Hivi ni lini propaganda zitakoma kuwa ndio injini ya kuendesha siasa za Tanzania?

Namichiga

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
356
524
Kwanza nianze na ufafanuzi wa kimantiki wa neno utawala, utawala(Excutive) katika nchi ni genge(syndicate), kwa maana ya kuwa ni kundi la watu lililojumuika pamoja na kujiwekea mienendo, kanuni na utaratibu wa kuongoza na kutawala nchi.

Na genge hilo lina msambao kuanzia ngazi za juu kabisa za kiuongozi hadi ngazi za chini kabisa kwa maana ya ngazi ya mjumbe wa nyumba kumi.

Lakini kadri iwavyo ndani yake kuna genge la juu kabisa ambalo tunaweza kuliita inner circle au #Deep state.

Ngazi hii ya juu ya genge, ndio yenye maamuzi ya mwisho kwamba nani awe nani katika kuliongoza taifa na kwa wakati gani.

Ngazi hii ya Deep state kwa kawaida huundwa na watu kutoka kada mbalimbali za kifumo ya kiuongozi na kiutawala, mfano vyombo vya dola kama vile majeshi na idara za kiusalama, na watu kutoka idara mbalimbali za kiserikali ambao wataonekana kuwa na umuhimu wa kimaamuzi na kiushauri katika Jambo husika. Lakini kwa kawaida wengi huwa ni watu waliokomaa na kupevuka akili za kiuongozi hasa hasa wastaafu.

Dhamira iliyo juu ni kuilinda ngazi hii ya kimaamuzi katika nchi ili isivamiwe na watu wa hovyo(labda wenye tamaa)ili kulinda tunu na usalama katika nchi. Kwani kwa neno lililo jepesi ni kwamba likiyumba kundi hili (Deep state) basi limeyumba taifa.

Sasa basi, baada ya ufafanuzi huo hebu nirudi kwenye mada, hapa nchini kwetu tangia nchi ipate uhuru hatukuwahi kupitia mabadiliko makubwa yoyote makubwa ya uongozaji wa nchi tunayoweza kuyatafsiri kwamba yaling'oa genge fulani la kimaamuzi na kupisha genge lingine(hapa namaanisha katika ngazi ya mwisho#deep state), mabadiliko ni labda katikangazi ya pili yake ambayo kwa sisi raia mtaani ndio tunayoiona kubwa, Rais, Makamu,Waziri mkuu n.k.

Lakini kiujumla hayo si mabadiliko thabiti ya kimfumo bali ni vinogesho au upakaji rangi ti.

Lakini swali la kujiuliza ni je, lini wana mikakati na wanafalsafa wa hili genge la deep state wataacha kuzitumia propagandu(utunzi wa matamshi kwa kusudio maalum) kuwa ndio silaha ya mwisho katika mfumo wa uendeshaji wa nchi?

Hebu tazama, wakati wa utawala wa Rais mwendazake John P. Magufuli Watanzania tulilishwa maneno na tukaswagizwa kuyaimba kwamba tangia nchi ipate uhuru, hatukuwahi kupata mkuu wa nchi mzalendo na mpambanaji kama yeye. Hali iliyopelekea hata yeye kama mshika bendera ya genge(Rais) kutapanya maneno na kuwakashifu waliomtangulia wazi wazi.

Lakini kwa kuwa kusudio kuu la kitengo maalum cha watu wa propaaganda ilikua ni kuwaimbisha nyimbo Watanzania ili wao kwa pamoja wajenge utukufu na hatimaye kumpunguzia uzito wa kutawala na tishio kutoka kwa wananchi ambao wao hawaoni mjongeo wa kasi wa hali zao za kimaisha tangia uhuru, basi deep state wao hunyamaza tu ilihali lengo litimie la kuwapumbaza Watanzania na lengo lao litimie la kutawala na kuiongoza nchi bila kutumia nguvu kubwa na kukwepa mihemko kutoka kwa wenye nchi yao.

Sasa ona basi, baada ya kutokea mabadiliko ya kushika usukani kwa kutoka dereva mmoja (yasemekana katolewa na wao wenyewe) na usukani kukabidhiwa dereva mwingine ambaye alikua ndie msaidizi mkuu wa dereva basi nyimbo na matamshi vinabadilika.

Yaani kama ni gari ni lilelile, injini ile ile, lakini ni kama wamepaka langi na kubandika pepe nyuma basi. Na sasa tunaanza kuimbishwa Watanzania.

Leo watu wa propaganda wanaanza kutuimbisha kwamba yule aliepita kaaribu nchi, yule aliepita ni mtu wa hovyo na kiboko ni huyu wa sasa SSH. Lakini ukijaribu kuchunguza kiundani ni watu haohao na ni kundi hilohilo!

Na kiujumla huu ndio umekuwa mfumo tegemezi kwao tangia uhuru,mkanyagie yule na sifia huyu. Alipoingia Mwinyi tukaimbishwa nchi imefunguliwa kwa Ruksa, baadae mkapa tukaanza kuimbishwa Mwinyi alikua mbovu, basi ni hivyo tu ilimradi siku ziende na wana genge wazidi kuitafuna keki ya nchi.

Sasa sisi kama walalahoi wa nchi hii, tunauliza ni lini mtaacha mfumo wenu huu wa kutumia propaganda na nyimbo za mapambio kuwa ndio silaha yenu ya kuendesha nchi?
 
Back
Top Bottom