SoC02 Kukosekana kwa Ajira kwa Vijana Wengi Kumeibua Ajira Mpya kwa Waajiriwa

Stories of Change - 2022 Competition

Taric Hiyari

Member
Jul 26, 2021
5
3
1E1B6123-7661-4637-BC6C-7E464B4D9CD5.jpeg
960F1FC1-BD27-4A53-A06E-861E850EAEB7.jpeg

Kuna Wimbi kubwa sana la Vijana mtaani wanaomaliza masomo yao katika Ngazi mbalimbali za Elimu lakini vijana hao wapo mtaani wakihaha na Kuwaza ni lini watapata Ajira Rasmi, Ilhali wapo Vijana ambao walichukua Uamuzi wa Kujiongeza na kuthubutu kujiajiri kutokana na kile walichokipata wakati wakiwa Vyuoni kwa wale waliobahatika kupata Mikopo au waliowezeshwa na Watu wao wa Karibu kutokana na Changamoto walizoziona na kuzibadili kuwa Fursa, Lakini Je ? Watu wote wanaouwezo wa Kujiajiri ?,

Je ni wote wanauwezo wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na Biashara za Kujiajiri ?, Je ni Wote wenye Uwezo wa kupata Mitaji ya kuendeshea Biashara ? Jibu ambalo litaweza kujibu Maswali yote haya japo kwa ufupi ni kuwa "si kila mtu ni Mfanyabiashara ama Mjasiriamali”, ndio maana hata ambao wanaoamua kuchukua uamuzi wa Kuanza Biashara, basi nyingi miongoni mwao kama si kuishia kati basi hufa kabisa katika kipindi kifupi, na ndio katika Hatua hii kunakua na Umuhimu wa Wahitimu wengi Kutafuta Ajira rasmi kama kimbilio la kutatua changamoto za Maisha yao Kutokana na kile Walichosomea na Kutarajia kukifanyia kazi,

Lakini kwa Upande wa Pili Imekua tofauti zaidi na Vile walivyotegemea

Dar es Salaam : Binafsi ni Mhitimu katika Elimu yangu ya juu ambapo nilitarajia kuwa ningepata Ajira mapema mno kama nilivyotegemea ambayo ingeweza Walau kunipatia afueni ya Kuendesha Maisha yangu binafsi na Kuwasaidia wale wanaonizunguka kama Baba, Mama, na Hata wadogo zangu pia, kwakua Mimi ndie Mtoto wao wa kwanza na ndio tegemezi ambae nimeweza kufungua Njia na Kua kama Mfano wa kuigwa kwa wanaonifuata,

Lakini imekua tofauti na vile nilivyotegemea na ni zaidi ya miaka minne sasa tangu nimalize masomo yangu na kuhitimu ( Peter : Sio jina halisi ) Bado anahaha kutafuta Ajira na ikipatikana basi Stori huwa ni Tofauti.

Safari yake ya kutafuta Ajira imekua siyo Rahisi kama ilivyo kwa Vijana wengine wanaotuma maombi kila kukicha bila ya Mafanikio na Kufikia Hatua ya Kukata Tamaa na kuamua kukaa tu Nyumbani kufanya mambo mengine,

Hii inatokana na Waajiri wengu kuleta Maslahi yao Binafsi mbele kuliko mahitaji ya Waajiriwa na kugeuza kua njia ya kujipatia Vile wanavyohitaji,

Kuna Mifano Mingi, Baadhi nitaiambatanisha kwenye picha ili kulidhihirisha hili na kuonyesha jambo hili jinsi linavyozidi kuchipua mizizi upyaa katika Taasisi mbalimbali, Kiasi cha kwamba Huwezi kupata nafasi mpaka Utoe Chochote kitu (Pesa, Ngono na vitu mfano wa Hivyo), au Uwe na Mtu wa karibu katika Taasisi unayohitaji Kuomba kazi (Vijana wa Mjini wanaita Konekshen), Bila ya Hivyo Inabidi ukae pembeni Usubiri Miujiza ya Mungu Ichukue nafasi, Kama si Nyota na Bahati basi wewe utakua ni Mtu wa kutuma Maomba na Kusubiri Majibu yasiyojibika, Na Umekua ni Mwiba unaoumiza kwa Vijana Wengi Ukizingatia kuna Wimbi kubwa la Vijana Mtaani linalohaha Usiku na Mchana kutafuta Ajira,

