Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huteuliwa na Raisi kusimamia Wizara zitakazoundwa kulingana na Taaluma zao. Aidha kuna Wizara nyeti ambazo ni lazima taaluma ya Waziri na hata Naibu Waziri izingatiwe sana.
Tuje upande wa pili wa upinzani ambapo kuna mawaziri vivuli, je suala la waziri kivuli na taaluma yake na wizara anayopangiwa, je linazingatiwa?
Mfano John Mnyika ni waziri kivuli katika wizara ya nishati, madini na gesi, je kwa unyeti wa wizara hii, anayo taaluma ya nishati, madini ama gesi?
Godbles Lema nae ni waziri kivuli katika wizara ya ulinzi na usalama, je alishapitia japo mgambo?
Huwa napata shida sana mawaziri vivuli wanapowasilisha bajeti zao maana ni kama unaona kabisa hawajui wanachokiwasilisha pengine kwa kukosa taaluma ya kutosha katika kile wanachokomalia serikali ifanye.