Hivi ndivyo Watanzania wanavyoteswa na waajiri wao

olevaroya

JF-Expert Member
May 6, 2012
1,224
512
1. VYETI VYA NIT (MAFUNZO YA KUPATA LESENI MPYA)


Tunasikitika sana kwa sababu tulitakiwa na Serikali kubadilisha leseni jambo ambalo tuliliona ni jema na la busara kuingia katika tecknolojia ya kisasa ya digitali. Sisi kwa sababu ni wengi hapa leopard na kwa pia kampuni hii ya leopard ni kubwa na ina wageni wengi sana haikuwa rahisi kuhudhuria mafunzo ya NIT kwa pamoja wote ila Tajiri wetu alituandalia Darasa la hapa hapa Leopard ambalo lilifanyika katika garage ya Leopard tours njiro, tulifurahia sana tukadhani tajiri wetu anatujali sana kumbe ilikuwa ni tofauti na mawazo yetu, alichokifanya alitulipia gharama za kusoma darasa la NIT ambalo kila mtu alimlipia kiasi cha laki mbili ( 200,000), na kilicho fuata ni kila mwisho wa mwezi tulikuta tunakatwa fedha kidogo kidogo mpaka hilo deni likaisha jambo ambao lilikuwa sio baya hata kidogo,


Cha kushangaza vyeti vyetu vilivyo toka NIT tulitegemea tungepewa ila haikuwa hivyo aliwadanganya watu wa NIT kuwa wamletee yeye ya kuwa atatupatia hivyo vyeti, na kusema ukweli hajawahi kutupatia amevishikilia mpaka sasa hivyo na ni zaidi ya mwaka mmoja sasa !!!! sasa kama alikuwa anavihitaji kwa nini basi asingetulipia na kuacha kutukata kwenye mshahara wetu ili tusiwe na haki ya kudai? Au labda NIT watuambie sheria yao inasemaje ya kuwa mtu akishamaliza chuo chao vyeti wanampa nani? Mwajiri au mhusika?
 
1. VYETI VYA NIT (MAFUNZO YA KUPATA LESENI MPYA)


Tunasikitika sana kwa sababu tulitakiwa na Serikali kubadilisha leseni jambo ambalo tuliliona ni jema na la busara kuingia katika tecknolojia ya kisasa ya digitali. Sisi kwa sababu ni wengi hapa leopard na kwa pia kampuni hii ya leopard ni kubwa na ina wageni wengi sana haikuwa rahisi kuhudhuria mafunzo ya NIT kwa pamoja wote ila Tajiri wetu alituandalia Darasa la hapa hapa Leopard ambalo lilifanyika katika garage ya Leopard tours njiro, tulifurahia sana tukadhani tajiri wetu anatujali sana kumbe ilikuwa ni tofauti na mawazo yetu, alichokifanya alitulipia gharama za kusoma darasa la NIT ambalo kila mtu alimlipia kiasi cha laki mbili ( 200,000), na kilicho fuata ni kila mwisho wa mwezi tulikuta tunakatwa fedha kidogo kidogo mpaka hilo deni likaisha jambo ambao lilikuwa sio baya hata kidogo,


Cha kushangaza vyeti vyetu vilivyo toka NIT tulitegemea tungepewa ila haikuwa hivyo aliwadanganya watu wa NIT kuwa wamletee yeye ya kuwa atatupatia hivyo vyeti, na kusema ukweli hajawahi kutupatia amevishikilia mpaka sasa hivyo na ni zaidi ya mwaka mmoja sasa !!!! sasa kama alikuwa anavihitaji kwa nini basi asingetulipia na kuacha kutukata kwenye mshahara wetu ili tusiwe na haki ya kudai? Au labda NIT watuambie sheria yao inasemaje ya kuwa mtu akishamaliza chuo chao vyeti wanampa nani? Mwajiri au mhusika?


