Hivi ni lini Serikali itaanza kugawa vitambulisho vipya vya wajasiriamali wadogo?

wankuru nyankuru

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
491
763
Habari wadau?

Mimi ni mjasiriamali mdogo katika kipindi hiki cha janga la covid 19 nimeamua kuanzisha biashara yangu ili iweze kuniingizia kipato.

Na ili niweze kufanya biashara yangu bila ya matatizo, wadau wamenishauri nikachukue kitambulisho cha ujasiriamali ( vitambulisho vya magufuli).

Kabla hata ya kuanzisha biashara na kufanya uamuzi wa kuchukua kitambulisho nilikuwa najiuliza sana kuhusiana na janga hili la corona na biashara yangu. Kwa kuwa naweza chukua kitambulisho hicho badae ikala kwangu.

Hivyo Basi, naomba kujua ni lini vitambulisho hivyo vitatolewa tena kwa mwaka 2020/2021?.

Lakini pia kwa janga hili la corona nahofia inaweza ikala kwangu endapo nikachukua kitambulisho alafu biashara isilipe, wajasiriamali wenzangu hili limeakaaje?.

Vile vile, kwa wale wajasiriamali wenzangu waliowahi kuwa na vitambulisho hivi ni changamoto gani mlizowahi kutana nazo katika biashara zenu ? Tusaidiane kwenye hili ndugu zangu wapendwa.
 
Suala la vitambulisho vya wajasiriamali wadogo nahisi serikali haikujipanga vema. Walikurupuka bila kuwa na utaratibu mzuri wa kuvitoa kwa wahusika.
Mimi Nina Cha Mwaka 2018/19 ndicho nakitumia had Sasa
In short wahusika wamefeli


Wamefeli kabisa namimi nnacho cha last yr may! Labda watatoa vzuri zaidi!
 
Wameona haiwalipi, mtaani wafanyabiashara wameshaanza kuchangishwa makodi kama kawaida
 
Nafikiri hawakujipanga vizuri hasa kwenye utekelezaji lakini pia kulikuwa na mwingiliano kati ya TRA, Tozo za Halmashauri husika na Vitongoji vyetu, naamini wangeweka sawa mambo hayo mambo yangekuwa safi pasipo na mawaa
 
Back
Top Bottom