Hivi ni kweli Yesu alimtokea Nabii Mkuu physically?

Hivi ni kweli Yesu alimtokea Nabii Mkuu physically?

Y
Yesu haji physically ila kuna mazingira yanakukuta kama kwenye ndoto au maono au unaomba unasikia sauti. kujua ni Yesu kweli wa nazareth au wa tongereni ndio shida. kama mizimu inaweza kumtokea mtu kwanini Yesu asiweze?
Kwasasa Yesu ni roho hawezi kuja phisically, hizo ni story tu.
 
Kama unafanya meditation mambo haya ni ya kawaida sana.

Unaweza ukanya Astral Projection.
Mimi mbona nafanya hivyo mara kibao tu. Ninaweza nikaondoka kwenye mwili wangu na kuuona pale pembeni.

Kuna kitu kingine kinaitwa Lucid Dreaming unaweza kusafiri ukiwa kwenye ndoto na kuona yatakayotokea kesho.

Wale wanaosema ni matatizo ya akili huenda ni wazembe na wavivu wa kuujua Ulimwengu.

Tofauti na Physics kuna Metaphysics.

Leta maswali nitajibu na kuonesha jia za kufikia kuonana na Malaika, Yesu, Mizimu au Watu wa zamani waliokufa.
Kwa mfano kwa hapa nikitaka kuonana na kuongea na Nyerere au Hitler ninafanya vitu gani?
 
Wale mnaokataa haya mambo ni washamba wa Spiritual World. Kama wewe hujawahi kumuona basi kaa kimya wenzako wamemuona na wakaongea naye.
Wamemuona Yesu Kristo au Yesu wa Buza mkuu? Kristo huyu huyu au?
 
Kuna mazingira mawili unapotokewa na kitu ukathibitisha kwamba ni kweli basi kile kitu ulishakijua kabla ina maana hao watu sura ya yesu wanaijua na wamehakikisha.

kingine kuna mauzauza kama watu wa hallucinations ukichanganya na kufikiria kitu kwa sana baada kinweza kuja hata ndotoni kama ndoto ila unakuwa kama wewe upo macho vile ...
Ni kweli.
 
Kama kweli imetokea hivyo, kuna watu wana matatizo ya afya ya akili, baadhi ya matatizo haya yana dalili za hallucinations na kuona mauzauza kama hizo.

Inafaa kuangaliwa na wataalam wa mambo ya afya ya akili ili kupata uhakiki wa habari hizi.
Najaribu kukutafakari namna ambavyo hupinga uwepo wa Mungu halafu leo waliutangazia umma kutokewa kwao unawaita wametokewa na maluweluwe!
Deep down unaamini kuwa Mungu yupo na Yesu yupo... naishia hapa.
 
Kama watu mnaamini Paulo alitokewa na Yesu, mnaamini Musa alitokewa na Mungu na pia mnaamini kwamba Mohamed alitokewa na allah bila ushahidi wowote kwa nini msiamini kwamba Yesu alimtokea Nabii Mkuu Geo Davie ama Zumaridi?

Watu wa dini mmejaa unafiki, mnachagua cha kuamini na cha kuacha.
Una hoja nzito na nzuri sana
 
Kwa mafundisho ya imani tuliyojengwa nayo ujio wa Yesu Kristu hautakuwa wa mtu mmoja mmoja kama hao wapendwa wanavyo jaribu kutuaminisha. LABDA kama ni maono.
 
Najaribu kukutafakari namna ambavyo hupinga uwepo wa Mungu halafu leo waliutangazia umma kutokewa kwao unawaita wametokewa na maluweluwe!
Deep down unaamini kuwa Mungu yupo na Yesu yupo... naishia hapa.
Najaribu kukuelewa lakini sikuelewi.

Kuna contradiction gani katika maneno yangu?

Umejuaje deep down naamini Mungu yupo? Umejuaje ninachofikiri dep down?
 