Au labda wanatanzania wenzetu mtusaidie labda tunakosea kudai hivi vyeti kwa mwajiri wetu maana amesema hatoi tuende kokote tunakotaka na sisi kusema ukweli hatuna pa kushitaki maana huyu jamaa anayo nguvu ya ukweli wala akisema kitu atanii ni noma maana ukimsumbua anaweza kukupoteza kama anavyo semaga kila wakati kuwa serikali hii iko mkononi mwake,,,, mhhh jamani tusaidieni watu wa NIT najua mtaisoma hii habari please tuna omba mfuatilie hata kama mtataka kuja hapa leopard tours arusha tuko tayari kuchangia nauli yenu maana tunajua kuwa haya malalamishi yetu ni ya kweli na si vinginevyo.


VYETI VYA NIT NI MALI YETU SISI MAGUIDE WA LEOPARD MAANA ULITUKATA HIYO HELA SASA IWEJE LEO HII UTAKI KUTUPATIA ??? au ndo njia ya kutubana tusiache kazi ?????? tunaomba tu utupatie maana kweli maana sasa nadhani imefika wakati labda tuombe waandishi wa habari waje tuwe na maongezi wewe na sisi maguide na watu wa NIT tuone kama kweli nani ni muongo?





2. KUHUSU MASHINE YA KUSCAN WATU ( SECURITY SCANNING MACHINE).


Tulilalamika katika Habari ya mwanzo tuliyo itoa hapa katika JF tunashukuru watanzania wenzetu wenye huruma na wenzio wanaoonewa. Kusema kweli imeleta angalau katofauti kidogo ingawaje kabla yah ii habari kuruka hewani kuna wenzetu wamefukuzwa kazi na bossi wetu kwa sababu ya kutokupita kwenye hii mashine na kusema kweli tuliambiwa asiyetaka kupita aache kazi mlango ni mweupe(naukiangalia huna nssf wala nini halafu kuacha kazi Mhhh) …….. sasa hawa wenzetu kusema kweli kazi imeisha na la kufurahisha kama sio kusikitisha hawana chao ambacho wanaweza kudai kama mafao, maana hata ukienda Nssf unaambiwa hamna kitu kusema kweli inauma kuzungumzia hili jambo tunaomba kama kuna watu wanaousika wangetutembelea hapa leopard waone kama haya malalamishi ni ya kweli au ni uzushi.


Sasa sisi kama waongoza utalii hapa leopard tunasikitisha kuona kuwa Tajiri yetu badala ya kuangalia na kuona kuwa haya malalamishi yetu yakoje ili aweze kutusaidia Yeye alichokifanya ni kuita watu wa Atomic (akishirikiana na hawa maguide wanyarwanda) ili waje wahakikishe ni salama au la !!!? sasa sisi tunahoji kama kweli unayo pesa na umefanya jambo ambalo sio sawa katika jamii je utashindwa kutumia nguvu zako za pesa na kubadilisha ukweli????? Tusaidieni jamani kabla hatujashikwa na kansa watanzania wenzetu.


Sisi hatuamini kuwa kuna haki inaweza kupatikana maana ameshakusudia hiyo mashine iwepo hapo garage na kwa sababu yeye hapiti ni sisi wabongo ndo tuna pita pia kulingana na ukweli kwamba jamii ya watu wa kihindi wanatuchukuliaga kama nyani sidhani kama inaweza kuwauma kuona kama sisi wabongo tunakufa Mhhh? Sijui labda watanzania wenzetu mtusaidie kwenye hili .. Kitu kingine cha kusikitisha alicho kifanya amewaita wenzetu Fulani( wanyarwanda) tunaofanya nao kazi kama maguide, ambapo mhusika mkuu ni huyu anayeitwa kitanga yeye hatukatai anaongea kifaransa kizuri sana kwa sababu ni mnyarwanda amezaliwa huko na kakulia huko pia inakuwaje wewe Kitanga umpigie simu bosi umuambie utamletea watu wa atomic waipime hii mashine ????? kama sio unatetea ugali?


wewe na sisi kumbuka wote ni maguide na wote tunatakiwa tupite hata kama ugonjwa unakuja hautachagua mnyarwanda au mtanzania kumbuka sana hilo kaka yetu,,kitanga,, tunajua umeshazoea vita na misukosuko ila sisi hatujazoea please hili suala ni la management ungeacha waangaike wenyewe kwa sababu huyu ni mhindi siku zikimtimka utarudishwa kwenu kama mahindi siunajua ana nguvu katika kila ngazi za serikali?!!!? Na ndo maana umewezza kufanya kazi mpaka sasa billa mtu yeyote wa migration kukusumbua sasa unajisahau tunaona kumbuka OPERATION KIMBUNGA inakuja arusha sasa sijui boss atakusaidia kuhonga sikuzoe au la?


