Hivi ndivyo Roman Catholic ilivyo

Hivi ndivyo Roman Catholic ilivyo

Wasabato wanajumuishwa na hao wengine na wanatambuliwa kama mojawapo ya Christian cults zilizofanikiwa sana. Mojawapo ya mafundisho yao yanayopingana na Biblia ni hili: Wanaamini kuwa Yesu hakukamilisha kazi ya wokovu pale msalabani na kuanzia mwaka 1884 aliingia Patakatifu pa Patakatifu (Holly of Hollies) kuendelea kutuombea mbele ya Mungu Baba. Halafu wana kiherehere cha kutabiri kila jambo linalotokea duniani na kulihusisha na unabii. Yaani ukiwasikiliza aisee hutaweza kuishi. Ndiyo maana mwaka 1884 mwanzilishi wao aliwarubuni wafuasi wake kuwa mwaka huo Yesu anarudi wakauza kila kitu kumbe uwongo. Baadaye ndiyo ikasahihishwa kwamba mwaka 1884 haukuwa wa kurudi kwa Yesu bali ni Yesu alikuwa anahamia kwenye chumba cha Patakatifu pa Patakatifu huko mbinguni tayari kuanza kazi ya kutuombea mbele ya Mungu Baba.

Wanaweka msisitizo usio na sababu juu ya sheria za Musa hasa juu ya vyakula na ushikaji wa Sabato. Hakuna kula samaki wasio na magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika au wasiocheua na siku ya Sabato hairuhusiwi hata kupika. Msisitizo huu katika sheria za Musa hata Yesu aliukemea mara nyingi na alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na Mafarisayo. Ndiyo maana aliwakemea walipomzonga baada ya kumponya mtu siku ya Sabato na kumwambia ajitwike godoro lake aende.

Wanadhani kuwa kushika sheria hizi ndiyo kutawaokoa na wanadhani kuwa kwa kushika misheria hii ya Musa basi wao ni watakatifu kuliko Wakristo wengine. Kumbe Biblia na Yesu mwenyewe walifundisha kinyume chake. Yaani ni mvurugano mtupu lakini wanaamini kuwa wao ndiyo watakatifu pekee watakaokwenda mbinguni.
Mkuu nakushukuru sana yaani umenifungua nasoma sana agano la kale nakutana na hawa mafarisayo na masadukayo siwaelewi ni wakina nani!!

Mara wakasirike pale wanafunzi wa Yesu wanakula bila kunawa yaani visheria vingi vigumu vugumu..

Kumbe ndo kama hawa Wasabato mkuu???
 
Ukweli huwa unauma aiseee!!!!
Anyway ila ndo ukweli utafanyaje sasa.
 
Kwani kuna tofauti kati ya MSABATO NA MKRISTO?labda uje ja hoja zilizo wazi msabato sio mkristo?
Tujue kwanza maana ya mkristo ndo tutajua nani mkristo na nan sio.
 
Kaka umenikumbusha kitu wakati niko Dar. Kuna msabato mmoja alinipa ratiba nzima ya nchi atakazotembelea papa. Wakati huo alikua papa Benedict xvi. Katiaka ratiba aliyo nipa hakuna hata moja iliyotimia badala yake alienda uingereza ambayo haikuwemo hata kwenye ratiba yake. Akanipa viatabu vyote ni kuhusu papa. Mara the great controversy, America in history, secret terrorists. Vyote ukisoma ni papa na ukatoliki. Ikamuuliza hivi vitabu vinanijengaje kiroho. Akaniambia nitujua ukweli. Yani kwa msabato dhambi ni ukatoliki. Wanawafundisha judo vijana wao "Adventtist youth" eti ili wapambane na wakatoliki siku ya kulazimisha Sunday law. Kila zuri kanisa katoliki linalofanya wao wanaona ni mwanzo wa ukamilifu wa unabii wa ellen White. Kwa ujumla ukitaka hata kumgonga demu wa kisabato msifie mama white na mchukie papa. Hawa watu ni shida! Sasa naona hizi uzi za papa na ukatoliki zimejaa. Hii itakuwa propaganda zao sasa humu ndo wanakutana na wajanja. Majibu watapata kutoka kwa werevu na matusi watapata kutoka kwa machizi!
Wameleta uzi wakasepa...Ukishawagusia kihusu historia yao chafu wanakimbia
 
Mkuu nakushukuru sana yaani umenifungua nasoma sana agano la kale nakutana na hawa mafarisayo na masadukayo siwaelewi ni wakina nani!!

Mara wakasirike pale wanafunzi wa Yesu wanakula bila kunawa yaani visheria vingi vigumu vugumu..

Kumbe ndo kama hawa Wasabato mkuu???
Ulikuwa hujui kuwa Wasabato ni Mafarisayo...?
 
Ukitembelea hata Wikipedia ukiandika world Christian....Hapo utapata list of all Christians denomination

Ila wanaenda mbele wana-specify
"Other Groups that claims also to be Christian"
Hapo zinatajwa cult 4
1. Mormon
2. Seventh Day Adventist
3. Jehova Witness
4. Christian scientology
Unatia huruma.yaani wikipedia ndio reliable source kwako? Sisi tunategemea Biblia na sio wikipedia.
 
Maandiko katika biblia yanasema, dini safi ni hii kutazama wagonjwa, kusaidia yatima na wajane na kujilinda na dunia usitende dhambi. Mi naishi ktk misingi hiyo!
 
