Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
Mtu yeyote akitaja neno Dowans basi waliopo karibu watakunja nyuso zao na kusema kila aina ya ubaya kwa kampuni ya dowans. Nafahamu kuwa mchakato wake haukuwa wa wazi lakini swali je hayo makampuni mengine ya kufua umeme kama IPTL, SONGAS na mengineyo yalifuata taratibu zote za kisheria bila kuhusisha ruswa kwenye mikataba yao na Tanesco? Ikiwa hivyo basi tuna haki ya kuisakama Dowans na wale wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine na Dowans. Lakini ikiwa makampuni mengine yaliyosalia ukiitowa Dowans pia na yenyewe yamejaa usanii na mikataba yake haikuwa na tija na iliingiwa kwa hila basi sisi "Watanzania" ni wanafiki! Wanafiki na tuna sababu za nyuma ya pazia kuisakama Dowans!
Kuna habari nimepata kuzisikia kuwa Dowans ndio kampuni pekee inayochaji "capacity charges" kuliko makampuni mengine Dowans wanalipwa 152 mil per day, Songas over 250 mil per day na IPTL kwenye 300 mil per day.
Nadhani imefika wakati tujaribu kutafuta ukweli na kuyachambua makampuni yote yanayofua umeme tusiwe waitikia kiitikio "kolasi" na pili tuache unafiki kama kuna makampuni zaidi ya moja yanayohusika na hila basi yakemewe yote kwa nguvu zote yasishambuliwe makampuni baadhi kwa sababu ya hila na chuki binafsi huku mengine yakiendelea kutunyonya.
Kabla ya kuwakilisha na kukaribisha hoja napenda kukoselewa na kuelimishwa hayo ni maoni yangu binafsi na figures nilizotoa ni just round figures sina source ikiwa kuna mtu ana source itakuwa kafanya jambo la maana akituletea source ya charges zinazolipwa na Tanesco kwa makampuni husika.
Nawakilisha.....