Ila kwa muonekano wa kawaida hatushangai maana unalipwa ghali sana kitanga na sisi tunashangaa iweje ulipwe kiasi hicho wakati unaongea lugha moja tu kifaransa????? Na wakati kuna watu wanaongea lugha nne na wanalipwa hela ya mboga tu ??? usawa uko wapi?? Labda ndo maana umeamua kuitetea hii mashine ili tajiri akuongezee mshahara ?? tungekuona wa maana kama kweli unatupenda sisi wafanyakazi wenzio kwa kumshawishi tajiri yetu aongeze mshahara na allowance ili angalau tuwe wote uniform, ila sasa wewe ndo kabisa unatafuta kuvutia kwako jamani muogope hata Mungu,kwani nani alikuchagua wewe kitanga kuwa msemaji wetu ???


basi hata kama unajipendekeza basi ungekuwa hata unatutetea kidogo jamani wenzio… badala yake ukiitwaga na boss tu wewe una kuwa upande wake hauna unachokiongea kazi kujisifia tu kuwa umeongea na boss hii sisi itatusaidia nini?? .


Ila hatuoni ajabu maana kitanga kama hiyo pesa yote unayolipwa dola 1000. Kwa mwezi kwa kweli na bado unalipiwa nyumba na watoto wako wanasomeshwa na kampuni sisi hatuoni cha kutushangaza kama ukiwa upande wa tajiri maana uko juu sana kimapato, na pia hata kama ikitokea ume taka mkopo unapewaga bila masharti yoyote ushaidi upo, sasa hayo yote unafanyiwa kweli wewe unaweza kuwa na uchungu wowote kwa sisi wafanyakazi wenzako watanzania? Uzuri sisi tulilelewa vizuri na Mwalimu Nyerere tupendane, Na ndo maana hatujawahi kukuripoti kwa operesheni kimbunga, ila wanakuja tumeshawapa taarifa zenu,


Labda watanzania tuwape picha halisi ya hapa garage palivyo; kuna geti la kwanza ambalo ukirudisha gari la safari unaingia na kukaguliwa kama kila kitu kiko sawa na pia unaongeza na mafuta kab isaaa kabla haujapaki gari tayari kwa safari, so ukishakaguliwa unaingia geti la pili ambalo limewekewa mashine hii balaa ya kutuscan na kutumaliza, ukishapita hili geti la pili unaingia parking. Kisha unatoka nje kwa kupitia kwenye hii mashine, hivyi ndivyo palivyo hapa kwetu. Sisi tuliomba kuwa kutokana na hali ilivyo kwa nini tusiache magari hapa baada ya kuingia geti la kwanza ? na Boss yeye ateue mhindi yeyote anaye mwamini sana aingize hayo magari geti la pili ili sisi tusiingie tubakie geti la nje ili tuwe salamaa??? Pili kutokana na kuwa tayari kuna mafundi ambao wao ni wanyonge hawawezi kulalamika popote na pia ingawaje sio wengi kama tulivyo sisi maguide ambao tunakaribia 250, na mafundi wao wanakaribia 30, sasa kwanini sisi tusingeishia hapo nje ili angalau kama ni magonjwa wapate wachache ( mafundi) tu kuliko kuangamiza watu wote?? Tunaomba kama kuna mtu anayeweza kutusaidia tuepukane na hii kero please atusaidie, pia kama inawezekana kuwaokoa na mafundi ambao ni wanyonge siku zotebasi atusaidie ila kama haiwezekani basi hata okoa hao 250 kuliko kuacha madereva 250 na mafundi 30 kuangamia. Asanteni sana watanzania kwa kulitazama hili kwa undani, maana wenzetu tayari wameshapoteza ajira kwenye hili, na pia bado wengine wanasubiria .


