Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,957
- 30,304
HIVI NDIVYO SHEIKH HASSAN BIN AMEIR ALIVYOWEZA KUIINGIZA DAAWAT – UL – ISLAMIYYA BURUNDI KUSAIDIA UKOMBOZI DHIDI YA UKOLONI WA WABELGIJI
Kwa miaka mingi historia ya Sheikh Hassan bin Ameir imekuwa ikielezwa kwa mdomo wanafunzi wake wakiwaeleza watu kazi alizofanya kuanzia sheikh alipokuwa Zanzibar hadi alipohamia Dar es Salaam mwaka wa 1940.
Halikadhalika wanafunzi wake wanaeleza safari zake alizofanya nchini Tanganyika, Belgian Congo, Rwanda na Burundi kote huko akieneza Uislam. Bahati mbaya sana wanafunzi wake hawakulifunua jamvi alilokuwa akikalia Sheikh Hassan bin Ameir kuangalia nini alikuwa ameficha chini yake.
Kwa mtafiti yeyote yule aliyepata kutafiti maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir kabla hajaingia katika siasa kwa uwazi Tanganyika mwaka wa 1950 akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee na kukabiliana na ukoloni uso kwa macho mengi katika historia ya Sheikh Hassan bin Ameir ni usomeshaji wake na uandishi wa vitabu hakuna harakati zake katika uwanja wa siasa.
Historia hii yote imepokewa katika simulizi za mdomo.
Yawezekama mwandishi ndiye mtu wa kwanza kueleza maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir katika maandishi akimweleza kama mmoja wa wazalendo ndani ya TANU waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini kubwa na hili ndilo lililowashangaza wengi ni namna kwa njia ya pekee aliweza kuwaingiza Waislam TANU kumuunga mkono Mwalimu Julius Nyerere kama rais wa TANU na kiongozi wa kudai uhuru.
Mwandishi siku zote alikuwa anajiuliza Sheikh Hassan bin Ameir aliweza vipi kupanda ngazi ile kiasi ya yeye kuwa juu kileleni kama kiongozi wa kwanza Waislam wa Tanganyika yeye akiwa ni Mzanzibari na pili vipi yeye kama Mzanzibari iliwezekanaje kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika pembeni ya Mwalimu Nyerere.
Historia ya Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi inashangaza zaidi.
Hakuna Sheikh katika Afrika ya Mashariki aliyeweza kuingia Belgian Congo, Rwanda na Burundi kumpita Sheikh Hassan bin Ameir akieneza Uislam na wakati huo huo kwa ujanja mkubwa akiwafunza mbinu za siasa.
Waislam wa Congo, Rwanda na Burundi walikuwa wamebaguliwa na Wabelgiji wakawanyima elimu. Wabelgiji waliweka elimu yote katika mikono ya Wakatoliki.
Waislam wa Burundi wenyewe wakijiita Waswahili waliita upendeleo huu ‘’monopole.’’
Waislam walijitahidi sana kupeleka malalamiko ya serikalini lakini hakuna lililofanyika ikawa tegemeo kubwa la Waislam kuwapa watoto wao elimu ni katika madrasa zao ambazo kwa bahati nzuri serikali hawakuziingilia kwani waliziona si tishio katika maslahi yao.
Sheikh Hassan bin Ameir aliwashauri Waislam wa Burundi chini ya ungozi wake waunde jumuiya ya Waislam.
Waislam wa Burundi wakaunda taasisi iliyokuwa ikijulikana kama Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi kwa kifupi ASMARU.
ASMARU ilijikita zaidi katika suala la elimu kwa Waislam na ilishughulika sana katika kupeleka serikalini madai ya Waislam kuhusu kupunjwa elimu wakidai wapewe ‘’subventions,’’ yaani ruzuku kama wafuasi wa dini nyingine ili na wao waweze kujenga shule zao.
Kanisa lilikuwa likitumia shule zao kama moja ya njia ya kuwabadili dini watoto wa Kiislam waliokuwa wanapelekwa kusoma na wazazi wao kwenye shule zao.
Waislam walitoa hoja kuwa wao wanalipa kodi kama raia wengine kwa hiyo wana haki sawa kama raia wenzao wa dini nyingne. Wabelgiji walikuwa wanawapa Waprotestanti 50, 000 F kwa mwaka fungu kubwa zaidi ya hilo likienda kwa Wakatoliki.
