Hivi ndivyo Sheikh Hassan bin Aameir alivyoweza kuiingiza Daawat – ul – Islamiyya Burundi kusaidia ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wabelgiji

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
HIVI NDIVYO SHEIKH HASSAN BIN AMEIR ALIVYOWEZA KUIINGIZA DAAWAT – UL – ISLAMIYYA BURUNDI KUSAIDIA UKOMBOZI DHIDI YA UKOLONI WA WABELGIJI

Kwa miaka mingi historia ya Sheikh Hassan bin Ameir imekuwa ikielezwa kwa mdomo wanafunzi wake wakiwaeleza watu kazi alizofanya kuanzia sheikh alipokuwa Zanzibar hadi alipohamia Dar es Salaam mwaka wa 1940.

Halikadhalika wanafunzi wake wanaeleza safari zake alizofanya nchini Tanganyika, Belgian Congo, Rwanda na Burundi kote huko akieneza Uislam. Bahati mbaya sana wanafunzi wake hawakulifunua jamvi alilokuwa akikalia Sheikh Hassan bin Ameir kuangalia nini alikuwa ameficha chini yake.

Kwa mtafiti yeyote yule aliyepata kutafiti maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir kabla hajaingia katika siasa kwa uwazi Tanganyika mwaka wa 1950 akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee na kukabiliana na ukoloni uso kwa macho mengi katika historia ya Sheikh Hassan bin Ameir ni usomeshaji wake na uandishi wa vitabu hakuna harakati zake katika uwanja wa siasa.

Historia hii yote imepokewa katika simulizi za mdomo.

Yawezekama mwandishi ndiye mtu wa kwanza kueleza maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir katika maandishi akimweleza kama mmoja wa wazalendo ndani ya TANU waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kubwa na hili ndilo lililowashangaza wengi ni namna kwa njia ya pekee aliweza kuwaingiza Waislam TANU kumuunga mkono Mwalimu Julius Nyerere kama rais wa TANU na kiongozi wa kudai uhuru.

Mwandishi siku zote alikuwa anajiuliza Sheikh Hassan bin Ameir aliweza vipi kupanda ngazi ile kiasi ya yeye kuwa juu kileleni kama kiongozi wa kwanza Waislam wa Tanganyika yeye akiwa ni Mzanzibari na pili vipi yeye kama Mzanzibari iliwezekanaje kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika pembeni ya Mwalimu Nyerere.

Historia ya Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi inashangaza zaidi.

Hakuna Sheikh katika Afrika ya Mashariki aliyeweza kuingia Belgian Congo, Rwanda na Burundi kumpita Sheikh Hassan bin Ameir akieneza Uislam na wakati huo huo kwa ujanja mkubwa akiwafunza mbinu za siasa.

Waislam wa Congo, Rwanda na Burundi walikuwa wamebaguliwa na Wabelgiji wakawanyima elimu. Wabelgiji waliweka elimu yote katika mikono ya Wakatoliki.

Waislam wa Burundi wenyewe wakijiita Waswahili waliita upendeleo huu ‘’monopole.’’

Waislam walijitahidi sana kupeleka malalamiko ya serikalini lakini hakuna lililofanyika ikawa tegemeo kubwa la Waislam kuwapa watoto wao elimu ni katika madrasa zao ambazo kwa bahati nzuri serikali hawakuziingilia kwani waliziona si tishio katika maslahi yao.

Sheikh Hassan bin Ameir aliwashauri Waislam wa Burundi chini ya ungozi wake waunde jumuiya ya Waislam.

Waislam wa Burundi wakaunda taasisi iliyokuwa ikijulikana kama Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi kwa kifupi ASMARU.

ASMARU ilijikita zaidi katika suala la elimu kwa Waislam na ilishughulika sana katika kupeleka serikalini madai ya Waislam kuhusu kupunjwa elimu wakidai wapewe ‘’subventions,’’ yaani ruzuku kama wafuasi wa dini nyingine ili na wao waweze kujenga shule zao.