Kwa kweli tumechoka kunyanyaswa hapa leopard tours ltd, Maana ukiangalia Allowance haitoshi, sasa jamani kama mnatulipa elfu ishirini kwa siku (20,000), haya tunaenda safarini na kulala katika hoteli malazi ni 15,000. Kwa siku Sasa mfukoni tunabaki na shs 5000, Sasa tunaomba tutofautishiwe kati ya Safari imprest na Safari allowances


tutafurahia sana kama utaweza kututofautishia kati ya safari imprest na safari allowances maana inaweza kutusaidia hata kurejesha zile ndoa zilizo vunjika, maana imekuwa kama hiyo elfu ishirini (20000) unayotupatia kama safari imprest na ndo hiyo hiyo safari imprest na ndo hiyohiyo ya kuoshea magari jamani hii ni sawa? tunachojua sisi ni kuwa mtu unaposafiri unapewa safari imprest ili kama gari inaharibika au kuna emergence yoyote uweze kutumia na mwisho wa siku urejeshe risiti, sasa Fazal wewe unatuna hii elfu ishirini tangia miaka mitano iliyopita mpaka sasa kweli?/?
Unajua mara nyingi tunapokuwa na wageni wanatuambiaga kuwa wameshatulipia guiding allowance dola 100 kwa siku , sasa inakuwaje wewe unatulipa elfu ishirini hiyo hela yetu nyingine unapeleka wapi? au ndo unatumia kujengea maghorofa kila kukicha.,?


tunaomba sana mara moja , uache mara moja na uturekebishie hayo mahitaji yetu.na pia utulipe hiyo guiding fees ambayo ni kama kaisi cha kati ya 100 na 50.Dola za kimarekani. umeturusha sana kwa siku nyingi ila sasa imefikia kuwa mwisho tunaomba pesa zetu.uwezi kutulipa elfu ishirini kisha ndo iwe ndo
, na hapo hapo hatupewi guiding fee, wala tax money, wala overtime tunafanyishwa kazi kama mapunda tuna mnufaisha mtu mmoja tu, sasa sisi tunahoji iweje kampuni iweze kufunga magari yote 250 car tracking system ambapo ametumia mamilioni ya pesa?? Sasa kwa nini hata asingewekeza hiyo hela kwenye mishahara yetu si tungekuwa mbali jamani?


Akaona haitoshi ameamua kununua scanner mashine kwa bei ya ajabu na pia akaamua kununua security camera za hapo garage kote amefunga hata ukienda kujisaidia chooni kuna kamera sasa kwa nini usingeacha hatta basi moja kati haya na angeyasitisha ili angalau atuboresheemshahara, na pia kuwaambia wageni kuwa kutoa tip ni lazima kwa kila kichwa.


Tumeamini kwa sababu amefanikiwa kuwaita hawa jamaa wa Atomic kuhusiana na hii mashine na wao tunaamini wamepokea chochote maana ukiongea na bosi anakupa namba ya watu wake wa Atomic wanakuambia kuwa piteni tu haina shida. LAITI KUNGEKUWA NA UWEZEKANO KISHERIA AMBAO UKO JUU YA PESA ILI ITUSAIDIE. jambo ambalo tunaliona kuwa ni ngumu sana maana ni nani asiyependa pesa? ndo maana unaweza kumtukana hata waziri kisha unampooza na pesa naye anakubaliana . KWA KWELI FAZAL UNAYO PESA.


maana mpaka sasa watu waliofukuzwa kwa ajili ya kutokupita katika hii mashine idadi imeongezeka, na unafukuzwa kama mbuzi bila hata chochote,!!


3. UPANGAJI WA KAZI


Kwa kweli kusema ule ukweli tumeamua kulalamikia hili kama katika jamii kuna mtu anayeweza kudiriki kukutana na huyu tajiri yetu aweze kumpa hata ushauri jinsi ya upangaji wa kazi ili kuzuia mianya ya rushwa na pia tunaamini inawezekana tajiri yetu hajui kama kuna mambo kama haya yanayo endelea na pia kama kuna mtu wa KUZUIA RUSHWA atakaye soma hili atupe mbinu ili tujue tufanye ili tukomeshe rushwa hapa leopard tours maana imekithiri.


