Hivi ni kweli wanawake Tanzania hawabaki wanamme!.

Hivi ni kweli wanawake Tanzania hawabaki wanamme!.

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Nimejaribu kudurusu sheria za Tanzania bara na hasa sheria ya Makosa ya Kujamiiana au kwa lugha ya kwini wa Uingereza ‘Sexual Offences Special Provisions Act’ (1998) ambayo ililetwa na serikali ili kuzifanyia marekebisho sheria kadha wa kadha za makosa ya jinai kama vile Kanuni ya Adhabu, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai n.k.

Nimepatwa na mshangao kugundua kuwa pamoja na mabadiliko mapya katika sheria ya kanuni za Adhabu na hasa katika makosa ya utu sura ya 15. Kuanzia ibara ya 129A-162, hakuna kipengele kinachomtia hatiani mwanamke kwa kosa au makosa ya kumbaka mwanamme badala yake ni mwanamume ameandamwa kwelikweli na hii sheria.

Hivi ni kweli wanawake Tanzania hawabaki wanamme?.

Hivi ni kweli kukosekana kwa sheria kunawafanya wanamme wasitafute haki yao kwenye vyombo vya sheria baada ya kubakwa na wanawake.

Kwenye nchi kama Zimbabwe tunasikia kesi za wanawake kuwabaka wanamme kama ilivyotokea katika moja ya tukio hili,

Bulawayo24 NEWS | SA man raped by 3 Zimbabwe 'sperm harvesters'

Hata kwenye nchi za Magharibi vile vile wanamume wanabakwa kama ilivyotokea katika moja ya tukio hili,

IT HAPPENED TO ME: I Was Raped By a Woman (And Then Dated Her For Two Years) | xoJane
na hii kesi,


​Canadian Man Sexually Assaulted By Four Women, Showing Rape Goes Both Ways - PolicyMic

Ninafikiri Serikali ameshindwa kulinda haki za wanaume kisheria kama inavyotakiwa katika Katiba ya nchi (1977) sura ya tatu, ibara ya 13 (1-2) pale inaposema,

13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.

Kwa nini wanawake tu ndiyo watambuliwe kama watendewa makosa wakati hata wao pia wanayatenda makosa hayo hayo kama viashiria binavyoonyesha sehemu mbali mbali.



 
^^
Wanakuja wazee wa jalada na somo gumu kabisa la evidence!
Mi simo
^^
 
sheria inasema anayemuingiza mwenzake ndio kabaka wakiamin kua ni vigumu kwa mwanaume kusimamisha kama hutaki.....
 
sheria inasema anayemuingiza mwenzake ndio kabaka wakiamin kua ni vigumu kwa mwanaume kusimamisha kama hutaki.....
Unaposema ni vigumu ina maana inawezekana.

Kwa nini huo uwezekano usiwekewe sheria kwa sababu case kama za Zimbabwe zinaonyesha mwaname anawekewa kinywaji ambacho kinamfanya apate hamu ya kufanya tendo la ndoa bila kupenda.

Hili tukio linaonyesha hata kama mwanamme atakuwa hataki lakini kunafikia point anakuwa hana uwezo wa kukataa kama ilivyotokea katika tukio hili,

Shocking Caught Live : Chinese Woman ‘Rapes’ Passing Man on Street.


Bold and Powerful Chengdu Woman “Rapes” Man on Street: Saw a ferocious woman at Jiuyanqiao. Probably drank too much [is drunk]! Pressed a man passing by onto the ground, took off her pants, and then suddenly climbed on top of him. At first, the man even resisted for a moment! But ultimately surrendered to the woman’s violent rape, pulled up his underwear and walked away red in the face! After pulling up her pants, the woman walked along Jiuyanqiao crossing the street… Numerous male netizens on Weibo today proclaimed that they’re going to Chengdu to “wait by the tree for a rabbit”

Shocking Caught Live : Chinese Woman

attachment.php
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    79.4 KB · Views: 543
Wakati wa mchakato wa maoni ya katiba mpya, ulikua wapi?? Ila hata hivyo hujachelewa bado huenda wakakuskia
 
Unabakwa vipi?ukiwa huna hisia mshedede hausimami.
 
Shocking Caught Live : Chinese Woman mkuu ndio maana ikaandikwa kabisa kuwa ni shockina kuonesha wazi kuwa hilo sio jambo la kawaida hata kidogo,na mi kwa upande wangu without considering sijui hiyo shocking news,mwanaume hawezi kubakwa labda awe ametaka.
 