Kanisa lilikuwa likitumia shule zao kama moja ya njia ya kuwabadili dini watoto wa Kiislam waliokuwa wanapelekwa kusoma na wazazi wao kwenye shule zao.

Waislam walitoa hoja kuwa wao wanalipa kodi kama raia wengine kwa hiyo wana haki sawa kama raia wenzao wa dini nyingne. Wabelgiji walikuwa wanawapa Waprotestanti 50, 000 F kwa mwaka fungu kubwa zaidi ya hilo likienda kwa Wakatoliki.

Waislam walipoona juhudi zao zote hizi zinagonga ukuta kupitia wakaona waombe msaada kwa kutoka kwa ndugu zao Waislam wa Tanganyika kupitia kwa Sheikh Hassan bin Ameir.

Waislam wa Burundi wakapata msaada na wakajenga shule moja ambayo hadi leo ipo Barabara ya Nane na ya Tisa, Buyenzi na inajulikana kwa jina la Jumuiyya.

Sheikh Hassan bin Ameir alialikwa aje Burundi kuifungua shule hii na ipo hadi leo.

Katika juhudi na harakati hizi taatifa za kikachero zikafikishwa serikalini kuwa Sheikh Hassan bin Ameir kutoka Tanganyika ndiye aliyekuwa akiwachochea Waislam wa Burundi dhidi ya Wabelgiji.

Haiyumkini kabisa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir atakuwa kaingiliana na watu wa Rwanda kwa kiasi ile ikawa yeye hawaelezi hali ya siasa ya Tanganyika na vipi Waurundi kwa kiasi kile cha kuwawezesha kujenga shule asifunze na mbinu za siasa za mapambano.

Uhusiano huu wa Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi uliwatia hofu Wabelgiji kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kwa Waislam wa Burundi wakajiunga na Waislam wenzao wa Tanganyika na kwengineko katika kupambana na serikali.

Katika hali hii ya fitna viongozi wa ya Wabelgiji wakaitisha mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa wazi na kuwataka wananchi wahudhurie mkutano ule.

Yawezekana sana kuwa nia ya mkutano huu ulikuwa kuwaonya wananchi na hasa Waislam kuhusu njama zozote za kupinga serikali. Kufika mchana uwanja wa mkutano ukawa umejaa watu wakisuburi kufika kwa Gavana kuwahutubia.

Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mkutano huu pamoja na kundi kubwa la Waislam wake kwa waume wamekaa sehemu yao wametulia wakisubiri kuwasili kwa Gavana uwanjani pale.

Kilichotokea pale uwanjani siku ile kilikuwa hakijaonekana.

Mara msafara wa Gavana ulipoingia uwanjani kwa vishindo vyote wanawake wa Kiislam wakasimama huku wanapiga vigelele kwa sauti ya juu sana.

Uwanja mzima ulipigwa na butwaa wakiwaangalia na kuwashangaa wanawake walijitanda vizuri waliokuwa wakipiga vigelegele kumshangilia Gavana.

Uwanja ulisisimka na waliokuwapo wakawa wamepigwa na mshagao pamoja na Gavana mwenyewe.
Walikuwa hawajapata kuona kitu kama hicho kabla.

Gavana alipokaa wale wanawake wakanyamaza na wao wakakaa.

Ulipita ukimya mzito watu wakitafakari kile kilichotokea pale uwanjani.

Gavana aliposimama kuzungumza kitu cha kwanza alichouliza ni kuwa wale waliokuwa wanapiga vigelegele ni nani na wametokea wapi?

Gavana akaelezwa kuwa wale ni raia wake Waislam wakiongozwa na kiongozi wao kutoka Tanganyika, Sheikh Hassan bin Ameir.

Pale pale Gavana akawashukuru kwa kumuadhimisha kwa kiasi kile na akaagiza kuwa Sheikh Hassan bin Ameir ni mtu wa Mungu yeye na watu wake wasibughudhiwe.