Mwanzoni ilikuwa ni sawa unakuta wanatoa chati ya wiki nzima unakuta mtu una pata kujua kama unasafiri lini na uko na wageni wangapi pia na jirani yako anawageni wangapi jambo ambalo lilikuwa angalau bora kwa maana kama mtu mmoja amebeba wageni sita safari hii na akabeba safari ifuatayo sita na hapo hapo kuna mwingine amebeba wawili safari tatu mfululizo basi inakuwa rahisi kuhoji kulikoni kwa sababu mnaona chati nzima, ila hapa kwetu leopard tours kuna ukiritimba kwenye hii meza ya Mr Kamal ( transport manager) anatoa chati ya siku mbili ??


maana yake nini kama sio kufunika uchafu anaoufanya????? Tunayasema haya tukiwa na ushaidi kamili kabisa ingawaje kwenye hili inawezekana mwenye kampuni halijui (Mr Fazal). Ndo maana tumeamua kulianika ili kama kweli alijui ajue ili alifanyie kazi, maanake hakuna usawa hapa kwetu leopard, maana hapa kwa kawa ida kuna watu wa kazi Fulani wao mwaka hadi mwaka wanabeba kati ya watu 5 hadi 6 ndani ya gari kila safari ukiuliza unaambiwa ni request, sasa ina maana kama hawa watu wakifa mfano nani atabeba???? Tunayo mifano kamili hata kwa majina mfano kama vile Samwel hayuma ( fundi) jamani fuatilieni kazi anazozibeba muone, wako wengi sana tuna yo majina yao ikitakiwa tuyataje na kazi waliyo beba na tarehe tunazo hatubahatishi,


kusema kweli kama kuna mtu anayejua ofisi ya leopard tours iliko aje hapo nje upande wa pili kuna muuza kibanda huyo ndo agent wao mkuu kamal na mwenzake pesa zinaletwa na kuachwa hapo please fuatilieni muone kama ni uongo. Tungeomba kama Mr Fazal halijui hili basi afuatilie kweli na pia kama inawezekana atuite wote, tuongee aaangalie wote ambao wamekuwa wakibeba wageni wawili tu kasha awaite alafu asikie kutoka kwao maana tunauchungu na hatutamfungia mtu macho tutasema kweli kweli tupu. Pia tunaomba kama bosi wetu ataamua kutuita basi atupe ruhusa ya kuongea maana kwa kawaida pakiwaga na mkutano wowote na bosi huwezi kuongea ni yeye tu maana atakuja na kuanza kutoa sera zake kasha matusi anaweza kuamua kumtukana mtu yeyote na sanasana tusi lake kuu ni ass hole.jamani hii ni sawa?????. Anyway ana pesa na ni bosi basi tumuache tu.

















Download entire message
 
Fupisha maneno unataka serikali tukupenini

Maana inaonyesha wewe nimlalamishi sana
 
Poleni sana Watanzania wenzangu iko siku mtasahau mateso yote maana mkoloni mweusi siku zake ni chache 2015 pepo Ccm tunakwenda kumtoa ameshindwa kutuongoza.
 
Unaweza kuta ww mwenyewe una ajira
una au huna, namshukuru Mungu taaluma yangu inaniwezesha kufanya kazi popote, nimemshauri atafute sehemu nyingine sababu hapo hata ufanisi hautakuwepo na kuendelea kulalamika hakumsaidii hakuna atakaemsikiliza, wenye mamlaka ya kumsaidia wako busy wanakula hawataki usumbufu
 
huyo mhindi wenu ana kiburi sana na dharau. Niliwahi kuongea na wafanyakazi wa Leopard wakaniambia anaweza kumpiga kibao mfanyakazi wake na asichukuliwe hatua yoyote. Anadai serikali ameishika. Anatamba hata aje nani hamfanyi lolote. Kweli serikali iangalie watanzania wasinyanyaswe na mgeni kisa pesa. Siku za kukata tama watanzania zikifika hakutakuwa salama hao Leopard.
 
Back
Top Bottom