Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,141
"Hivi ni kwanini bando zina expire? Simu ni ya kwangu, nimenunua bando kwa fedha yangu halafu unanilazimisha nitumie kwa muda unaotaka wewe, hii ni kwanini Mh Spika? Kama ni sheria, basi iletwe sheria hapa ibadilishwe, kwasababu tunaibia wananchi.
"Anatafuta fedha kwa jasho, ananunua simu, anataka awasiliane, ananunua bando anataka limsaidie anaambiwa ndani ya siku 7 linatakiwa liwe limeisha! Hivi hii ni sheria ya nchi gani?
"Kama ni sheri basi tunaomba ije hapa, kwanini unipangie kutumia bando langu? Mimi si ndio najua umuhimu wa mawasiliano na ndio maana nikanunua bando la wiki moja? Kama nimeamua kulitumia taratibu wiki moja imeisha nimeweka akiba kwanini wewe ulikate?
"Mh. Spika nakuomba sana kwa hili uwe mkali utuongoze hili jambo la kuibia wananchi lifikie mwisho."