Hivi ndivyo rais mstaafu Mwinyi anavyomzungumzia Makamba

Makamba una haha kujipa promo.....wakati unaibu waziri tu unakushinda.....wananchi wanaibiwa fedha zao na makampuni ya simu, wewe hata habari ya kuwatetea huna....leo unautaka urais kwa lipi hasa?

Mie huwa najiuliza hili swali kila siku, huyu unaibu uwaziri tu hajafanya lolote ETI anataka uraisi! nani alimwambia anafaa kutuongoza? kwa lipi? baba yake nae hakuwa na historia nzuri alipokuwa mkuu wa mkoa hasa hapa dsm!
 
we msese unataka mh.makamba akufundishekutumia simu??
hahah!! tatazo letu wabongo tunapenda sana ofa za kwenye mitandao ya cm!!!!
sasa wakitulima lawama kwa wizara! why?
ww ukiona umeibiwa na kampuni ya cm kwanza wafate hao kampuni wakuelekeze,, uzembe wako
Kweli nimeamini wapiga debe wa Ma_rope ni vichwa vitupu,nadhani hamkuandaliwa vyema namna ya kumtetea bosi wenu...unasema tuende tukayalalamikie makampuni ya CCM kwamba wizara haihusiki...oh yes hata akiwa rais tutarajie majibu ya namna hiyo kwamba twende tukawalalamikie watu wengine kwakuwa yeye rais ahusiki!No hatuhitaji Kikwete mwingine atuongoze.Tunamtaka kiongozi atakayefanya maamuzi magumu,hatutaki kiongozi atakayeyakimbia majukumu yake.
 
makakamba uraisi sio essay uandike usaishiwe .Swali langu moja tu Katiba pendekezwa ulichangia nini? Escrow? EPA? au ulikuwa hujazaliwa tunachotaka sio ujana bali mtu mwenya mawazo mapya mawazo yako ni sehemu ya mateso yetu na hiyo njia uliyotumia haikusaidii simama kwa miguu yako tunataka mabadiliko hatutaki muendelezo wa kulindana na ma network ya ajabuajabu ambayo wewe ni sehemu yake.umasikini unatuumiza wewe si maskini na hujakulia umaskini usitudanganye

Urais ni rahisi sana. Hilo ndio analolijua yeye kama muandika hotuba wa Rais asiyesikia aibu. Jee mnakumbuka ile hotuba ya kule Ujerumani? Mwenyekiti wa kikao kile alikuwa mwanamke, na mkulu akawa mmoja wa watoa mada na alianza hivi; " Thank you Madam Chairman .............." Sasa mwandishi wa hotuba hiyo leo anataka kuwa Rais.
Hii ni sawa na House girl baada ya kusisikia mama mwenye nyumba kafariki anatangaza nia kwa vile choo cha ndani alikuwa anadeki yeye.
 
Wapiga debe wa Ma_rope mna kazi sana...kumpromote huyo empty vessel wenu yataka moyo!Watanzania siyo wajinga wachague mtu kama Ma_rope. Ma_rope akiwa rais akiya mungu nahama nchi,maana hiki kitakuwa kielelezo cha umaskini wa akili wa hali ya juu wa Watanzania na mimi sitataka nionekane sehemu ya jamii hii iliyopoteza matumaini ya kuelevuka hapa duniani.
 
Ni dhambi kubwa kumrubuni Mzee Ruksa akuandikie Foreword ili nawewe mtu ambaye huna lolote kwenye utumishi wa Taifa hili ili tu uonekane unaweza. Januari jitendee haki, huna sifa hizo ambazo unajaribu kujivalisha. Kwanza kwenye Serikali ijayo hata ukishinda ubunge sioni kama utakuwepo kwenye baraza la mawaziri.

Tutasoma mengi!!!! Ila niwakumbushe tu wakati Kikwete anatafuta Ikulu, mtu mmoja dalali mashuhuri wa wanasiasa Tanzania, Bw Prince Bagenda alitunga kitabu, ati Kikwete ni tumaini lililorejea. Kwa kazi hiyo alikulakula vihela vya mgombea, CCM na baadaye Ikulu. Mwingine akabuni jina la Kikwete na kulifupisha kuwa JK hadi leo. Huyu ni Bw Salva Rweyemamu, ambaye baadaye aliteuliwa kuwa Mkurugenzi, Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu. Sasa kaja Karugendo, naye anaziwinda pesa za January Makamba, atazila. Kinachonifurahisha ni kuona hawa wenzetu (sijui tuite Wahaya) wana pua za kunusa pesa zilipo. Kila mahali Escrow, Escrow, kweli Mhaya hachezei nafasi.
 
