Hivi ni kweli Yesu alimtokea Nabii Mkuu physically?

Hivi ni kweli Yesu alimtokea Nabii Mkuu physically?

Wewe uliza tu. Lakini tufuate utaratibu.
Dunia hii nipana sana.
Ungekuwa unafahamu mambo ya Physics ningekuletea vitu hapa vingi tu.

Kama wewe hujawahi kukutana na vitu vinavyosemwa basi ni wewe wengine wanakutana navyo.

Ulishawahi kufanya maombi na ukajikuta upo kwenye ulimwengu wa roho ukizungumza na mtu?
Hapana, sasa jibu kwanza maswali machache hapo juu.
 
Biblia inaposema vijana wenu kuona maono unaju maana yake?

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Matendo ya Mitume 2:17
"Biblia inaposema vijana wenu kuona maono unaju maana yake?"
[emoji115][emoji115]
Unajua ni wakati upi hayo yalisemwa, na unajua waliambiwa nani? Specify swali lako ili niweze kukujibu kwa ufasaha.

Na ndiyo maana nikakuuliza. Wewe imani yako ni ipi? Wewe ni Mkristo au Muislam? Kila imani ina kitabu kitakatifu.!
 
Mbona mzee unabisha tu bila kusoma. Hapo imesema nyakati za mwisho.
Niambie nyakati za mwisho ni zipi?
Zimepita, za sasa au baadae?
Hapa tunaongelea biblia mzee
 
Mbona mzee unabisha tu bila kusoma. Hapo imesema nyakati za mwisho.
Niambie nyakati za mwisho ni zipi?
Zimepita, za sasa au baadae?
Kwa mujibu wa maandiko, nyakati za mwisho ni sasa. Haya nawe jibu hilo swali.
 
Kwa mujibu wa maandiko, nyakati za mwisho ni sasa. Haya nawe jibu hilo swali.
Kabla ya kukujibu tukubaliane kwanza kuhusu maono

17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Matendo ya Mitume 2:17

Je, maandiko haya umeyaelewa? Na unajua maana ya maono?
 
Nimeyaelewa sana, na ninajua maana ya maono. Wewe maono yako yalitoka kwa Mungu au Shetani?!

Nikusahihishe kidogo, hayo maono aliyatabiri Yoeli kuwa siku za mwisho ambazo ni sasa, vijana wa Mungu wataona maono(sasa wewe una uhakika ni miongoni mwa vijana tajwa?)

Ili uwe kijana wa Mungu Yoeli alimaanisha ni lazima uishi kwa mujibu wa neno la Mungu kutoka kwenye Biblia yake, je, wewe unatenda sawa sawa na neno la Mungu Mkuu?

Huwezi from nowhere kujiingiza miongoni mwa vijana waliotajwa, kuna utaratibu huo niliosema hapo juu.
 
kwa kweli ugonjwa wa akili unaiteza Dunia inasikitisha kuona wavivu wajinga wanadanganywa na wagonjwa wa akili
 
Nimeyaelewa sana, na ninajua maana ya maono. Wewe maono yako yalitoka kwa Mungu au Shetani?!

Nikusahihishe kidogo, hayo maono aliyatabiri Yoeli kuwa siku za mwisho ambazo ni sasa, vijana wa Mungu wataona maono(sasa wewe una uhakika ni miongoni mwa vijana tajwa?)

Ili uwe kijana wa Mungu Yoeli alimaanisha ni lazima uishi kwa mujibu wa neno la Mungu kutoka kwenye Biblia yake, je, wewe unatenda sawa sawa na neno la Mungu Mkuu?

Huwezi from nowhere kujiingiza miongoni mwa vijana waliotajwa, kuna utaratibu huo niliosema hapo juu.
Mzee mbona unaweka maana yako wakati maandiko yanasema Roho wa Mumgu atamwagwa kwa watu wote?

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Matendo ya Mitume 2:17

Nakusihi soma haya maandiko taratibu uyaelewe usiwahi kunijibu.
Ndipo utakapogundua kuwa kuna gap kubwa huijui biblia. Upo too emotional.