"Utakuta Kijana wa sasa wa Kitanzania Simu imejaa magroup ya fursa za Ajira kuliko umbea na Udaku yote hii ni kuhakikisha anakua karibu kupata Taarifa za kazi za Makampuni, Serikali na Mashirika mbalimbali ili aweze kujiendeshea Maisha yake licha ya kinachotafutwa kutopatikana kwa Urahisi”,

Licha ya kuwa na Vifungu vya Sheria vikali vinavyokemea vitendo hivi kama vilivyoanishwa katika Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na 11 ya Mwaka 2007 sehemu ya III inayosema katika vifungu vya 15-39 kuwa :-

KF 15 : Kuomba, Kushawishi au kulazimisha kupewa Rushwa, Kutoa au kuahidi kutoa Rushwa Faini 500000-1000000 au Kifungo cha Miaka 3-5 au vyote kwa Pamoja

KF 16 : Kutoa au Kupokea Rushwa ili kupata Mkataba wa kutoa Huduma kwa Idara ya Umma au Shirika la Umma Faini Shilingi 3000000 au kifungo cha Miaka 7 au Vyote kwa pamoja.

KF 20 : Rushwa katika Ajira Faini Milioni 5 au kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja

KF 25 : Rushwa ya Ngono, Faini milioni 5 au kifungo cha Miaka 3 au vyote kwa pamoja.
na Vingine vingi miongoni mwavyo vinavyoonesha adhabu zitakazowakuta wale wote watakaojihusisha na Vitendo hivi lakini zimeshindwa kufua dafu na hata zinapofanya kazi basi kwa kiasi kikubwa athari ya vitendo hivyo vinakuwa vimeshashika hatamu

Mara nyingi katika jamii zetu watu waliokatika tabaka Duni ndio wamekua wahanga wakubwa katika jambo hili, Utakuta mzazi Kamgharamikia Mtoto wake Kumsomesha kwa Kuuza Ng’ombe, Kulima na Kuuza mazao mtoto aende Shule, Akafaulu kwa Shida mpaka akafika Chuo kwa Bahati miongoni mwa wengi Hufanikiwa kupata Mkopo na Kupunguza makali ya kutafuta Elimu, Wenzangu namimu niliekosa Inabidi tena Michango Ichangishwe upyaa nyumbani, Baba , Shangazi, Mjomba ,Bibi na babu ili kuweza kupata Ada ya Chuo na mahitaji ya Hapa na pale,

Wazazi wanashukuru kwa Mtoto wao kumaliza Chuo kwa Ugumu na Shida nyingi na Sasa kaingia katika Soko la Ajira Lakini Ajira imekua ngumu kupatikana kiasi cha kushinda Magumu yale yote nyuma aliyoyapitia na Ubaya zaidi hizo ajira zikipatikana basi pasina Chochote kitu (Rushwa ya Pesa, Rushwa ya Ngono na vingine mfano wa Hivyo) basi hamna kitu (Ajira), Kwa namna Hii Mzazi huyu Sidhani bado atakua na nguvu na Uwezo wa kendelea kuwa na nguvu ya kuweza kutoa kima kile kilichohitajika ili mtoto apate nafasi kutokana na Uduni wa Maisha,

Ambapo hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa mno kwa kutengeneza Mazingira hatarishi kwa Vijana, pale ambapo kile ambacho kinachohitajika kinashindwa kupatikana huku nafasi akiwa anihitaji basi vitu vingi vinaweza kuibuka,