Suala la mwanaume kubakwa ni tata sana, mi naona haliingii akilini.
Labda kwa mtutu wa bunduki kwa mbaaali inaweza leta maaana
 
Wakati wa mchakato wa maoni ya katiba mpya, ulikua wapi?? Ila hata hivyo hujachelewa bado huenda wakakuskia
Mkuu hizi ni sheria zitokanazo na sheria mama. Hazihitaji mchakato wa sheria kwa sababu zinatokana na kipengele cha haki za binadamu na usawa kwenye katiba ambacho kwa sasa kipo kwenye Rasimu ya Katiba.
 
Mwanamme akibakwa anabaki na michubuko? Tutapataje ushahidi?
Maana ni hadi ithibitike ilipenyezwa bila ridhaa, na ushahidi unapimwa kwa michubuko. Akitumia lubricant mbakwaji kaumia.

Sasa mwanamme habakwi ila anashawishiwa tu.
 
Hivi demu akibakwa akafurahia utamu hapo sheria imekaaje?yaani mwanzoni kapiga kelele lakini akaanza kuusikilizia utamu
 
Katika elements znazotumika kugundua kama mtu kabakwa, mojawapo ni "penetration", mwanamke hana penis, how come abake??
 
Mkuu hizi ni sheria zitokanazo na sheria mama. Hazihitaji mchakato wa sheria kwa sababu zinatokana na kipengele cha haki za binadamu na usawa kwenye katiba ambacho kwa sasa kipo kwenye Rasimu ya Katiba.

Basi akina warioba wamekuskia
 
Hivi kubakwa kwa mwanaume ni lazima uume uingie ukeni?
Sheria ya Kanuni za Adhabu ibara ya 130 (4) inasema,
(4) Kwa madhumuni ya kuthibitisha kosa la kubaka-
(a) mpenyo japokuwa ni mdogo unatosha kuthibitisha tendo la ndoa
muhimu katika kosa;
Kwa mtazamo wangu ninafikiri hata kugusisha kiduchu kwa nia ya kutenda katika macho ya sheria inahesabika ni kubaka.
 
Unabakwa vipi?ukiwa huna hisia mshedede hausimami.
Hebu soma hii article,

A SOUTH AFRICAN man was last week sexually abused and robbed by three women in Mutare, police said.

The man lost a pair of shoes, his passport, a Samsung Galaxy 4 cellphone, satchel with clothes and US$900 cash.

Chief police spokesperson Senior Assistant Commissioner Charity Charamba said the man from Mafikeng in South Africa boarded a bus at Beitbridge border post for Mutare.

He befriended an unidentified woman in the bus and the two got off at Sakubva bus terminus and were picked up by a Toyota Ipsum, white in colour with unknown registration numbers.

The vehicle was being driven by a woman who had two passengers, a woman and a man, Snr Asst Comm Charamba said.

They drove to a bar in Sakubva for some drinks and later the man was offered accommodation by the woman from the bus.

It is alleged that the assailants drove towards the city and parked the vehicle soon after the flyover, off the road along Herbert Chitepo Street.

The South African was ordered by the man out of the vehicle and was forced to be intimate with the three women.

After the act, the complainant was assaulted all over the body by the unknown assailants, Snr Asst Comm Charamba said.

He was ordered to surrender all his belongings and the cash. He complied and the assailants drove off.

A report was made to the police and investigations are still in progress.

"We implore the public to be wary of strangers. Investigations are currently in progress," Snr Asst Comm Charamba said.

In April, a Chegutu man became the latest victim of rape after he was offered a lift by women who went on to inject him with an unknown substance before taking turns to be intimate with him.

A 33-year-old soldier was reportedly forced to drink an unknown substance by three women who later took turns to be intimate with him on the outskirts of Gweru in December last year.

Numerous attacks, thought to be for ritual purposes, have been reported in the past few years in various parts of the country.

No arrests have been made so far.
 
Shocking Caught Live : Chinese Woman mkuu ndio maana ikaandikwa kabisa kuwa ni shockina kuonesha wazi kuwa hilo sio jambo la kawaida hata kidogo,na mi kwa upande wangu without considering sijui hiyo shocking news,mwanaume hawezi kubakwa labda awe ametaka.
Mkuu, kwani wanamme kubaka wanawake toka lini likawa ni jambo la kawaida?. Kama isivyo jambo la kawaida kwa mwanamme kubaka mwanamke, hata mwanamke kubaka mwanamme vile vile siyo jambo la kawaida. Hata hivyo, inatokea kama habari hii ilivyo lakini cha ajabu Tanzania nguvu zote za kisheria zimemkinga mwanamke peke yake.
 
Back
Top Bottom