“ ‘In the last days, God says, I will pour out my Spirit on all people. Your sons and daughters will prophesy, your young men will see visions, your old men will dream dreams.
Acts 2:17 NIV
 
Hatuwezi kumpinga moja kwa moja. Huenda ni kweli alitokewa! Pia mtu anaweza kuona tu maruwe ruwe yake akasingizia ni Yesu, na hamuwezi kumbishia kwa sababu hamkuona.
Ni kweli hatupaswi kupinga maana inaweza ikawa ni kweli😅
 
Mzee mbona unaweka maana yako wakati maandiko yanasema Roho wa Mumgu atamwagwa kwa watu wote?

Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
Matendo ya Mitume 2:17

Nakusihi soma haya maandiko taratibu uyaelewe usiwahi kunijibu.
Ndipo utakapogundua kuwa kuna gap kubwa huijui biblia. Upo too emotional.

“ ‘In the last days, God says, I will pour out my Spirit on all people. Your sons and daughters will prophesy, your young men will see visions, your old men will dream dreams.
Acts 2:17 NIV
Unachanganya! Siyo watu wote ni wale tu watakokuwa na neno lake la kweli kwa mujibu wa maandiko na kufuata sheria zake.

Nakuuliza tena unajua ni nani waliolengwa? Soma tena hicho kisa usisome nusu nusu. Nipo na wewe bado mpaka mbivu na mbichi vijulikane.
 
Wewe ndiyo huijui, unaokoteza mistari nusu nusu, soma sura nzima ili upate maana kamili. Lazima ijulikane tu kama ulitokewa na malaika, au hukutokewa au ulitokewa na malaika wa giza au wa nuru. Twende taratibu
 
Unachanganya! Siyo watu wote ni wale tu watakokuwa na neno lake la kweli kwa mujibu wa maandiko na kufuata sheria zake.

Nakuuliza tena unajua ni nani waliolengwa? Soma tena hicho kisa usisome nusu nusu. Nipo na wewe bado mpaka mbivu na mbichi vijulikane.
Unataka kujifunza au unataka tubishane?
 
Sasa muda ndio Sina maana niliongea masaa 3 walinirekodi , wejua kuwa Kuna mahala watu wanaimba masaa yote weupe wananguo nyeupe wanawaka kama mng'ao wa almasi , na nywele zao za gold , Kuna malaika wanapiga tarumbeta na vitu vingine kusindikiza hizo nyimbo huku tulipo siye ilikuwa Kuna kila kitu MATUNDA yakila aina na vijito na vimito Kuna huo mmoja malaika wazamu wanakinga kwenye jagi za gold hizi vinywaji ila sio ya kilevi wanapewa watumbali mbali , na Kuna sehemu watoto tupo ambapo Kuna waliokufa , wanaosubiri kuzaliwa.

Nilikuwa na huyu mtu mweupe kavaa nguo nyeupe sura yake ni ya gold kiasi hata nywele yupo kama Hawa waisraeli sio weupe kama wazungu , huyu ndio alikuwa kanipokea . Ilikuwaje niliumwa sana nilipewa sumu na mtu kwenye sherehe watu walisema sintopona na wakaniacha tu ICU. Sina matumaini hata wazazi walisema si wakupona , ila Sasa duniani nipo mahututi ila roho yangu nilijikuta katikati ya barabara mbili Moja inamaua mazuri sana na haina wanyang'anyi na ingine ilikuwa inayo Tena nyembamba inavimisitu misitu na walikuwepo wanyang'anyi. Mie sikuwa na mizigo but huyu Mzee niliyekutana naye alikuwa kabeba mgongoni mzigo, ila kabla sijachagua pa kwenda niliona watu wanapenda kwenda wengi kwenye hiyo barabara yenye maua na wakifunguliwa huo mlango ni giza nene na wengine wanalia ila nimsururu wa watu wengi sana but here siwezi wamention ni watu wenye wadhifa sana ila Kwa upande wadini , ila wanaenda , kwenye njia nyembamba ni watu wachache , ni real na msione ni utani , ndio nikaanza kuona it's best kujirisk , nanilikuwa curious kwanini watu hawaendi hiyo barabara mana hata watu wanoenda hawafiki kumi , kwenye hiyo barabara nyembamba mbaya sana basi tukaanza safari ila haikuwa rahisi , maana wale wanyang'anyi wao nawatu ambao wanakupa hard time walikuwa ni wengi nilihangaika kufika mwisho, maana ilikuwa sio rahisi mpaka mnakimbizwa mnataka kuuwawa kabisa ili mkate tamaa yakufika . Ila nilifika to the end nikaona Kwa mbali mji mzuri kweli aisee haufanani na wowote hapa duniani ni mkubwa unameremeta kama almasi na gold ni mzuri sana nilikuwa nimechoka ila pembeni mwangu nikaona mto mdogo msafi nikaona nioshe USO nakunywa maji . Nikaanza safari yangu yakwenda kwenye huo mjumba wa heri ,