January anatumia mkakati wa kujitangaza kwenye vyombo vya habari. Na hilo la kumchukua Mzee Mwinyi, amuandikie dibaji, unafikiri Mz. Mwinyi angekataa? Mzee hasikiki katika masuala mtambuka ya nchi zaidi ya kusikia amedhalilishwa kwa kupigwa vibao na vijana wahuni. Ilikuwa ni heshima kwa Mz. Mwinyi kumuandikia hiyo dibaji.

Turudi kwa January, bado hatoshi na ndio maana hata maana hata raisi wake amemuacha kwenye nafasi ya unaibu muda wote.

January, kete yake kubwa ni kuwa amemuangalia rais akitenda kazi , hivyo anafikiri kuwa basi ana ufahamu wa kutosha wa majukumu ya uraisi.

Nimemuambie January... mashabiki wanaokwenda kumuangalia live CR au Messi , hawawezi wakasema wataingia uwanjani na kufanya vitu vya CR au Messi ni zaidi ya hapo.
 
Nimefarijika kuyasoma mazungumzo baina ya Padri Privatus Karugendo na Ndugu January Makamba, mmoja wa viongozi mahiri wa zama za sasa.Nawapongeza kwa kuamua kuyaweka mazungumzo yao katika rekodi ya maandishi. Hakika tumejifunza mengi kuhusu na kutokana na historia na falsafa ya maisha ya Ndugu Makamba pamoja na fikra zake kuhusu Tanzania ijayo.

Jamii inanufaika tunapowafahamu kwa kina viongozi wetu. Utaratibu huu wa Padri Karugendo ni jambo jema na inabidi uendelezwe. Binafsi nilikuwa namfahamu Ndugu Makamba kama kiongozi ndani ya Chama chetu na kwenye Serikali. Fursa ya kusoma mazungumzo yake imenisaidia kumfahamu zaidi kama mtu lakini pia kufahamu fikra zake. Nimefarijika kwamba nchi yetu na Rais wetu Kikwete ameendeleza utamaduni aliouanzisha Mwalimu Nyerere na kuendelezwa nami wa kuwaamini vijana na kuwapa fursa za uongozi ili kuwaandaa kuiongoza nchi yetu.

Nilimteua Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mbunge na Naibu Waziri akiwa na umri wa miaka 38 tu na baadaye Waziri wa Wizara muhimu ya Maji, Nishati na Madini akiwa na umri wa miaka 40 na baadaye Waziri wa Fedha. Sikufanya hivyo kwasababu tu ya umri wake bali kutokana na kuamini katika msingi wa kuandaa viongozi wa vizazi vijavyo kwa kuwapa majukumu katika Chama na ndani ya Serikali. Kwa kusoma mazungumzo ya Padri Karugendo na Ndugu Makamba ni dhahiri kabisa kwamba Ndugu Makamba aidha ameandaliwa au amejiandaa vizuri kuwa kiongozi mkubwa. Kazi hii ya kuandaa viongozi lazima iendelee kufanywa. Kiongozi mzuri ni yule anayetengeneza viongozi wengine wapya.

Kila zama na kitabu chake, kila zama na changamoto zake na kila zama na mitume wake. Wenye zama zao wanakitendea haki kizazi chao na vizazi vijavyo wanaporekodi masaibu na matumaini ya zama husika. Nimejifunza kupitia mazungumzo haya kuhusu aina ya Tanzania ambayo Ndugu Makamba anaitaka. Imani yangu ni kwamba mazungumzo haya, pamoja na mengine ambayo wengine watayafanya, yataleta mjadala wenye afya kuhusu Tanzania tuitakayo.


View attachment 218769

Ali Hassan Mwinyi
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dar es Salaam
22/12/2014

Kwa akili yako bado unafikiri ujinga watz ni mtaji wa kisiasa, ok tusubiri
 
Nilikuwa simpi nafasi sana mwanzoni lakini nadhani huyu Kijana ni Obama wa bongo anafaa.
 
