Mkulungwa01
JF-Expert Member
- Jul 14, 2021
- 3,977
- 5,352
Ni siku mpya leo. Habarini!
Ndugu Waislamu nawatakia muendelezo mwema wa mfungo wa Ramadan!.
Tukianza na member mmoja humu akiitwa BOOM1, yeye anasema kuwa alitokewa na Yesu Kristo akiwa Mtwara na akaambiwa "fanya kazi yangu". Japokuwa huyu BOOM1 alisimulia kana kwamba ilikuwa ni kawaida kwake na hakushangaa sana, hii inavuta 'attention' kutoka kwa yeyote mwenye 'reasoning' na akili timamu kuhoji.
Anasema alimuona mtu kavaa mavazi meupe anameremeta huku akitabasamu, ila hakusema alijua vipi kuwa ni Yesu Kristo mwenyewe.
Tuje kwa huyu mwingine anaitwa Venus Star, huyu anasema miaka 35 iliyopita alitokewa na malaika akiwa Ilboru, anajisomea darasani usiku, yaani 'prepo', akachukuliwa mpaka sehemu wafu walipo. Anyway nachefukwa nisiendelee.
Haya tuje kwa wa mwisho GeorDavie, huyu anajiita nabii mkuu na yupo Kisongo Arusha. Anasema aliwahi kutokewa na Yesu Kristo 'live' kabisa yaani 'physically' na akapewa funguo 'physically' pia.
Huyu naye ana mengi ya kumuhoji kwenye hili.
Najiuliza: Je, ni kweli hawa watu walitokewa na Yesu au walikuwa wanadanganya? Mtu akiwa na njaa huwa anaona maruwe ruwe, je, hawa watu walikuwa wana shibe wakati wakitokewa na Yesu? Vipi kuhusu utimamu wa akili zao? Hawakuwa ndotoni? Hawakuwahi kujihusisha na utumiaji wa vilevi mfano bangi na pombe hapo kabla?
Jamani, naona kama baadhi ya watu wanamchezea sana huyu Yesu na wanamchukulia poa sana. Jamani hebu mliowahi ku 'experience' hii hali jitokezeni ili huu wasiwasi wengine ututoke, mnatupeleka kasi sana ndugu zangu, punguzeni.
Au mnafanya haya kwa sababu mnajua hata watu wakihoji hakuna ushahidi wa kusema ninyi waongo? Kwa sababu ya hofu/uoga wa kiimani?
Yaani mtu anakurupuka tu 'from nowhere' na kudai Yesu kamtokea, mara ooh malaika kanitokea, sasa huu ni wakati wa kujua mbivu na mbichi. Kama wanadanganya, je, wana ajenda gani? Ili wapate nini? Wanatumwa na nani?
NB: maneno ndani ya funga semi ni ya kiingereza, samahanini kwa mliotajwa ikiwa mtachukulia suala hili kwa uhasi, nimewataja kwa nia njema ya kuufahamu ukweli wa mliyoyasema.
Wasaalam!