Hivi ni kwanini huwa inatokea kumkinai 'crush' wako baada tu ya kumfahamu kwa machache?

Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
7,515
25,163
Hi guys,

Niwatakie maandalizi mema ya kuianza kesho maana baadhi yetu 'we do hate Mondays'..

Back to the topic, Hivi ni kwanini kuna muda unam crush mtu mpaka unatamani hata umuone kila sekunde ila ukishafahamu machache kumuhusu unajikuta zile asilimia ghafla zinashuka mpaka 0°

Nakumbuka miaka flani ya nyuma nikiwa kijana bado, tulikuwa kwa semina moja ya vijana, Wakati semina ikiendelea kuna upande nikatazama daamn'. Nikagongana macho na mkaka mmoja anavutia kutazama jamani, dah' nikajikuta natamani tu kumtazama kila muda,

Hivyo ikawa ni mwendo wa kuviziana kutazamana, kidogo kidogo tukaanza kutabasamu, mpaka semina iliyokuwa inaboa ikaanza kuleta mvuto wa kipekee, kikitokea cha kuchekesha tunatazamana tunacheka ka mazuzu hivii,

Semina ikaisha, tukawa tupo nje tunasalimiana kwa tunaofahamiana tuagane kila mmoja atembee na Bwana, Hivyo nikaanza kumtafuta that crush aliiteka attention yangu pale ndani, ili at least nimtie tena machoni kabla niende, badluck nikawa simuoni, nikaboeka, hivii anaanzaje kuondoka kirahisi namna hii na hata asiage?

Kwenye ule umati wa watu kumbe naye akawa ananisakanya, tukatazamana tena kwa mara nyingine, moyo ukapiga paa'..! finally nikafarijika, akawa anazungumza na wenzie huku anatazama upande niliopo, Kwa makusudi nikajitenga na watu ili anikujie nikashangaa naye ni kama anataka kuja halafu anaona haya, huku namie naitwa na wenzangu tuondoke, hii ndo kipindi pekee wadada tunapendaga 'strong men'.

Nikawa namuangalia naye ananiangalia halafu hakuji, Nikajiuliza sasa nitawaambia nini wenzangu? Eti kuna mtu namsubiri ila anaogopa kunifuata? Haha' nadhani ningechekesha.

Akajikaza mno nadhani, ndo akaja, tukasalimiana hata hatukuongea sana tukabadilishana contacts tukafahamiana majina, kila mmoja akaenda.

Hapo moyoni najiona mshindi, natabasamu kama kachizi fresh. Hakunitafuta mpaka jioni alivyokuja kuniuliza 'ulifka xalma'? Nikasema ooooh' so this is one,
Nikavumilia nikajibu 'ndiyo nashukuru',
Nikaona this will ruin my mood, Enwei, Nikamuaga akanijibu 'uxku mwema pia', nikalala zangu.

Nakuja amka asubuhi nakuta 'umeamkaje mke wangu'? I was like wtf.? Ile ya kwanza nilivumilia nikajua pengine nitamuelekeza lakini the second trash nika prove kabisa this guy hayuko matured kabisa.

Nikamueleza tu kistaarabu, huwa sipendi kuitwa hivyo na mtu ambaye we got nothing, na in fact we got nothing sababu hatukuzungumzia lolote lile kuhusu sisi.. Jamani mtu akaanza kulalamika ooh' nisamehe kama nimekukwaza naona kama nimejipendekeza kwako, sijui nini maneno kibaooo.

Huwezi amini nilimkinai right at the spot, nikampotezea na kum block papo hapo. Vile sipendi mwanaume asiye muelewa halafu mlalamishi kama vile nimemchomolea 'life support machine'.

Huo ukawa mwisho wa kiherehere changu, Na hii ni moja kati ya matukio yangu mengi ya kukinai 'crushie' at the first touchings.

Wacha kwanza nilale kwa Leo, nimechoka kuandika na nisiwachoshe kusoma thread ndefu kama mvua.
 
A mismatch of expectations vs reality.

If you meet someone and ukamuwekea expectations fulani; either because of the way they look, au how you initially interacted, or because you let your mind run wild with daydreams, then you get to really know them and find out they're not what you expected them to be, lazima utakuwa disappointed tu.

Soln: When you meet someone don't put them on a pedastal or put them in a certain category made up in your mind, you'll save yourself alot of headaches and disappointments later on.
 
Sijawahi kinai pombe and pombe it izi mai crush my beloved one my kidney my life



We hukumkinai uliuzika tu na approach yake ukamtoa kichwani ulijenga taswira tofauti lakini ulichokutanacho hukutarajia so ukawa disappointed

And yes sometimes unaweza ukawa una mcrush mtu Fulani lakini ukashindwa kuji express na kila siku huyo let say huyo binti unamuona unafanya kila kitu yaani unajitoa msaada wa hapa na pale at least a feel the same way about you lakini wap haha unajikuta unaitwa best au kaka my fulendi hapo anakuwa amekuweka friend zoned at the end of time una lose interest nae UNAMKINAI unakuwa na ile mentality kwamba siwezi kuwa nae kuliko kuumiza moyo bora nimpotezee ndo mnakuta mwengine anabadili namba kabisa anapotea hataki utamfute maana akiona text yako anaumia moyo



Daah kweli inabidi kuwe na silabasi na mitaala ya kozi fupi kwa madomo zege
 
Mi nadhani,
Kama aliweza kukuvutia mpaka ukatamani kuwa karibu yake, bhasi niamini mimi huyo mtu ana vingi vizuri ambavyo ungekuja kuvifurahia...
Lakin bahati mbaya uliyokutana nayo, ni kwamba ulianza kumfahamu kwenye ubaya wake...

Mimi nadhani, ulikuwa ni wakati mzuri xaxa wewe kum’badilisha na kuwa vile unavyotaka wewe...
 
A mismatch of expectations vs reality.

If you meet someone and ukamuwekea expectations fulani; either because of the way they look, au how you initially interacted, or because you let your mind run wild with daydreams, then you get to really know them and find out they're not what you expected them to be, lazima utakuwa disappointed tu.

Soln: When you meet someone don't put them on a pedastal or put them in a certain category made up in your mind, you'll save yourself alot of headaches and disappointments later on.
thanks much Mr. stritglow nimejifunza hilo pia nadhani, I don't expect too much from anyone right now sababu high expectations real disappoints at it's baddest..!!
 
Back
Top Bottom