Yesu haji physically ila kuna mazingira yanakukuta kama kwenye ndoto au maono au unaomba unasikia sauti. kujua ni Yesu kweli wa nazareth au wa tongereni ndio shida. kama mizimu inaweza kumtokea mtu kwanini Yesu asiweze?
Usifanye conclusion ya unachokisema
Musa alitokewa na MUNGU physical , licha ya kutooneshwa tu sura

HESABU 12: 6-8​

Kisha Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Sikilizeni maneno yangu: Kama kuna nabii miongoni mwenu, mimi Mwenyezi-Mungu hujifahamisha kwake katika maono na kuongea naye katika ndoto. Lakini kumhusu mtumishi wangu Mose, hali ni tofauti kabisa. Yeye ana jukumu la kuwatunza watu wangu wote. Mimi huongea naye ana kwa ana, waziwazi na si kwa kutumia mafumbo. Yeye huliona umbo langu mimi Mwenyezi-Mungu. Kwa nini, basi, hamkuogopa kusema vibaya dhidi ya mtumishi wangu Mose?”
 
Ni siku mpya leo. Habarini!

Ndugu Waislamu nawatakia muendelezo mwema wa mfungo wa Ramadan!.

Tukianza na member mmoja humu akiitwa BOOM1, yeye anasema kuwa alitokewa na Yesu Kristo akiwa Mtwara na akaambiwa "fanya kazi yangu". Japokuwa huyu BOOM1 alisimulia kana kwamba ilikuwa ni kawaida kwake na hakushangaa sana, hii inavuta 'attention' kutoka kwa yeyote mwenye 'reasoning' na akili timamu kuhoji.

Anasema alimuona mtu kavaa mavazi meupe anameremeta huku akitabasamu, ila hakusema alijua vipi kuwa ni Yesu Kristo mwenyewe.

Tuje kwa huyu mwingine anaitwa Venus Star, huyu anasema miaka 35 iliyopita alitokewa na malaika akiwa Ilboru, anajisomea darasani usiku, yaani 'prepo', akachukuliwa mpaka sehemu wafu walipo. Anyway nachefukwa nisiendelee.

Haya tuje kwa wa mwisho GeorDavie, huyu anajiita nabii mkuu na yupo Kisongo Arusha. Anasema aliwahi kutokewa na Yesu Kristo 'live' kabisa yaani 'physically' na akapewa funguo 'physically' pia.
Huyu naye ana mengi ya kumuhoji kwenye hili.

Najiuliza: Je, ni kweli hawa watu walitokewa na Yesu au walikuwa wanadanganya? Mtu akiwa na njaa huwa anaona maruwe ruwe, je, hawa watu walikuwa wana shibe wakati wakitokewa na Yesu? Vipi kuhusu utimamu wa akili zao? Hawakuwa ndotoni? Hawakuwahi kujihusisha na utumiaji wa vilevi mfano bangi na pombe hapo kabla?

Jamani, naona kama baadhi ya watu wanamchezea sana huyu Yesu na wanamchukulia poa sana. Jamani hebu mliowahi ku 'experience' hii hali jitokezeni ili huu wasiwasi wengine ututoke, mnatupeleka kasi sana ndugu zangu, punguzeni.

Au mnafanya haya kwa sababu mnajua hata watu wakihoji hakuna ushahidi wa kusema ninyi waongo? Kwa sababu ya hofu/uoga wa kiimani?

Yaani mtu anakurupuka tu 'from nowhere' na kudai Yesu kamtokea, mara ooh malaika kanitokea, sasa huu ni wakati wa kujua mbivu na mbichi. Kama wanadanganya, je, wana ajenda gani? Ili wapate nini? Wanatumwa na nani?

NB: maneno ndani ya funga semi ni ya kiingereza, samahanini kwa mliotajwa ikiwa mtachukulia suala hili kwa uhasi, nimewataja kwa nia njema ya kuufahamu ukweli wa mliyoyasema.

Wasaalam!
Watu wanatokewa na majini wanasema yesu
 
Kama unafanya meditation mambo haya ni ya kawaida sana.

Unaweza ukanya Astral Projection.
Mimi mbona nafanya hivyo mara kibao tu. Ninaweza nikaondoka kwenye mwili wangu na kuuona pale pembeni.

Kuna kitu kingine kinaitwa Lucid Dreaming unaweza kusafiri ukiwa kwenye ndoto na kuona yatakayotokea kesho.

Wale wanaosema ni matatizo ya akili huenda ni wazembe na wavivu wa kuujua Ulimwengu.

Tofauti na Physics kuna Metaphysics.

Leta maswali nitajibu na kuonesha jia za kufikia kuonana na Malaika, Yesu, Mizimu au Watu wa zamani waliokufa.
Mkuu unafikiri watakuamin bas kumamka sio kwa kila mtu bora ukaushe tu
 
Back
Top Bottom