Kwa watakao weza kukabiliana na hali wataamua kuchukua Uamuzi wa kupambania vitu vingine mtaani lakini matatizo mengi yataweza kuibuka pindi pale watakpoamua kuachana na Mfumo rasmi, matatizo hayo ni kama yafuatayo ;

• Kupoteza Malengo ya Vile walivyosomea au kutarajia kuja kuvifanyia kazi,
Kuna kauli niliwahi kuambiwa na Rafiki yangu ambe alinitangulia Darasa Moja yaani kimsingi alimaliza Chuo baada yangu Mara baada ya kumtembelea Ofisi yake (Duka la Simu) lililopo Kariakoo jijini Dar es salaam na Kuniambia "….Unawaona wanaouza simu wote hawa kwenye haya Maduka Wengi ni "Degree Holders” yaani watu na Degree zao Vichwani, tena sio za Hovyo ni za maana tu, Sema ndo hivyo Soko limekua gumu na Maisha hayasimami sasa utafanyaje unafikiri, Inabidi ujichangaje upate kwenda Chooni….”

Maneno yake kamwe sitoweza kuyasahau yamekua yakiishi katika Kichwa changu kwa Miaka sasa, n sio hao tu ni wangapi watu na "GPA” zao za maana lakini tunakula nao Moshi Barabarani na kuharibu mapafu yetu kwa kuamua kua Madereva Bodaboda na Ukizingatia hata huyo aliyekua ofisini kwa huyo kijana bado anasubiri…"nikimaanisha Uwezo wake ni Mkubwa mno ila ndo vile kwasababu ya Changamoto kama za namna hii

•Tumezoea Kuwa "Panya Road”(Vikundi vidogo vidogo vya kihalifu) na Vikundi mfano wa Hivyo kuwa vinatokana na Vijana labda walioishia Shule za Msingi ama Kidato cha pili au cha nne au wasiosoma kabisa (Vijana wa mitaani) ila kwa Miaka kumi au kumi na tano ijayo tutarajie hali hiyo kuwa tofauti,

Kutokana na Idadi kubwa ya Wasomi kuongezeka inasababisha kuwa na Ufinyu wa Ajira za kuweza kutosheleza watu wengi kuingia katika Ajira hizi na Kusababisha wachache kupata na wengi kati yao kukosa na Ikumbukwe adha hii ya Ajira sio tu kwa vijana wadogo bali kwa watu wenye Umri zaidi ya Vijana ambao wengi wao waliacha kazi zao za awali au kuzipoteza kutokana na Sababu mbalimbali, sasa swali linakuja kundi kubwa kama hili likafika kikomo cha ukomo wa kuchukua maamuzi ya kuamua kutafuta njia fupi fupi za kutafuta kipato kutokana na Ugumu wa Miasha hali itakuaje katika Jamii zetu ?Jibu Unalo (Huu ni mtazamo tu)

•Elimu kushuka na kupoteza thamani yake
Imekua ni jambo la kawaida mno kwa jamii zetu za kileo kumsikia mtu akisema "….Mtu mwenye degree hana tofauti na yule aliyeishia kidato cha nne au darasa la Saba…” Ilhali ya ule

Msemo wa kiswahili usemao "Mjinga aliyesoma si sawa na Mjinga asiyesoma” au tofauti ya wewe Uliyesoma likitokea Jambo lenye kukuhitaji na una fani na ujuzi nalo ila vyeti ulivifungia kabatini basi inakuwa rahisi kuanza tofauti na yule aliyekua kijiweni pasina chochote kupata nafasi hiyo, ila Jamii imefasiri hivyo kutokana na ule uhalisia kua katika Jamii zetu kwasasa ni Ngumu kumtofautisha yupi aliyesoma na Asiyesoma kutokana na Mabadiliko ya Maisha inapelekea ata yule Mwenye Uwezo fulani wa Elimu kushirikia kazi ambazo kwa Hadhi yake ya Elimu si sawa Yeye kufanya hivyo ila inambidi afanye hivyo ili Maisha yaende Mfano : Madereva bodaboda, Makondakta, Wabeba zege na Kazi nyingi mfano wa hizo, Ambapo kwa kawaida tumezoea wao ni watu wa maofisini tu kutokana na Elimu zao, ingawa sio jambo baya ila tafsiri inayopatikana hapa ni kuwa, Elimu haina hadhi tena kama vile ilivyo zamani