Vyama vya siasa vilipoanza Burundi viongozi wa vyama hivi walikuja kuwa karibu sana na TANU kutokana na msingi huu alioweka Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam hawakusita kujiunga kwa wingi katika vyama hivi.

Viongozi wa vyama hivi wakawa wanaiangalia TANU na viongozi wake kama taa ya kuwaangazi kwenye kile kiza chao chini ya Wabelgiji na walihangaika sana kutaka na wao watiwe katika ‘’Panafricanisme,’’ kama Warundi walivyoita yaani, Pan African Freedom Movement in East and Central Africa (PAFMECA).

Haya ni katika mengi sana kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir ambayo bado hayajafanyiwa utafiti wa kutosha.

Msomaji huu ni mukadama yaani utangulizi na kilichonifanya niandike utangulizi huu ni nyaraka niliyoiona ‘’news letter,’’ Sauti ya Islam (Daawat – ul – Islamiyya Dar es Salaam Chini ya Uangalizi wa Raisi Sheikh Hassan bin Ameir el Shirazy) August 1945 No. 4.

In Shaa Allah itaendelea...
 
Hassan Ameir ndio sheikh pekee katika historia ya waislam, aliefukuzwa umufti kwa utovu wa nidhamu.
Laki...
Mimi nimefanya staha hapa kwa kuandika historia hii kwa uangalifu mkubwa na kujizuia kueleza mengi ambayo yangeshusha historia ya baadhi ya viongozi wetu.

Wewe huijui historia ya Sheikh Hassan bin Ameir unasema tu linalokujia hata kama litakuwa tusi kwetu.

Huu so ustaarabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hakufukizwa umufti?
 
Kwani hakufukizwa umufti?
Remote,
Sheikh Hassan bin Ameir hakufukuzwa kwenye nafasi ya Mufti.

Ilipodhihirika kuwa lazima EAMWS ivunjwe kuzuia ujenzi wa Chuo Kikuu ikawa kuwa kuunda BAKWATA ilhali Sheikh Hassan bin Ameir bado anaishi Tanganyika na ndiye Mufti wa Tanganyika uongozi wa BAKWATA utapata shida.

Utapata shida uongozi wa BAKWATA kwa sababu kati ya wale wote waliokuwa wanategemewa kukabidhiwa uongozi wa BAKWATA hakuna aliyemkaribia Sheikh Hassan bin Ameir kwa ilm.

Uamuzi wa serikali ukawa Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe usiku nyumbani kwake atiwe ndani ya ndege arudishwe Zanzibar na asiruhusiwe kukanyaga ardhi ya Tanganyika maisha yake yote.

Baada ya haya kufanyika ndiyo BAKWATA ikafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wake.

Naamini hili suala limeeleweka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mod hii peleka jukwaa la dini.
Remote,
Sheikh Hassan bin Ameir kama walivyokuwa masheikh wengi ndani ya TANU walikuwa na sura mbili.

Kwanza walikuwa masheikh wanazuoni wa dini na pili walikuwa wanasiasa wapigania uhuru.

Hapa tunamzungumza Sheikh Hassan bin Ameir mwanasiasa.

Wote walikuwa wanachama Shupavu wa TANU.

Sheikh Mussa Rehani Makuka alipewa Kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji na Sheikh Hassan Bin Ameir siku ya Ijumaa baada ya Sala.

Sheikh Hassan Bin Ameir akiwa katika juhudi za kuhuisha TANU na Harakati za Uhuru.

Hata Bwana Kambarage Nyerere alipokuja Ujiji kwa mara ya Kwanza walikuja na barua maalum aliyokuja nayo Sheikh Suleiman Taqadir toka kwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo kuwaomba wazee wa Ujiji wawapokee vijana wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, samahani inaonekana lugha ya kufukuzwa umufti hukupendezwa nayo , basi tutumie hili neno, "alipinduliwa umufti" na BAKWATA. BAKWATA hawa unaowachukia ndio wamewajengea waislamu chuo kikuu morogoro,
 
Tatizo kubwa ulilokuwanalo wewe ni kutoijua historia hii tunayojadili na mengine ndani ya nafsi yako yanayokutaabisha.

