Hivi ni akili au matope! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni akili au matope!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WALIMWEUSI, Jan 11, 2012.

 1. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Inakuwaje wewe kijana wa kiume unaishi kwa kakayako, naye ana mke. Wewe uko pale kwa vile umeshindwa shule, sasa unafanya kuungaunga walau upate pa kujishikiza. Kaka yako na mtoto mdogo, akaamua atafute house girl wa kumsaidia mkewe hasa awapo kazini. House girl ni mchapa kazi sana na anamheshimu kakao na mkewe. Wewe kijana wa kiume ambaye umeonewa huruma na kakako, na kuchukua zigo la kukusomesha unaanzisha mahusiano ya kimapenzi ndani ya nyumba ya kakako na house girl.

  Kwa vile huwa unaenda shule, wamdanganya mtoto wa watu kuwa unasoma chuo kikuu kumbe unareseat mitihani ya form foru. Halafu kibaya zaidi mnafanya mapenzi humo humo ndani kwa kaka yako, usiku wakati wao wamelala. Kibaya zaidi unamshauri huyo demu aondoke coz hujisikii vizuri kumuona akiwa house girl (mbaya zaidi ze comedy wanapowaitaga ma beki tatu).

  House girl anataka kuondoka ghafla tu na hali shemeji yako yupo kazini na hategemei kupata likizo. Jamani, hivi ndugu zetu nyie tuache kuwasaidia?Huko mnakosoma na kuzurura hamkuwaona wadada tena warembo kuliko housegirls?Ni adabu kweli kugeuza nyumba ya kaka yako guest house, sometimes mchana wapo kazini nyie mnafanya starehe zenu?

  Kwa wale wote wenye tabia hii nawaomba muache.:hatari:
   
 2. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Kwanini usimwambie muhusika???
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Niutoto tuu wakikia wataacha tabia hiyo wala usijali....
   
 4. Darlingtone

  Darlingtone JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa unafuga ugonjwa... Timua huyo mfitini arudi kwa mama yake akafanyie ushenzi huko
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Fukuzia mbali huyo ni mwanaharamu!
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Hivi unapoandika muda huu bado unaendelea kumlisha tu?
  Aondoke, kama ni ada umtumie kwa Mpesa!
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Watoto hua hawajui kuvuana makabati !
   
 8. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #8
  Jan 11, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kusema kweli sijaona kundondokeana kimapenzi inaingiliana vipi na mmoja wao kua house gal na mwingine kua mzigoa kwa kakake (as you call it) Hebu iangalie kwa upande huu....

  House gal ni binti mzuri na mastaarabu na katulia, na ni binti ambae kama mabinti wengine once in a while fall in Love... Anachapa kazi, ana adabu (as per your say); Huyo kijana anakosa gani kumpenda huyo binti? Kwamba sababu ni binti wa kazi hana feelings za mapenzi ama hastahili kupendwa?

  Haya basi yaelekea kijana kweli kampenda binti kwa dhati.... Na twaelewa kua a true man always wants what is best for her lady... Wee mwenyewe hapo wasema mahouse gal wanajina lingine (obviously intended at mocking) la beck tatu.... Je kuna mwanaume ambae anampenda kweli mwanamke wake atataka awe house gal?

  IMO makosa ambayo naona anayo kijana ni haraka yake.... Kama kweli awategemea kaka na shemejie na ndio anarudia form four; yupo faster saana... Anamshauri huyo binti aondoke aende wapi na atamsaidia vipi? Hata hivo huo ni mtazamo wangu tu....
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Kwanza huyo fomu foo na hausi gelo hawawezi soma jf, ujumbe hauwafikii.

  Afu huyo mdogo mtu hadi kufikia point hiyo mmemdekeza wenyewe.
  Ningekuwa mie, angeshaisoma namba siku nyiiiingi.
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuwabeba ndugu ni kitu kizuri ila mara nyingine ni mzigo mzito kupitiliza!
  Unaweza kuishia selo bureeeeeeeee
  !!Najaribu kupata picha, huyo mshenzi angekuwa kwangu,
  ningemuachia Mungu na daktari wamuokoe.
   