Sikuwa pekee yangu nilikuwa na yule Mzee yule Mzee alikuwa amechoka kushinda Mimi ila nilienda naye hadi tukafika . Kutaka kuingia mlangoni umefungwa na koki .kubwa zuri la gold Ile tu tumelishika akatoka kijana mrefu kama hao hao ninao walezea wananguo nyeupe wote , nikaulizwa jina nikaambiwa lipo ila Kwa yule Mzee akaambiwa halipo ngoja , Mimi nikafunguliawa ndani ndio nikaanza kwenda kuona humo ni pazuri ila waleo sijapaelewa waleo maana mara Kuna wanyama ila hawang'ati , Garden ninzuri watoto wanacheza , kawaida ila Sasa unajua tu huku ni paajabu Kuna mahali hurusiwi kuingia maana humo Mungu yupo na wale wakina Ambraham na sijui isaka na yakobo ila Kwa wanaoishi humo ukikubali kubaki unamwona ila mie sikuwa nimekufa exactly so baada ya siku hizo kadhaa humo nikaonyweshwa wazazi wangu walikinililia siamki wakimwomba Mungu nirudi duniani , wakauliza unaenda duniani au unabaki huku nikaona ngoja nirudi , na wakaniambia ukirudi utapata shida sana sana nikidhani niuongo ila kweli nilipitia kazi ambayo hata shetani hajawahi.

Nikarudishwa duniani na hadi Sasa mie nipo napambania kombe good day mkiamini sawa msipoamini sawa ila hapo ni kidogo sio hadithi yote Kuna mengi sana yakuhadithia tena kule kuzimu it's real watu wanachomwa watu wanasaga meno eti
Mhhh we jamaa,siku ya mwisho si ndo kuna mambo ya kuchomana,we ulivyoenda umekuta tayari watu wanachomwa aloo,halafu swala la kuona watu weupe nalo mhh mkuu siku unaota hiyo ndoto ulikula kweli?
 
Kujifunza, pili ni kuhojiana ili ukweli ufahamike(kuhakikisha ulichosema kama ni kweli kwa mujibu wa Biblia). Hivyo tu!
Mzee sitaki nianze kufundisha somo la bible. Sitaki nianze kufundisha theology hapa.
Ninachokuomba tu tujadiliane kwa kutumia references.
Nakusihi ulete references kutoka kwenye maandika kuweza support hiki unachokisema.

Nimekuwekea Mistari mingi tu kutoka kwenye bible lakini wewe hapa unakuja na maneno matupu.

Ndio maana ninakuambia you a too emotional.
Leta references inayosema kuwa Roho wa Mungu siyo kwa watu wote.

Asante
 
Mhhh we jamaa,siku ya mwisho si ndo kuna mambo ya kuchomana,we ulivyoenda umekuta tayari watu wanachomwa aloo,halafu swala la kuona watu weupe nalo mhh mkuu siku unaota hiyo ndoto ulikula kweli?
Ndioo hivyoo nilivyoota mie demu sio jamaa
 
Back
Top Bottom