Historia ya Sheikh Hassan bin Ameir Burundi imewasisimua wengi.

"Inspiration," ya kuandika utangulizi ule ni news letter ya Daawatul Islamiyya ya August 1945.

Naandika kitabu na hayo ni utangulizi wa moja ya sura inayomuhusu Sheikh Hassan bin Ameir.

Kwako wewe yote yale hukuyaona ila kuja na kejeli.

Wala BAKWATA si waliomfukuza Sheikh Hassan bin Ameir Tanganyika kwani hawakuwapo bado na hata kama wangelikuwapo hawakuwa na uwezo wa kufanya hilo.

Lakini yapo mengine wewe huyajui watu wa BAKWATA nini ulikuwa mwisho wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, Hassan Ameir alifukuzwa Tanganyika kwa kuchanganya dini na siasa, na hii ndio shida ya waislamu wengi kuweka dini mbele zaidi ya maslahi na maendeleo ya nchi. waislamu wengi baada ya uhuru, badala ya kushirikiana na serikali ya TANU, wakawa wapinzani wa serikali
 
Laki
Kumbuka walioisaidia hii inchi kupata uhuru kwa hali na mali ni WAISLAM lakin baadae wakaanza kubaguliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, Hassan Ameir alifukuzwa Tanganyika kwa kuchanganya dini na siasa, na hii ndio shida ya waislamu wengi kuweka dini mbele zaidi ya maslahi na maendeleo ya nchi. waislamu wengi baada ya uhuru, badala ya kushirikiana na serikali ya TANU, wakawa wapinzani wa serikali
Laki...
Unazungumza jambo usilokuwa na ujuzinalo.

Hivi unafahamu kuwa ni Sheikh Hassan bin Ameir aliyesaidia kuiongoza TANU kuwa "a nationalist-secularist party?"

Unajua alitoa hotoba ya muongozo huu kwenye mkutano uliofanyika Mtaa wa Pemba na ulihudhuriwa na masheikh mmoja wapo akiwa Sheikh Nurdin Hussein na Abdallah Chaurembo pamoja na viongozi wa TANU mmojawapo Rajab Diwani?

Hili ilikuwa 1955.

Unajua kuwa katika vijana waliomsaidia katika kazi hii walikuwa Bantu Group na hawa akina Abbas Bakis walikuwa vijana wa Kiislam?

Mimi najizuia kueleza mengi kwa kuwa si lazima kila kitu kisemwe.

Kwa nini hujiulizi historia hii mbona ilifutwa?

Tatizo lilikuwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Waislam si kuchangia dini na siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, historia ya hao wazee wako akina sheikh Hassan Ameir haikufutwa, bali hakuna alieiandika, na bahati mbaya na wao hawakuandika historia yao. wapigania uhuru walikuwd wengi sana haingewezekana kuandika historia yao wote
 
ingeleta maana kama historia ya wazee wako ingekuwa imeandikwa , halafu ikafutwa, lakin kulalamika tu eti imefutwa, wakati haijawah kuandikwa, haileti maana, mfano, waasisi wa TANU walikuwa 17, lakini mpaka leo kuna wengine hawajulikani kabisa, mfano Geremano Pacha, Joseph Kamalando, Milinga, Kisunguta Gabara, Patrick Kunambi, bora hao akina Sykes wanajulikana kidogo
 
miaka ya 50s na 60s kuanzisha chuo kikuu cha waislamu isingeleta taswira nzuri, waislamu walikuwa wako huru kusoma shule za mission zilizotaifishwa kutoka kwa wakoloni, kuanzisha chuo cha dini kungeleta mgawanyiko wa jamii
 
Laki so pesa
.mbona shule na vyuo vya wakristo zilitaidishwa mwaka 1967 na sio miaka ya nyuma kama unavyodai

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI NDIVYO SHEIKH HASSAN BIN AMEIR ALIVYOWEZA KUIINGIZA DAAWAT – UL – ISLAMIYYA BURUNDI KUSAIDIA UKOMBOZI DHIDI YA UKOLONI WA WABELGIJI

Kwa miaka mingi historia ya Sheikh Hassan bin Ameir imekuwa ikielezwa kwa mdomo wanafunzi wake wakiwaeleza watu kazi alizofanya kuanzia sheikh alipokuwa Zanzibar hadi alipohamia Dar es Salaam mwaka wa 1940.

