Hivi ni kwanini hakuna waziri mkuu aliyekuja kuwa Rais wa Tanzania?

Hata nyerere alitupa ukapuni uwazir mkuu ili awe rais,sasa hawa wengine wanadhan kuandika historia ni rahis
 
Uwaziri mkuu ni nafasi ya kuteuliwa kwa utashi wa mtu mmoja (Rais) kwa kutumia vigezo anavyoona vinafaa kwa fikra zake: ili uchaguliwe kuwa Rais kuna watu engi wanahusika ktk kumpata anayefaa, hivyo vigezo vitakavyotumika vinaweza kuwa vingi zaidi (kutokana na idadi ya wapiga kura) ya vilivyotumika kumfanya mtu awe waziri mkuu. Hivyo hii inaweza kuwa sababu mojawapo ya kuwa mawaziri wakuu si mara zote hukidhi haja za watu wengi kimtazamo kuwawezesha kushika wadhifa wa uras!
 
......Nadhani lazima ujiuzulu uwaziri mkuu ndipo utakapopata nafasi ya uraisi.......kama ilivyokuwa kwa nyerere.......
 
Kwani umeambiwa tanzania imekufa? Hivi cha ajabu ni nini? Taifa changa lililopata kuwa na marais wa nne tu mnalitengenezea vi -theory vya ki hisiahisia!. Bado kuna uchaguz 2015, wahamasishe mawaziri wakuu wastaafu wagombee, ni wao kujua kanuni za mchezo na kuwekeza kwenye ugombea ndiyo siri ya ushindi
 
Ukiachilia Nyerere, hakuna waziri mkuu mwingine wa Tanzania ambae alifanikiwa kuja kuwa Rais wa nchi, kwa mfano Kawawa, Msuya, Salim, Warioba, Malecela, Sumaye, Sokoine, na kuna kila dalili kwamba at least kwa uchaguzi mkuu ujao 2015, CCM haitamsimamisha mgombea Urais kutokana na Mawaziri wakuu waliopita.

Sababu ya hili ni nini - je ni mpango maalum (kama vile unwritten principle) au huwa inatokea tu?

Waziri mkuu ni preference ya Rais. Urais ni tofauti. Urais unahusisha wadau wengi na mchakato wake ni mrefu kidogo. Kuna migongano ya fikra na preference baina ya wadau waliopo kwenye mchakato wa kupendekeza jina la rais katika chama.

 
Sasa si umeshasema nyerere? na 2015 Tukifanya masihara Lowasa atakuwa

Jibu rahisi ni kwamba, waziri mkuu huchaguliwa na mtu mmoja (rais) na wengi huchagua yule anedhani anafanana nae kimtazamo, wakati rais wa nchi huchaguliwa na watu wengi(wnanchi) na wnanch wanapenda mabadiliko kwani uzoefu unaonyesha kila rais ansetoka madarakani huwa na mapungufu mengi hivyo kuhitaji mtu mpya wa kusahihisha na sio kuleta sura inayofanana kiutendaji na raisi aliyekuwepo madarakani.

Kwa mfao, huyo Lowassa unayemsema hawezi kuwa chaguo la wengi kutokana na kashfa zinazomkabili alipokuwa Waziri Mkuu wa Jk.
 
Watu ambao ni potential wa kuwa Rais Tanzania (toka kwa chama tawala) ni pamoja na mawaziri, mawaziri wakuu, makamu wa rais na rais wa Zanzibar. Ukiondoa JKN, Tanzania imeshakuwa na rais Mwinyi aliyetokea kwenye urais wa Zaanzibar na wengine wawili tu waliotokea kwenye uwaziri!

Sio sawa kusema kwamba historia inawatenga mawaziri wakuu kwenye mbio za urais, ilhali tunazungumzia rais watatu pekee! Mbona hatusemi kuhusu makamu wa rais?
 
Back
Top Bottom