 11. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  housegirl nae anahitaji kupashwa kidogo mwili wake, jamani nae ni mwanamke kama nyinyi, anatamani ile kitu kama nyinyi msimuonee eti katembea na mdogo wa bosi wake
   
 12. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2012
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo bold tuko pamoja sana.Na kama hali ni hii wote HG na kijana ni wajinga wasio na mfano.Ni kama vipofu wawili wanaelekezana njia.Hapo hakuna mwenye mwelekeo wa maisha wa kumsaidia mwingine bali wametawaliwa na tamaa za mwili tu hakuna lolote.
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  wakati anamwambia aondoke asiondoke hivi hivi bila mimba,atlsist kijana abebeshwe mzigo wa kuoa.
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu well said lakini anapokosea huyu mdogo mtu anaesaidiwa ni kumshauri aondoke wakati hawezi kumfanyia msaada wowote. So wenye tabia za ushauri negative kama huu ni vyema wabadilike. Also True love siku zote zinakwenda na kuwa mkweli so ni bora mdogo mtu hapa awa mwazi ili nae mwenzake akajua jins ya kujiandaa na kujipanga kama wana mpango wa kujaishi pamoja
   
 15. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nadhani umeeleza vizuri, ingawa nia yangu sio kuunga mkono uhusiano wa namna hiyo. Wao kama binadamu pia wanaweza kupendana, upendo kama mjuavyo huwa unawafanya watu wawe vipofu, ndio maana unaona wanafanyana humo ndani ya nyumba, halafu hata hivyo unategemea waende wapi?, Guest? Hawawezi kumudu. Siungi mkono mapenzi yasiyo ya ndoa, lakini ninachotaka kusema ni kwamba mtoa mada ulitakiwa ukae nao uzungumze, uwaelimishe na kuwaonya kwa upendo kuhusu hizo tabia na madhara yake. Kwa rika lao hilo ni mambo ambayo unaweza kutarajia.
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hata kama hawezi ingia humu Jf ila inawezakutumika kama fundisho kwa walio humu Jf
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  suala kama hili ni vyema kutumia busara zaidi ili ufanye umuzi ambao mtu hutokuja jutia
   
 18. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  hahahaha PJ
  atume kwa airtel money or tigo pesa
  watu wengine wapenda kufundisha wenzao kutenda mabaya
   
 19. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,363
  Likes Received: 1,188
  Trophy Points: 280
  respect nitonye!!!! kwanza ukimkawiza beki tatu anaweza akampa mpemba wa gengeni..then hata bro akakuona waubaridi!!!
   
 20. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2012
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  dada asha tuko pamoja ila ambako sijapendezewa ni kijana kumwambia binti aondoke,sababu naona kama kuna uwezekano wa kijana kumyumbisha huyu binti sbb kijana angekua na kazi ya kumwezesha kwenda kumpangishia binti mahala ili asiwe housegirl hapo ningemuelewa lkn kijana mwenyewe kula yake ya kusaidiwa,pili sijafurahi kumwambia binti aondoke ilhali kijana anajua fika kwamba binti ndiye msaada mkubwa hapo home na akiondoka shemeji yake atapata shida ukichukulia siku hiz ni shida kuwapata hawa mabinti.Tatu kwa nin hapend kuona binti akiwa hapo kama housegirl wkt uhousegirl si kosa la jinai wala dhambi kwa kauli hiyo inaonesha kijana anamdharau binti kwa kuona uhousegirl ni kitu cha aibu.Yeye kijana na huyo binti kupendana ndani ya nyumba ya kaka wa kijana sion tatizo juu ya hiyo,hata kama kijana bado analelewa bado ana haki ya kupenda ila tu anapodanganya yuko chuo kikuu ilhal anareseat form four na anavyomwambia binti aondoke inanitia mashaka kuwa anataka binti aondoke labda kisha amtose maana labda kijana anaona binti akiendelea kuishi hapo anaweza siku moja kugundua kuwa si kweli kuwa anasom chuo kikuu.
   
Loading...