Page 94
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 5,204
- 15,198
Salaam Wakuu,
Hii imekuwa ni tofauti kama utaratibu unavyopasa. Kikawaida,wanufaika wote wa mikopo kutoka HESLB wamekuwa wakipewa fedha za kujikimu kila baada ya siku 60 yaani miezi miwili. Lakini mpaka sasa kuna vyuo ambavyo imeshapita mpaka miezi mitatu na huu tunaelekea wa 4 (yaani mwezi mmoja mbele zaidi ya kipindi kinachopaswa) hakuna fedha za kujikimu kwa wanufaika.
Kila jitihada zinapofanyika bodi wanadai fedha hakuna mpaka wazipate kutoka hazina. Sasa cha kujiuliza,je hazina haioni umuhimu wa kutoa hizi fedha? Je,ni kweli hazina haijatoa fedha au bodi ndo inazingua?
Hali imekuwa mbaya vyuoni. Hakuna pesa kwa ajili ya matumizi ya chakula. Mbaya zaidi kuna wengine wanategemea kutumia fedha hizo kwa ajili ya kulipia ada (sehemu iliyobaki). Mitihani inatarajia kuanza wiki ijayo na wale ambao hawajakamilisha malipo ya ada hawaruhusiwi kufanya mitihani.
Jamani,Hazina tunaomba roho ya huruma iwaingie. Hizi fedha hatuzipati kama msaada. Ni za kuzirudisha tena ikiwa na riba. Hii ni haki yetu ya Msingi kabisa.
Dada zetu huku chuoni wanaangamia. Hatujui kinachowaweka mjini kwa sasa. Hakika kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia ambacho siyo kwa matakwa yao Bali ni hali mbaya ya kiuchumi inayotokana na kuchelewa kwa fedha hizo.
Mh Rais uliahidi kwamba wanafunzi watapewa fedha zao kwa wakati. Hazina ipo chini yako na hakika kauli yako ndo itawalazimu kutoa hizo fedha. Tunakuomba Mkuu wetu utusaidie. Hali inasikitisha.
Hata kupiga msuli hauingii. Madude hayapandi kichwani kwa sababu tumboni kupo empty.[/COLOR=RED]
Nimeandika kwa rangi nyekundu maana hakika Uzi huu ni wa masikitiko.