Halikadhalika wanafunzi wake wanaeleza safari zake alizofanya nchini Tanganyika, Belgian Congo, Rwanda na Burundi kote huko akieneza Uislam. Bahati mbaya sana wanafunzi wake hawakulifunua jamvi alilokuwa akikalia Sheikh Hassan bin Ameir kuangalia nini alikuwa ameficha chini yake.

Kwa mtafiti yeyote yule aliyepata kutafiti maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir kabla hajaingia katika siasa kwa uwazi Tanganyika mwaka wa 1950 akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommittee na kukabiliana na ukoloni uso kwa macho mengi katika historia ya Sheikh Hassan bin Ameir ni usomeshaji wake na uandishi wa vitabu hakuna harakati zake katika uwanja wa siasa.

Historia hii yote imepokewa katika simulizi za mdomo.

Yawezekama mwandishi ndiye mtu wa kwanza kueleza maisha ya Sheikh Hassan bin Ameir katika maandishi akimweleza kama mmoja wa wazalendo ndani ya TANU waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kubwa na hili ndilo lililowashangaza wengi ni namna kwa njia ya pekee aliweza kuwaingiza Waislam TANU kumuunga mkono Mwalimu Julius Nyerere kama rais wa TANU na kiongozi wa kudai uhuru.

Mwandishi siku zote alikuwa anajiuliza Sheikh Hassan bin Ameir aliweza vipi kupanda ngazi ile kiasi ya yeye kuwa juu kileleni kama kiongozi wa kwanza Waislam wa Tanganyika yeye akiwa ni Mzanzibari na pili vipi yeye kama Mzanzibari iliwezekanaje kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika pembeni ya Mwalimu Nyerere.

Historia ya Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi inashangaza zaidi.

Hakuna Sheikh katika Afrika ya Mashariki aliyeweza kuingia Belgian Congo, Rwanda na Burundi kumpita Sheikh Hassan bin Ameir akieneza Uislam na wakati huo huo kwa ujanja mkubwa akiwafunza mbinu za siasa.

Waislam wa Congo, Rwanda na Burundi walikuwa wamebaguliwa na Wabelgiji wakawanyima elimu. Wabelgiji waliweka elimu yote katika mikono ya Wakatoliki.

Waislam wa Burundi wenyewe wakijiita Waswahili waliita upendeleo huu ‘’monopole.’’

Waislam walijitahidi sana kupeleka malalamiko ya serikalini lakini hakuna lililofanyika ikawa tegemeo kubwa la Waislam kuwapa watoto wao elimu ni katika madrasa zao ambazo kwa bahati nzuri serikali hawakuziingilia kwani waliziona si tishio katika maslahi yao.

Sheikh Hassan bin Ameir aliwashauri Waislam wa Burundi chini ya ungozi wake waunde jumuiya ya Waislam.

Waislam wa Burundi wakaunda taasisi iliyokuwa ikijulikana kama Association Scolaire Musulmane du Ruanda-Urundi kwa kifupi ASMARU.

ASMARU ilijikita zaidi katika suala la elimu kwa Waislam na ilishughulika sana katika kupeleka serikalini madai ya Waislam kuhusu kupunjwa elimu wakidai wapewe ‘’subventions,’’ yaani ruzuku kama wafuasi wa dini nyingine ili na wao waweze kujenga shule zao.

Kanisa lilikuwa likitumia shule zao kama moja ya njia ya kuwabadili dini watoto wa Kiislam waliokuwa wanapelekwa kusoma na wazazi wao kwenye shule zao.