Wasabato wanajumuishwa na hao wengine na wanatambuliwa kama mojawapo ya Christian cults zilizofanikiwa sana. Mojawapo ya mafundisho yao yanayopingana na Biblia ni hili: Wanaamini kuwa Yesu hakukamilisha kazi ya wokovu pale msalabani na kuanzia mwaka 1884 aliingia Patakatifu pa Patakatifu (Holly of Hollies) kuendelea kutuombea mbele ya Mungu Baba. Halafu wana kiherehere cha kutabiri kila jambo linalotokea duniani na kulihusisha na unabii. Yaani ukiwasikiliza aisee hutaweza kuishi. Ndiyo maana mwaka 1884 mwanzilishi wao aliwarubuni wafuasi wake kuwa mwaka huo Yesu anarudi wakauza kila kitu kumbe uwongo. Baadaye ndiyo ikasahihishwa kwamba mwaka 1884 haukuwa wa kurudi kwa Yesu bali ni Yesu alikuwa anahamia kwenye chumba cha Patakatifu pa Patakatifu huko mbinguni tayari kuanza kazi ya kutuombea mbele ya Mungu Baba.

Wanaweka msisitizo usio na sababu juu ya sheria za Musa hasa juu ya vyakula na ushikaji wa Sabato. Hakuna kula samaki wasio na magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika au wasiocheua na siku ya Sabato hairuhusiwi hata kupika. Msisitizo huu katika sheria za Musa hata Yesu aliukemea mara nyingi na alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na Mafarisayo. Ndiyo maana aliwakemea walipomzonga baada ya kumponya mtu siku ya Sabato na kumwambia ajitwike godoro lake aende.

Wanadhani kuwa kushika sheria hizi ndiyo kutawaokoa na wanadhani kuwa kwa kushika misheria hii ya Musa basi wao ni watakatifu kuliko Wakristo wengine. Kumbe Biblia na Yesu mwenyewe walifundisha kinyume chake. Yaani ni mvurugano mtupu lakini wanaamini kuwa wao ndiyo watakatifu pekee watakaokwenda mbinguni.
Uongo ni dhambi,na kila asemaye uongo ni wa ibilisi kwani yeye ndiye baba wa huo.
 
Wasabato na mauzauza yao. Yaani hata Papa akijamba tayari unabii umetimia. Wakati huo huo hata wenyewe historia yao kuanzia kwa mwanzilishi wao Miller na kuendelea mpaka kwa "nabii" wao mama Ellen G. White imejaa mauzauza tupu. Na wanaamini kabisa kuwa wao peke yao ndiyo watakwenda mbinguni kisa eti wanaabudu siku ya Jumamosi, hawali samaki wasio na magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika na wale wasiocheua

Unajua waafrika ni watu wa ajabu sana. Mzungu kaleta dini kwa malengo yake lakini huku kila siku watu kulumbana mara oh nan kafanya nini. Waliozileta wametulia wanaendelea na kuiba rasilimali zetu. Hao akin Mama White ni binadamu tu lkn wanatukuzwa kuliko mama zetu kisa eti watu wanadanganywa kuwa ni mitume sijui manabii wa wap. Aliyeturoga kishakufa
 
Ukizijua the Four Cult hutopata shida...

Sasa mada yenyewe imeletwa na mmoja ya cult nani wa kupoteza muda....

Tupoteze muda na takataka kama SDA, Mashahidi wa Yehova..? Acha utani bana..

The Four Cult Religion on Earth
Seventh Day Adventist
Mormon
Jehova Witness
Christian Scientology
Tatizo lenu mnakaririshwa ujinga na hao mapadre wenu hata hamhoji kama huo uzushi una support yeyote ya Biblia.Eti source wikipedia! too pathetic!
 
Anaitwa prof walter j veith angalia Youtube lecture zake amefanya research kuhusu maelezo yote na source zote za vatican upapa na ujesuit na NWO agendas freemasons jinsi wanavyoshirikia katika kuhakikisha Uwongo unaaminiwa na wengi...
Lecture iliitwa Battle of the bible wanavyotaka kuichakachua biblia kwa kuleta tafsiri za kipagani na kichawi kwa kuhariri biblia ya king james version.

Sasa mtu kama mimi binafsi na maisha yangu, hayo unayoyaongelea yananisaidia nini? Kwan wewe babu na mababu zako walikuwa wanawajua hao unaowazungumza ni hivyo vitabu vilivyoletwa ili kuwapumbaza??
 
Unahangaika sana.... Fanya kazi, ingiza kipato...porojo za mitaani na lesson zitakuangamiza

Ujumbe wako ni murua
 
We lazima ni msabato tu Roman Catholic Taifa kubwa, huwez kuja na hoja eti zilizoandikwa na magezeti sjui maneno ya watu acheni figisu hubirini neno la Mungu
Hivi Mme uliyemkimbia na ukaenda kuanzisha nyumba yako na kaamua kukaa kimya unamtafuta tafuta wa nini.
Jamani tuacheni RC tufuate yetu, endeleeni na yenu...hubirini injiri si kusimanga imani za wenzenu.
Nashindwa kuelewa huwezi hubiri imani yako bila kumfuata fuata mwenzako?
Catholic shall remain Catholic and its foundations which are intensively built....and no one with his human's power shall defeat it...only God if he deems so!
 
Back
Top Bottom