Kwa Upande wa pili na ambao ni wa muhimu zaidi ni Juu ya nini kifanyike ili kuweza kutokomeza hii hali ya "Waajiri wengi kuibua Ajira mpya kwa waajiriwa, kwa kutengeneza Mazingira ya kupata vile wanavyohitaji ili kukidhi haja na mahitaji yao binafsi nje ya lengo kuu la kuwaajiri pasina kuingiza kona kona katikati, mambo hayo ni kama yafuatayo:

i. Kwanza kama kijana ni Muhimu kujijengea Uwezo Binafsi wakutumia Ujuzi Ulionao pamoja na Vipaji Ulivyonavyo kuvigeuza kuwa kazi ama ajira yako binafsi ya kujiingizia Kipato kabla ya Kufikiria kuajiriwa,
Changamoto yetu kubwa sisi Vijana ama wasomi wengi tumeshaweka Akilini neno "Kuajiriwa” na Kusahau kua kumbe kuna Maisha mengine yanawezekana nje na kuajiriwa na ukaweza kuendesha Maisha yako Zaidi ya vile unavyodhani inaweza kuwa, kwamba bila ya kuajiriwa kuwa Haiwezekani, na hili linaweza lisiwe kosa la wasomi wengi Nchini bali ni Mfumo Ambao "Unakua ukikua ukikujenga” kuwa Mwajiriwa badala ya kukujengea uwezo wa kujiajiri na Mfumo ukiendelea kua hivyo na wala hutoweza kubadilika na kama ukibadilika, kwako itakua tena si fursa ya mabadiliko bali kwa vizazi vinavyokuja.

Lakini hilo kwako sio tatizo ndio Maana kukawepo na Majukwaa kama haya ili upate kuelimika na kuona kuwa bado haujachelewa na kwa wale waliowahi kuliona hilo haswa Vyuoni utakuta Mwanafunzi anapata uwezo wa kujiongeza kwa kuanzisha kabishara kwa kujiajiri kutokana na Ujuzi alionao na kuendesha Biashara yake katika Muda wake wa ziada na Maisha yakaendelea, Ama kwa wale walioamua kubadili vipaji vyao kuwa Fursa na Maisha yao yakaendelea, Hivyo tunaona kua hili jambo linawezekana kama tukianza kuwajengea hari vijana na miundombinu wezeshi ili waweze kuepukana na wimbi hili lililojaa changamoto lukuki badala ya kua tegemezi kusubiri ajira basi waweze kujiajiri na kuepukana na vishawishi na changamoto zisizokua na ulazima.

ii. Maboresho katika Mifumo ya Usaili na Usajili (Mifumo ya Utoaji na Upokeaji kazi pamoja na Maombi),
Mnamo mwaka 2019 Ulizinduliwa mfumo wa kidigitali wa Maombi ya Kazi (Ajira Portal) Uliopo chini ya Ofisi ya Raisi sekretarieti ya Ajira ili kuondoa changamoto mbalimbali ikiwemo Vitendo vya Rushwa na Gharama za Kutangaza Ajira katika Vyombo vya Habari, Ambapo mfumo huo Unajumuisha Maeneo Makuu matatu lakwanza likiwa;