Waislam walitoa hoja kuwa wao wanalipa kodi kama raia wengine kwa hiyo wana haki sawa kama raia wenzao wa dini nyingne. Wabelgiji walikuwa wanawapa Waprotestanti 50, 000 F kwa mwaka fungu kubwa zaidi ya hilo likienda kwa Wakatoliki.

Waislam walipoona juhudi zao zote hizi zinagonga ukuta kupitia wakaona waombe msaada kwa kutoka kwa ndugu zao Waislam wa Tanganyika kupitia kwa Sheikh Hassan bin Ameir.

Waislam wa Burundi wakapata msaada na wakajenga shule moja ambayo hadi leo ipo Barabara ya Nane na ya Tisa, Buyenzi na inajulikana kwa jina la Jumuiyya.

Sheikh Hassan bin Ameir alialikwa aje Burundi kuifungua shule hii na ipo hadi leo.

Katika juhudi na harakati hizi taatifa za kikachero zikafikishwa serikalini kuwa Sheikh Hassan bin Ameir kutoka Tanganyika ndiye aliyekuwa akiwachochea Waislam wa Burundi dhidi ya Wabelgiji.

Haiyumkini kabisa kuwa Sheikh Hassan bin Ameir atakuwa kaingiliana na watu wa Rwanda kwa kiasi ile ikawa yeye hawaelezi hali ya siasa ya Tanganyika na vipi Waurundi kwa kiasi kile cha kuwawezesha kujenga shule asifunze na mbinu za siasa za mapambano.

Uhusiano huu wa Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wa Burundi uliwatia hofu Wabelgiji kuwa kuna uwezekano mkubwa sana kwa Waislam wa Burundi wakajiunga na Waislam wenzao wa Tanganyika na kwengineko katika kupambana na serikali.

Katika hali hii ya fitna viongozi wa ya Wabelgiji wakaitisha mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa wazi na kuwataka wananchi wahudhurie mkutano ule.

Yawezekana sana kuwa nia ya mkutano huu ulikuwa kuwaonya wananchi na hasa Waislam kuhusu njama zozote za kupinga serikali. Kufika mchana uwanja wa mkutano ukawa umejaa watu wakisuburi kufika kwa Gavana kuwahutubia.

Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mkutano huu pamoja na kundi kubwa la Waislam wake kwa waume wamekaa sehemu yao wametulia wakisubiri kuwasili kwa Gavana uwanjani pale.

Kilichotokea pale uwanjani siku ile kilikuwa hakijaonekana.

Mara msafara wa Gavana ulipoingia uwanjani kwa vishindo vyote wanawake wa Kiislam wakasimama huku wanapiga vigelele kwa sauti ya juu sana.

Uwanja mzima ulipigwa na butwaa wakiwaangalia na kuwashangaa wanawake walijitanda vizuri waliokuwa wakipiga vigelegele kumshangilia Gavana.

Uwanja ulisisimka na waliokuwapo wakawa wamepigwa na mshagao pamoja na Gavana mwenyewe.
Walikuwa hawajapata kuona kitu kama hicho kabla.

Gavana alipokaa wale wanawake wakanyamaza na wao wakakaa.

Ulipita ukimya mzito watu wakitafakari kile kilichotokea pale uwanjani.

Gavana aliposimama kuzungumza kitu cha kwanza alichouliza ni kuwa wale waliokuwa wanapiga vigelegele ni nani na wametokea wapi?

Gavana akaelezwa kuwa wale ni raia wake Waislam wakiongozwa na kiongozi wao kutoka Tanganyika, Sheikh Hassan bin Ameir.

Pale pale Gavana akawashukuru kwa kumuadhimisha kwa kiasi kile na akaagiza kuwa Sheikh Hassan bin Ameir ni mtu wa Mungu yeye na watu wake wasibughudhiwe.

Vyama vya siasa vilipoanza Burundi viongozi wa vyama hivi walikuja kuwa karibu sana na TANU kutokana na msingi huu alioweka Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam hawakusita kujiunga kwa wingi katika vyama hivi.

