Hivi ni harali nyimbo za dini kupigwa baa?

Hivi ni harali nyimbo za dini kupigwa baa?

Bzimana

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2013
Posts
554
Reaction score
162
nyimbo za dini siku hizi ndizo zinazotumika kuwaburudisha walevi/wanywaji wa pombe vilabuni, hasa zile bar za mafichoni..
Nakalibisha hoja.
 
Hivi moja ya kazi za Dini sio kuwaokoa so called wakosaji ? Kama ndivyo basi Bar, Vilabuni na kule kote ambako kuna uwezekano wa watu kupotea hizi nyimbo ndio mahali pake kuliko hata kwenye sehemu za Ibada.

By the way nyimbo zinakidhi mambo mengi, burudani ikiwa mojawapo
 
Za rose muhando na bonny mwaitege zinaruhusiwa kupigwa bar yeyote ile.
 
Mkuu hamna ubaya kama. Yesu alikuja kwajili ya wenye dhambi km wewe ni mhislam utaelewa chochote hapo
 
Najiuliza, hivi mfano ukapigwa wimbo wa kukosoa ulevi, walevi watakubali kweli???
 
""Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu, wenye afya hawakuhitaji daktari, wanaohitaji ni walio wagonjwa"""
 
Ukiona hivyo inawezekana ikawa vitu vyote ni haramu...Nyimbo, pombe na io Dini ambayo weyenyewe wameruhusu nyimbo zao zipigwe baa..... Akili haikubali mambo ya ibada yafanyike kwenye vilevi....kwa sababu mlevi akishalewa sote tunawajua....mikojo,matapishi...wengine mpaka kinyesi......
 
Ukiona hivyo inawezekana ikawa vitu vyote ni haramu...Nyimbo, pombe na io Dini yenyewe ilioruhusu nyimbo zao zipigwe baa..... Akili haikubali mambo ya ibada yafanyike kwenye vilevi....

wewe wasema na labda sio mkristo ndio.maana hujui maana sahihi ya kuokolewa kiimani
 
inaonyesha mtoa mada hujaelewa suali lake....ni hili hapa.

"nyimbo za dini siku hizi ndizo zinazotumika kuwaburudisha walevi/wanywaji wa pombe vilabuni, hasa zile bar za mafichoni..
Nakalibisha hoja"....nyimbo mkuu hapa zinatumika kuwatumbuiza walevi na sio kuwaokoa kiimani.....
 
Mkuu kibusara ukitaka kumuokoa mtu kwenye kutendsa dhambi....ni bora umwendee akiwa na akili timamu.....au wewe ni mpigaji wa Kitaa kwa ajili ya mbuzi?
 
Mkuu kibusara ukitaka kumuokoa mtu kwenye kutendsa dhambi....ni bora umwendee akiwa na akili timamu.....au wewe ni mpigaji wa Kitaa kwa ajili ya mbuzi?

mkuu mimi binafsi nakunywa pombe siwezi ficha hilo, niulize swali kwa mtindo huu, hivi hujawahi sikia kuwa sehemu zenye mabaa kuna madili sana ya pesa, si wote wakiwa kwenye influence ya pombe hawana busara kuna wengine wanasikia na wanayafanyia kazi yale waliyoyasikia ndio maana nikatolea mfano wa madili wanayopeana watu wanapokunywa huwa wanayafanya baada ya hapo
 
Huko na hizo nyimbo zinatakiwa kupigwa 24/7. Hao ndo wanazihitaji zaidi ingawa si kwamba walevi ni wenye dhambi.
 
Kwa vile umeniambia wewe ni mnywaji wa pombe...mimi nakaa nje ya mada mkuu... kwa sababu najua pombe hukingia kwa utamu na vizuri wa hali ya juu ukiwa unasikiliza nyimbo za kanisani....kila la kheri mkuu
 
Back
Top Bottom