Hivi ni kwanini hakuna waziri mkuu aliyekuja kuwa Rais wa Tanzania?

Nipashe

Member
Nov 4, 2007
52
14
Ukiachilia Nyerere, hakuna waziri mkuu mwingine wa Tanzania ambae alifanikiwa kuja kuwa Rais wa nchi, kwa mfano Kawawa, Msuya, Salim, Warioba, Malecela, Sumaye, Sokoine, na kuna kila dalili kwamba at least kwa uchaguzi mkuu ujao 2015, CCM haitamsimamisha mgombea Urais kutokana na Mawaziri wakuu waliopita.

Sababu ya hili ni nini - je ni mpango maalum (kama vile unwritten principle) au huwa inatokea tu?
 
Naweza kusema ndiyo hasa ikizingatiwa kuwa chama chao kimeona hivyo. Kwa kumbukumbu ni kwamba waliwahi kujitokeza akina John Malecela aliyekataliwa baada ya mwalimu Nyerere kusema ni mhuni asiyeweza kuaminiwa madaraka.

Ni bahati mbaya kuwa Malecela hakukanusha. Salim Ahmed Salim alijitupa uwanjani akina Kikwete wakamchafua kiasi cha kuachana na dhamira hiyo. Msuya na Warioba walijaribu na kubwagwa kwenye mchujo. Kwa vile walikuwa wakishindanishwa na wengine, naweza kusema kuwa uwezo wao haukukidhi viwango vya chama chao.
Kwahiyo jibu lako hapa ni kwamba kila wakati wamejitokeza watanzania wengine wenye uwezo kuliko mawaziri wakuu husika?
 
Naweza kusema ndiyo hasa ikizingatiwa kuwa chama chao kimeona hivyo. Kwa kumbukumbu ni kwamba waliwahi kujitokeza akina John Malecela aliyekataliwa baada ya mwalimu Nyerere kusema ni mhuni asiyeweza kuaminiwa madaraka.

Ni bahati mbaya kuwa Malecela hakukanusha. Salim Ahmed Salim alijitupa uwanjani akina Kikwete wakamchafua kiasi cha kuachana na dhamira hiyo. Msuya na Warioba walijaribu na kubwagwa kwenye mchujo. Kwa vile walikuwa wakishindanishwa na wengine, naweza kusema kuwa uwezo wao haukukidhi viwango vya chama chao.
Kwa maneno mengie ni kwamba marais wanaowateua wanachagua watu dhahifu kulinganisha nao! Pengine ni kuwa nafasi ya uwaziri mkuu ni changamoto na mteule anapata shida kuwaridhisha watu kumpa ofisi ya juu. Waziri mkuu anatengeneza maadui wengi kuliko wanasiasa wengine.
 
Sasa si umeshasema nyerere? na 2015 Tukifanya masihara Lowasa atakuwa

Kwa maana hii, historia ya waziri mkuu wa nchi baadae kuja kuwa rais wa nchi inaweza kujirudia kwenda kwenye vitabu vya historia kwamba walikuwa ni watu wawili tu, Nyerere na Lowassa, very interesting. Kwa mujibu wa hoja ya 'father of all' hapo awali,Mawaziri wakuu huwa hawakidhi vigezo vinavyotumika na CCM. Hoja hii ni pana sana kwani haina maana kwamba vigezo hivyo ni formally established bali ni pamoja na vigezo vinavyojengwa kwa misingi ya Fitina.

Haingii akilini kwa Waziri Mkuu kushindwa kupata kura za kutosha katika ushindani na mawaziri wa kawaida. Kwa maana nyingine, kumekuwa na juhudi kubwa wakati wote (kifedha na kifitina) kuhakikisha kwamba waziri mkuu husika hapiti, vinginevyo iwapo ushindani ungekuwa fair & transparent, matokeo yangekuwa ni tofauti. Hapa haina maana kwamba mawaziri wakuu waliopo sasa wanafaa zaidi kuliko wana CCM wengine kuelekea 2015, bali mjadala huu lengo lake ni kuhoji tu kulikoni, na sio zaidi ya hapo.
 
umejichanganya sana hapo, mara unauliza hakuna waziri aliewahi kuwa rais afu mbeleni unatuambia ukiacha nyerere, sasa huyo nyerere hakuwa waziri? jipange na hoja zako.
 
umejichanganya sana hapo, mara unauliza hakuna waziri aliewahi kuwa rais afu mbeleni unatuambia ukiacha nyerere, sasa huyo nyerere hakuwa waziri? jipange na hoja zako.

