1. VYETI VYA NIT (MAFUNZO YA KUPATA LESENI MPYA)
Tunasikitika sana kwa sababu tulitakiwa na Serikali kubadilisha leseni jambo ambalo tuliliona ni jema na la busara kuingia katika tecknolojia ya kisasa ya digitali. Sisi kwa sababu ni wengi hapa leopard na kwa pia kampuni hii ya leopard ni kubwa na ina wageni wengi sana haikuwa rahisi kuhudhuria mafunzo ya NIT kwa pamoja wote ila Tajiri wetu alituandalia Darasa la hapa hapa Leopard ambalo lilifanyika katika garage ya Leopard tours njiro, tulifurahia sana tukadhani tajiri wetu anatujali sana kumbe ilikuwa ni tofauti na mawazo yetu, alichokifanya alitulipia gharama za kusoma darasa la NIT ambalo kila mtu alimlipia kiasi cha laki mbili ( 200,000), na kilicho fuata ni kila mwisho wa mwezi tulikuta tunakatwa fedha kidogo kidogo mpaka hilo deni likaisha jambo ambao lilikuwa sio baya hata kidogo,
Cha kushangaza vyeti vyetu vilivyo toka NIT tulitegemea tungepewa ila haikuwa hivyo aliwadanganya watu wa NIT kuwa wamletee yeye ya kuwa atatupatia hivyo vyeti, na kusema ukweli hajawahi kutupatia amevishikilia mpaka sasa hivyo na ni zaidi ya mwaka mmoja sasa !!!! sasa kama alikuwa anavihitaji kwa nini basi asingetulipia na kuacha kutukata kwenye mshahara wetu ili tusiwe na haki ya kudai? Au labda NIT watuambie sheria yao inasemaje ya kuwa mtu akishamaliza chuo chao vyeti wanampa nani? Mwajiri au mhusika?