Waislam walipoona juhudi zao zote hizi zinagonga ukuta kupitia wakaona waombe msaada kwa kutoka kwa ndugu zao Waislam wa Tanganyika kupitia kwa Sheikh Hassan bin Ameir.
Waislam wa Burundi wakapata msaada na wakajenga shule moja ambayo hadi leo ipo Barabara ya Nane na ya Tisa, Buyenzi na inajulikana kwa jina la Jumuiyya.
Sheikh Hassan bin Ameir alialikwa aje Burundi kuifungua shule hii na ipo hadi leo.
Katika juhudi na harakati hizi taatifa za kikachero zikafikishwa serikalini kuwa Sheikh Hassan bin Ameir kutoka Tanganyika ndiye aliyekuwa akiwachochea Waislam wa Burundi dhidi ya Wabelgiji.
Haiyumkini kabisa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir atakuwa kaingiliana na watu wa Rwanda kwa kiasi ile ikawa yeye hawaelezi hali ya siasa ya Tanganyika na vipi Waurundi kwa kiasi kile cha kuwawezesha kujenga shule asifunze na mbinu za siasa za mapambano.
Uhusiano huu wa Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi uliwatia hofu Wabelgiji kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kwa Waislam wa Burundi wakajiunga na Waislam wenzao wa Tanganyika na kwengineko katika kupambana na serikali.
Katika hali hii ya fitna viongozi wa ya Wabelgiji wakaitisha mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa wazi na kuwataka wananchi wahudhurie mkutano ule.
Yawezekana sana kuwa nia ya mkutano huu ulikuwa kuwaonya wananchi na hasa Waislam kuhusu njama zozote za kupinga serikali. Kufika mchana uwanja wa mkutano ukawa umejaa watu wakisuburi kufika kwa Gavana kuwahutubia.
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mkutano huu pamoja na kundi kubwa la Waislam wake kwa waume wamekaa sehemu yao wametulia wakisubiri kuwasili kwa Gavana uwanjani pale.
Kilichotokea pale uwanjani siku ile kilikuwa hakijaonekana.
Mara msafara wa Gavana ulipoingia uwanjani kwa vishindo vyote wanawake wa Kiislam wakasimama huku wanapiga vigelele kwa sauti ya juu sana.
Uwanja mzima ulipigwa na butwaa wakiwaangalia na kuwashangaa wanawake walijitanda vizuri waliokuwa wakipiga vigelegele kumshangilia Gavana.
Uwanja ulisisimka na waliokuwapo wakawa wamepigwa na mshagao pamoja na Gavana mwenyewe.
Walikuwa hawajapata kuona kitu kama hicho kabla.
Gavana alipokaa wale wanawake wakanyamaza na wao wakakaa.
Ulipita ukimya mzito watu wakitafakari kile kilichotokea pale uwanjani.
Gavana aliposimama kuzungumza kitu cha kwanza alichouliza ni kuwa wale waliokuwa wanapiga vigelegele ni nani na wametokea wapi?
Gavana akaelezwa kuwa wale ni raia wake Waislam wakiongozwa na kiongozi wao kutoka Tanganyika, Sheikh Hassan bin Ameir.
Pale pale Gavana akawashukuru kwa kumuadhimisha kwa kiasi kile na akaagiza kuwa Sheikh Hassan bin Ameir ni mtu wa Mungu yeye na watu wake wasibughudhiwe.
Vyama vya siasa vilipoanza Burundi viongozi wa vyama hivi walikuja kuwa karibu sana na TANU kutokana na msingi huu alioweka Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam hawakusita kujiunga kwa wingi katika vyama hivi.
Viongozi wa vyama hivi wakawa wanaiangalia TANU na viongozi wake kama taa ya kuwaangazi kwenye kile kiza chao chini ya Wabelgiji na walihangaika sana kutaka na wao watiwe katika ‘’Panafricanisme,’’ kama Warundi walivyoita yaani, Pan African Freedom Movement in East and Central Africa (PAFMECA).
Haya ni katika mengi sana kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir ambayo bado hayajafanyiwa utafiti wa kutosha.
Msomaji huu ni mukadama yaani utangulizi na kilichonifanya niandike utangulizi huu ni nyaraka niliyoiona ‘’news letter,’’ Sauti ya Islam (Daawat – ul – Islamiyya Dar es Salaam Chini ya Uangalizi wa Raisi Sheikh Hassan bin Ameir el Shirazy) August 1945 No. 4.
In Shaa Allah itaendelea...