Iwapo unaelewa siasa za nchi yetu, hoja yake ya msingi bado ipo pale pale; uwaziri mkuu wa Nyerere ulikuwa wa aina tofauti, vinginevyo hata asingemtaja Nyerere, wengi humu wasingejadili kwamba Nyerere alikuwa ni waziri mkuu;
 
wote ni vilaza...wengi wao huteuliwa kwa fadhila na siyo utendaji wao.

Mawaziri wakuu vilaza ni wapi hasa kwani siamini kwamba ni wote. mimi nadhani mbabaishaji alikuwa ni Sumaye na kwa kiasi fulani Kawawa (RIP). Hawa wawili waliteuliwa kwa misingi ya uwezo wao mdogo. Tukirudi kwa Sumaye, kuna hoja kwamba huyu aliwekwa pale na Nyerere ili Mkapa asiwe overshadowed katika muhula wake wa kwanza kwani ilichukua juhudi kubwa sana za Nyerere kuaminisha watanzania kwamba kati ya wagombea wote, Mkapa alikuwa ndio chagua bora kwa watanzania, kwahiyo kuweka waziri mkuu mwenye uwezo mkubwa kunge dismantle hoja na image nzima ya Nyerere katika muktadha huo. Nje ya hawa, sidhani kama tutakuwa sahihi sana kusema kwamba Malecela, Warioba, Msuya, Lowassa walikuwa ni vilaza, na hata Pinda baada ya kumaliza muda wake sidhani kama itakuwa sahihi kusema kwamba alikuwa ni waziri mkuu kilaza. Vinginevyo kama kuna vigezo vya ukilaza ambavyo haujavijadili kwa kina.
 
nafasi ya uwaziri mkuu ni nafasi ya kujiongezea maadui ndani na nje ya chama chako,
maadui wa rais wako ndo maadui yako, ni nafasi ambayo ukimaliza tu mahasimu wapo na wewe...
nakumbuka maneno ya Lowasa, ''.....tatizo ni uwaziri mkuu.....''
hii nafasi kila mtu anaitaka, ukiteuliwa tu chuki zinaanza utajikuta unalia bungeni.
waziri mkuu ambaye angeweza kuwa rais wa nchi hii (Mungu amrehemu) ni Sokoine tu.
 
Mawaziri wakuu vilaza ni wapi hasa kwani siamini kwamba ni wote. mimi nadhani mbabaishaji alikuwa ni Sumaye na kwa kiasi fulani Kawawa (RIP). Hawa wawili waliteuliwa kwa misingi ya uwezo wao mdogo. Tukirudi kwa Sumaye, kuna hoja kwamba huyu aliwekwa pale na Nyerere ili Mkapa asiwe overshadowed katika muhula wake wa kwanza kwani ilichukua juhudi kubwa sana za Nyerere kuaminisha watanzania kwamba kati ya wagombea wote, Mkapa alikuwa ndio chagua bora kwa watanzania, kwahiyo kuweka waziri mkuu mwenye uwezo mkubwa kunge dismantle hoja na image nzima ya Nyerere katika muktadha huo. Nje ya hawa, sidhani kama tutakuwa sahihi sana kusema kwamba Malecela, Warioba, Msuya, Lowassa walikuwa ni vilaza, na hata Pinda baada ya kumaliza muda wake sidhani kama itakuwa sahihi kusema kwamba alikuwa ni waziri mkuu kilaza. Vinginevyo kama kuna vigezo vya ukilaza ambavyo haujavijadili kwa kina.
Kwenye siasa za kwetu ma-rais wataendelea kuteuwa mawaziri wakuu wenye uwezo wa chini ili ma-rais wasiwe overshadowed. Rais akimchagua PM mjanja watagongana watashindwana kama JK na Lowasa, Moi na Ouko, n.k. Pinda amefaa kwa sababu amekubali kuwa zoba, leo anatumwa akaseme hiki anaenda kikileta matokeo mabaya JK anakanusha hakumtuma na Pinda anakaa kimya siku zinaenda. CCM wanalitambua hilo ndio maana inakuwa vigumu kuwapitisha kuwa wagombea wa urais.
 
Back
Top Bottom