Mshukuru Mungu kwa kila jambo

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,460
Habari wadau wote

Kuna nyakati mbalimbali tunazopitia katika maisha yetu ziko nyakati za furaha , huzuni, kicheko, kupata na kukosa kuwa na kitu ama kutokuwa nacho, kuwa pekee au kuwa na watu, kuwa mtu wa juu ama wa chini yote katika maisha yapo hivyo huna budi kupambana na kujifunza na kumshukuru Mungu kwa yote upitiayo

Yawe mambo ya kutia moyo au kukatisha tamaa wewe mshukuru Mungu kwa kukupa uhai na afya njema, kuna ambao wako hospitallini hawajiwezi kabisa hawana tumaini lakini katika kipindi hicho huna budi kumshukjru Mungu kwani ndiye atupae kuishi na kutoishi pia ndiye atuondoleae wapendwa wetu ama atupae wapendwa wetu shukrani za kwa Mungu milele.

Zab 136:1-25Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.​


Hivyo huna budi kumshukuru Mungu kwa hali zote unazopitia hata kama unakosa chakula au unapata chakula, wewe jifunze kumshuukuru Mungu

Tunavyoenda kufunga mwaka huuu angalia mangapi ambayo Mungu amekutendea, mangapi ambayo amekulinda , je umemlipa nini Mungu kwa pumzi unayopumua, uhai , jifunze kurudisha shukrani kwa Mungu aliyekuumba sema asante Mungu kwa kuwa wewe umwema kwangu

NIWATIKIE MWAKA MPYA MWEMA WENYE BARAKA NA FURAHA NA AMANI TELE TUWE WATU WA SALA KWA MWAKA UJAO 2024

Nawapenda sana mabestito wangu wa jf

Wasalaamu;
Ladyf aka mama mfundaji
 
umevuka inabidi kumshukuru Mungu tena kuuona mwaka mwingine na mwombe Mungu akuwezeshe kukabiliana na mambo na changamoto za mwaka huu mapema
 
Back
Top Bottom