Viongozi wa vyama hivi wakawa wanaiangalia TANU na viongozi wake kama taa ya kuwaangazi kwenye kile kiza chao chini ya Wabelgiji na walihangaika sana kutaka na wao watiwe katika ‘’Panafricanisme,’’ kama Warundi walivyoita yaani, Pan African Freedom Movement in East and Central Africa (PAFMECA).

Haya ni katika mengi sana kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir ambayo bado hayajafanyiwa utafiti wa kutosha.

Msomaji huu ni mukadama yaani utangulizi na kilichonifanya niandike utangulizi huu ni nyaraka niliyoiona ‘’news letter,’’ Sauti ya Islam (Daawat – ul – Islamiyya Dar es Salaam Chini ya Uangalizi wa Raisi Sheikh Hassan bin Ameir el Shirazy) August 1945 No. 4.

In Shaa Allah itaendelea...
Mzee Mohamed naomba nikuulize swali moja!hivi kwa nini kila mara anapokuwepo sheikh anatangaza dini unamuhusisha na siasa za uhuru
 
Mohamed Said, historia ya hao wazee wako akina sheikh Hassan Ameir haikufutwa, bali hakuna alieiandika, na bahati mbaya na wao hawakuandika historia yao. wapigania uhuru walikuwd wengi sana haingewezekana kuandika historia yao wote
Laki...
Hassan Upeka alikuwa kachero wa TANU toka alipomaliza shule Tabora 1956 na kuajiriwa na TANU mwaka huo.

Baada ya uhuru akapelekwa mafunzoni Israel, Yugoslavia na kwengine kwingi.

Yeye ndiye aliyeanzisha Maktaba ya CCM Dodoma pamoja na Ditopile Mzuzuri.

Upeka kwangu mimi ni kaka na yeye siku zote akinichukulia mimi kama bwana mdogo wake.

Upeka alikuwa kwenye jopo la Chuo Cha CCM Kivukoni lililoandika historia yaTANU na uhuru wa Tanganyika aliwazidi wenzake kwa umri na kuijua TANU.

Upeka kazaliwa Dar es Salaam.

Alileta kwenye jopo lile "notes," za mazungumzo aliyofanya na Abdul Sykes kabla hajafa kuhusu historia ya TANU.

Mwenyekiti wa jopo alikataa kupokea "notes," zile kwa madai kuwa historia wanayoandika haina uhusiano wowote na Abdul Sykes.

Ikawa jopo limemkataa Abdul Sykes katika TANU na ukimtoa Abdul ndiyo umemtoa na baba yake Kleist muasisi wa African Association pamoja na historia yote ya nyuma.

Lakini kubwa zaidi ndiyo umemfuta na Sheikh Hassan bin Ameir ambae Abdul Sykes ndiye alimuingiza katika TAA Political Subcommittee 1950.

Nimemtaja Hassan Upeka kwenye utangulizi wa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Viongozi waasisi wa TANU na wapigania uhuru wa Tanganyika wanafahamika wote na hawakuwa wengi kushindwa kuadhimishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mohamed naomba nikuulize swali moja!hivi kwa nini kila mara anapokuwepo sheikh anatangaza dini unamuhusisha na siasa za uhuru
Mtoto...
Jibu lako nimeitoa kutoka kwa ndugu yangu Hamisi Hababi hilo hapo chini:

"Sheikh Mussa Rehani Makuka alipewa Kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji na Sheikh Hassan Bin Ameir siku ya Ijumaa baada ya Sala.

Sheikh Hassan Bin Ameir akiwa katika juhudi za kuhuisha TANU na Harakati za Uhuru.

Hata Bwana Kambarage Nyerere alipokuja Ujiji kwa Mara ya Kwanza walikuja na Barua maalum aliyokuja nayo Sheikh Suleiman Taqadir toka kwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo kuwaomba wazee wa Ujiji wawapokee vijana wao."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom