Hivi ni kwel hakuna namna!!!!!

Ngai Moko

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
1,281
1,699
Habar zenu wanaJF, ni wiki ya pili sasa toka niambiwe mwanangu hawezi kupona ni kama nimechanganyikiwa vile, kuna kipindi mwanangu aliugua ikabidi Mama yake ampeleke hospital kama ilvo kawaida ya mgonjwa kupelekwa sehem husika, mtoto alitibiwa kwa kuchomwa sindano na dawa kadhaa zlitolewa.

Baada ya siku mbili ile sehemu aliyochomwa sindano ilileta mushkel kwa maana mtoto hakuweza tena kusimama kwa miguu yote ule mguu alochomwa sindano ndo ulikua shida. Ilibid tumrudshe hospitali na jibu tulopewa ni kua "Mguu umepooza, mrudsheni nyumban hakuna namna nyingine".
Hivi ni kwel hakuna namna nyingine!
 
Pole sana mkuu! mwanao mlimpeleka hosptali gani kuchomwa hiyo sindano?
Pengine itakuwa nesi/daktari aliyemdunga alikosea ktk uingizaji wa sindano akachoma hadi mfupa!

Au mtoto alikuwa anarusha miguu pindi sindano inamwingia ikapelekea mdungaji kukosa umakini wa udungaji!

Nakushauri uende hospitali kubwa kwa uchunguzi zaidi na hakikisha unarudi kupata maelezo ya kina kule alikopatwa tatizo.
Pole sana maishani mwangu nishawahi shuhudia wawili walipata ulemavu kwa style hii!
 
Habar zenu wanaJF, ni wiki ya pili sasa toka
niambiwe mwanangu hawezi kupona ni kama
nimechanganyikiwa vile, kuna kipindi mwanangu
aliugua ikabidi Mama yake ampeleke hospital
kama ilvo kawaida ya mgonjwa kupelekwa sehem
husika, mtoto alitibiwa kwa kuchomwa sindano na
dawa kadhaa zlitolewa.
Baada ya cku mbili ile sehemu aliyochomwa
sindano ilileta mushkel kwa maana mtoto
hakuweza tena kusimama kwa miguu yote ule
mguu alochomwa sindano ndo ulikua shida. Ilibid
tumrudshe hospitali na jibu tulopewa ni kua
"Mguu umepooza, mrudsheni nyumban hakuna
namna nyingine". Hivi ni kwel hakuna namna
nyingine!!!!!!!!!!!!
pole,mkuu fanya hv:nenda hospitali kubwa,ukitoka uko pia waweza jaribu mitishamba,ukitoka uko Mpeleke katika Maombi kama ni mkristo nenda kanisani,kama mwislamu onana na viongozi wako wa dini
 
Hakuna lisilowezekana, ebu badili hospitali haraka sana hata kama ni kutumia gharama kubwa
 
Physiotherapy can help. Kama ni muda mfupi tu umepita( chini ya miezi 6) mpeleke kwa wataalam wa mazoezi. Uko wapi kwani mkuu?
 
Pole sana mzazi. I can feel it. Ila hakuna kinachoshindikana ukimwamini Mungu. Mpeleke mtoto hospital kubwa bila kusahau kumlilia Mungu kwa ajili ya mtoto. Nina Imani kubwa kuwa mtoto atapona. Pole sana.
 
Pole sana, kama alichomwa mshipa wa fahamu (nerve) basi tatizo kama hilo linaweza kutokea.

Mpeleke hospital kubwa akapate multivitamins na physiotherapy japo Siyo 100% ila itamsaidia
 
Inasikitisha sana.yaani hao waliomchoma sindano wanajibu kiurahisi tu kwamba hakuna namna.hakiya mungu ningemtandika daktari sijui nesi aliyesababisha majanga hayo.pole sana.
 