Eneo la Mwombaji wa kazi (Applicant), Eneo la Mwajiri (Employer), na eneo la Sekretarieti ya Ajira (Handling interview process and placement/adjustment) Licha ya kuwa ni moja ya Ngao kubwa sana katika vitendo vya Rushwa, Utashi na Upendeleo katika Sekta ya Ajira Nchini, Lakini Bado tatizo na Vitendo hivi vinazidi kushika hatam kila Uchao, Hivyo serikali pamoja na Wadau wa Maendeleo na watu mbalimbali katika Tasnia za Tehama, kuna umuhimu wa kujikita na kuja na Mifumo tumishi mingine bora zaidi itakayoweza kutokomeza tatizo hili la Rushwa katika anga zote za Maisha na Sekta za Ajira kwa Ujumla.

iii. Jukumu la Kuzuia na Kupambana na Janga hili la Rushwa ni letu sote kama Taifa
"…Nilianza Mapinduzi nikiwa na watu 82 kama nikipewa nafasi nyingine ya kufanya hivyo, Nitafanya na Watu 10 au 15 wenye Imani madhubuti, Haijalishi Udogo ulionao kama una nia na mipango madhubuti…” Maneno haya aliyasema Raisi wa zamani wa Cuba Bwana Fidel Alejandro Castro Ruz, Yaweza yasiendane na kile nilichokiandika hapo juu ila ninachotaka kumaanisha hapa ni kua,

Ni bora kuwa na Jamii yenye watu wachache itakayosimamia Usawa, Uadilifu na Haki kwa wote kuliko tukawa na Taifa lenye watu wengi lakini Sheria ikawa haifuatwi wala kufuata mkondo wake na kuendeshwa na watu wenye ulafi na tamaa yakutaka vile wanavyohitaji kwa kua Madhara ya Vitendo hivi ni Mengi mno kuliko faida yake na husababisha watu kutopata Stahiki zao, Kupewa kazi watu wasio kua na ujuzi wala vigeo stahili, Mmonyoko wa Maadili na vingine vingi ambavyo hata nikivitaja vipi sitoweza kuvimaliza,

Hivyo ni Muhimu kuwepo na Mazingira wezeshi yatakayoweza kuwasaidia Vijana
Kua na ari ya Kusoma wakitarajia kuja kuvifanyia kazi vile watakavyosomea, Pili Kufanyia kazi zile Sheria na taratibu zote zilizowekwa ili kuzuia vitendo vya Aina yoyote ile vya Rushwa kwasababu huu ni mwiba unaoua na kumaliza ndoto nyingi za Vijana.
 

Attachments

  • 9B406A53-CFB0-46A3-92DD-36043AD9C769.jpeg
    9B406A53-CFB0-46A3-92DD-36043AD9C769.jpeg
    73.8 KB · Views: 30
  • 33F79C05-40DA-48BD-A37C-0F220C90FB0A.jpeg
    33F79C05-40DA-48BD-A37C-0F220C90FB0A.jpeg
    41.3 KB · Views: 25
  • 8F1D3B72-1020-404F-B904-0BBF27623D9E.jpeg
    8F1D3B72-1020-404F-B904-0BBF27623D9E.jpeg
    29.6 KB · Views: 23
  • 15FA0203-44D8-4814-A4CB-E1F6708778D3.jpeg
    15FA0203-44D8-4814-A4CB-E1F6708778D3.jpeg
    79.8 KB · Views: 23
  • IMG_4944.MOV
    2.9 MB
  • 8435005B-6BED-412C-998E-8A6F63C1E866.jpeg
    8435005B-6BED-412C-998E-8A6F63C1E866.jpeg
    73.8 KB · Views: 22
  • 92FD221E-9CD9-43CC-B992-0913C8A944BE.jpeg
    92FD221E-9CD9-43CC-B992-0913C8A944BE.jpeg
    79.8 KB · Views: 20
  • 8A51A637-3B84-448F-9209-6943716C8C9D.jpeg
    8A51A637-3B84-448F-9209-6943716C8C9D.jpeg
    29.6 KB · Views: 21
  • D89180D1-8868-46F4-893A-3462256531CF.jpeg
    D89180D1-8868-46F4-893A-3462256531CF.jpeg
    41.3 KB · Views: 21

Similar Discussions

Back
Top Bottom