wanaume huwaogopa wanawake wa aina hiyo. Kwa sababu wengi huwa si wanyenyekevu. Elimu na taaluma zao huwa wanataka kuziapply mpaka ndoani.
 
It's difficult to resist nature and survive at the same time, loose one gain one.
M nahic kuna vitu vingine ni kama natural laws ambazo tumezaliwa nazo na tumekulia nazo ili maishe yasonge mbele bila vikwazo vilivyozidi. Watu tumekua tumekuta mama zetu wakiwaheshimu baba zetu. ila dada zetu wanataka wao waheshimike zaidi ya sisi kaka zao. Ndo matatizo yanapo anza. Eti unasoma ili mwanaume asije kuku nyanyasa hii mentality imefanya wadada wengi katika ndoa kuona mateso kutimiza majukumu yao, wanaona kama wana nyanyasika, ila hayohayo mama zetu walifanya kama majukumu yao. Any way ukitaka kitu kimoja kwa nguvu lazima upoteze kingine. Mkitaka kukimbia manyanyaso kwa mwanaume kubali kuishi single. Na huu ndio ukweli mchungu, kwa sababu wanaume hatupendi kuendeshwa au kuamliwa mambo na wanawake.
 
Ukijibu hii thread make sure umeolewa,sio unakuja kujimwambafai Hapa halafu kumbe kila jpili upo kwa mwamposa na rwakatare kupewa upepo wa kisulisuli
We mbugila nilishakukataza kuniquote
 
Na mbaya wanaume huwaogopa wanawake wa aina hiyo. Kwa sababu wengi huwa si wanyenyekevu. Elimu na taaluma zao huwa wanataka kuziapply mpaka ndoani.
Hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia manyanyaso yao na ukiwaona hadi unajiuliza mara mbili mbili! Kwa uzuri wao na kazi zao nzuri lakini wanavyolilia kuolewa!
 
Back
Top Bottom