Kwake yeye aaminiye hakuja jambo lisilowezekana, teta na MUNGU akupe njia ya kutoka, maana MUNGU kwetu sisi ni MUNGU wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye, hiyo njia mtoto anayoiendea ni ya kwenda mautini Muombe amurehemu.
 
Pole sana mkuu! mwanao mlimpeleka hosptali gani kuchomwa hiyo sindano?
Pengine itakuwa nesi/daktari aliyemdunga alikosea ktk uingizaji wa sindano akachoma hadi mfupa!
Au mtoto alikuwa anarusha miguu pindi sindano inamwingia ikapelekea mdungaji kukosa umakini wa udungaji!
Nakushauri uende hospitali kubwa kwa uchunguzi zaidi na hakikisha unarudi kupata maelezo ya kina kule alikopatwa tatizo.
Pole sana maishani mwangu nishawahi shuhudia wawili walipata ulemavu kwa style hii!

Mkuu ukichoma mfupa huwezi kusababisha paralysis.Huyo mtoto amechomwa mshipa wa fahamu(nerve) na kama alichomwa matakoni basi kuna uwezekano sciatic nerve ndio imejeruhiwa

Mleta mada jaribuni kumpeleka mwanenu hospitali kubwa mnaweza pata solution
 
Ni kweli mkuu. Chamsingi mleta mada afanye kila liwezekanalo amuwahishe mtoto kwenye huduma ya uhakika.
 
Hiyo ni moja ya madhara ya kuchomwa sindano. Yawezekaba mishipa ya fahamu iliumizwa au alipata jipu sehemu iliyochomwa, lakini pia yawezakuwa ni uzembe wa mchoma sindano.

Kosa kubwa kabisa walilofanya hao wadumu ni maelezo waliyokupa kwamba hakuna chakufanya zaidi, na kwa kosa hilo waweza hata kuwashtaki. Mtoto wako anaweza kupona na kurudia hali yake ya awali. Muwaishe hospitali kubwa iliyokaribu nawe kwa msaada zaidi.. kama aliumizwa mishipa ya fahamu atahitaji physiotherapy zaidi na baada ya muda ataweza kuwa vizuri.
 
Hakika maisha yana mitihani kila aina, usikate tamaa jaribu kwa uwezo wako wote huwenda atarudi katika hali ya kawaida
 
Habar zenu wanaJF, ni wiki ya pili sasa toka niambiwe mwanangu hawezi kupona ni kama nimechanganyikiwa vile, kuna kipindi mwanangu aliugua ikabidi Mama yake ampeleke hospital kama ilvo kawaida ya mgonjwa kupelekwa sehem husika, mtoto alitibiwa kwa kuchomwa sindano na dawa kadhaa zlitolewa.

Baada ya siku mbili ile sehemu aliyochomwa sindano ilileta mushkel kwa maana mtoto hakuweza tena kusimama kwa miguu yote ule mguu alochomwa sindano ndo ulikua shida. Ilibid tumrudshe hospitali na jibu tulopewa ni kua "Mguu umepooza, mrudsheni nyumban hakuna namna nyingine".
Hivi ni kwel hakuna namna nyingine!

mtoto wa kaka yangu alipata hiyo shida akapelekwa CCBRT anaimprove siku hizi ameanza kutembea
 
Ahsanten ndugu zang kwa ushaur wenu na nliacha kazi zang na kufanyia kazi ushaur wa kila alyetoa ilimradi kupata ufumbuzi w tatzo, majibu yalikuja kua ni mshipa ndo uliathiriwa hvo nlionana na wataalamu wa Physiotherapy na kunpa maelezo namna ya kumpa mazoez na yafanyke baada ya kila masaa ma4. Pia nlionana na wale wa dawa asili nao kuna dawa nlipewa na wakanshaur niwe namchua kwa mafuta ya zaitun hvo npo katka kpnd krefu kusubir matokeo huku nkitafuta namna nyingne ya tiba, Ahsanten wote.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom