Hivi ni kwanini mahari haikopesheki?

Hivi ni kwanini mahari haikopesheki?

Nimefikiria hili jambo nikagundua laiti mahari yangekuwa yanakopesheka wasichana wengi wangekuwa kwa waume zao maana kuna walioshindwa kuoa kwa kukosa mahari,na kuna waliobaki na pete za uchumba baada kwa kuachwa na mwanaume kwa kukosa hela ya mahari kwa gharama kubwa..
Laiti hii sheria ingebadilishwa labda kukawa na wadhamini pale mwanaume umempenda mwanamke na mwanamke akakubali kuolewa kama uwezo wa mahari hauna ukaruhusiwa kuoa kukawa na form maalum ya kujaza kuwa unadaiwa mahari kiasi fulani na mtu fulani hapa baadae baada ya kuishi ndo ulipe,,hii naona ingesaidia madada zetu kuolewa na kupungua kuzeekea nyumbani..
Naomba kuwasilisha..
kipo chama cha vijana wasiooa Mkuu wanapigania tuwe tunaoa kwa bei elekezi ya sh 50000
 
Usipende kukopa, mimi nasema ,mtu mkopaji huishia kua mwovu sababu kulipa huwa nimatanga namatokeo yake huishia kuchukia tu.

Alafu ,,ukiwa mtu wa madeni sanaaa ,ufiki mbali
 
Kama msichana ni mtu mzima mwambie kama anakupenda muanze maisha, akitanguliza mahari tafuta mwingine kwani mahari sio kipimo cha maisha yenu. Nijibu swali - inakopesheka kwani mnaishi kwanza mkipata chochote kwa mikono yenu mnawapa wazazi kama zawadi na sio mahari kwani hakuna kilichouzika. Zawadi kwa pande zote kwani wote wamehusika Katika kuwatunza. Kwangu nikidaiwa mahari itabidi waondoke na mtoto wao ili nikipata nipeleke,
 
Nadhani vijana wa sasa hivi ni wageni sana katika mambo haya.

Suala la Mahari ni suala la kimila zaidi na kwa waislamu ni suala la kiimani.
Ni jamii husika ndio inayopanga mahari, na jamii ya muoaji ndio inayolipa hiyo mahari.

Kwa makabila mengi mahari huwa hivi.
1/Mali za kiasili(Kama mifugo nk)
2/Ni suala la majadiliano.
3/Haipaswi kulipwa yote kwa mkupuo.
4/Haipaswi kwisha(Utaendelewa kudaiwa!!)
 
mbona watu tumeo bure tu. tafuta demu unaemkubali anza kugonga, mimba ikiingia atakuja mwenyewe geto.

ova
 
Back
Top Bottom