Haya yote ni matokeo makosa yaliyofanywa na Watanzania mnamo mwaka 2005.
Wengi kati ya tuwaona tuwaonao wakiji promo sasa wana amini watanzania hakuna kitu wanachoweza kukifanya vizuri tena kirahisi kama makosa. Wana amini watanzania wana kipaji cha kukosea kama makosa si sehemu ya maumbile yao.
Wana amini ujinga na tamaa ya watanzania ndiyo mtaji wao mkubwa katika harakati zao. Ndiyo maana wamevuruga miundo mbinu yote yenye kuamsha na kuchochea ufahamu ndani ya jamii ili wao waendelee kuwa juu...ndiyo waendelee kuwa juu ya wajinga na kuishia wafalme wa wajinga katika himaya ya wajinga.
 
January ni NAIBU WAZIRI AMBAYE YUPO LAKINI HAYUPO. Hakuna mwananchi wa kawaida anayejua kuwa January amefanya nini kwenye nafasi aliyopewa mpaka yeye kujifikiria kuwa anastahili kuongezewa kazi. Kwangu mimi naona Makamba hata nafasi ya unaibu waziri haiwezi maana ndani ya wizara hiyo kuna mengi ya hovyo, na hakuna anayejua January amefanya nini kuondosha ubovu uliopo wizarani kwake.

Nawezi kusema kuwa January hana upeo, uelewa hata akili ya kiuongozi. Viongozi wenye akili wakipewa nafasi, kwenye nafasi walizopewa, hufanya mambo makubwa ili kuuambia umma kuwa wana uwezo mkubwa zaidi na wanaweza kufanya makubwa zaidi wakiongezewa mamlaka. Siyo kupita unapiga kelele mitaani kuwa 'nautaka uraisi'. Ebo! Wewe utakuwa ni kichaa si bure. Yaani tukupe urais kwa kigezo gani?

Hapa Tanzania, huenda Kikwete atakuwa wa mwisho kupata urais bila ya kuwa na rekodi ya utendaji unaoonekana.

Viongozi wenye akili ni kama Magufuli, Mwakyembe na Muhongo. Wanafanya kazi hasa. Hiyo ndiyo kampeni ya watu wenye akili. Wenyewe hawajasema wanautaka urais lakini watu wanawaongelea, japo kwa mbali. Muhongo, sifikirii kama kuna mtu anamfikiria kuwa Rais lakini utendaji wake kazi ndiyo unampa kigugumizi hata Rais kutekeleza yale aliyoagizwa na Bunge. Nina hakika kama Muhongo angekuwa kama January, Maghembe, Ghasia, Shukuru au Masele angekuwa alikwishamtimua zamani kabisa.

Makamba anachukizwa na kila aina ya ufisadi, na mara kadhaa amaenuliwa akisema waliojipatia fedha za ESCROW akaunti isivyo halali lazima kila mmoja wao abebe mzigo wake..
 
Hehehe January Makamba to presidency uwiiii hicho ni kichekesho aisee...huyu jamaa ameganya kitu gani kwa taifa tukamuona anafaa....ubunge bambuli amejitahidi....jee unaibu wazirii jee ameweza hata kukemeaa kunavyopigwa katika bundles zetu huku...ameweza kuweka proposal kali za kuwadhibit hawa wawekezaji ktk wizi wa sekta ake
 
Mimi mgombea nitakayemchagua ni yule anayeunga mkono rasmi ya katiba ya Warioba.Lakini pia na sifa zingine muhimu kama vile uadilifu,uchapakazi nk.Hadi sasa sijampata mwenye sifa zaidi ya Dk.Slaa.
 
Hivi huyu Makamba si naibu waziri wa miundombinu? Mbona anashindwa kutatua wizi wa uwazi unaofanywa na makampuni ya simu na internet providers? Aje kuwa rais wetu atafanya nini cha maana ikiwa hapa alipo tu anashindwa kutekeleza wajibu wake?
 
We should not rely on these silly 40 questions and a man come out calling himself a president to be....ohooohooo...i wonder if he can answer any ugly questions like...what positive and credible thing did U do in ur ministry and to the Tanzanians in general that can c U as a proper presidential candidate......
 
January tatizo lake moja tu ...na hilo mtakubaliana na mimi! Not tough enough!!!! Mmemuona hata kwenye escrow jamani kimya kama hayupo bungeni! Jinsi tunavyoibiwa na makampuni ya simu, yanavyo chakachua kodi ya serikali hakuna alichofanya!!!!!! He doesn't have balls to lead this Tanzania now!!!
 
Jk amesababisha urais uonekane mwepesi hd kila mtu anautaka maana wanajua wakifika ikulu watapiga hela ndefu kwsbb huko ni kwenye kichaka cha majambazi na pia watakwea pipa angani mara nyingi watakavyo, hivyo wanatafuta kukamata fursa kisha waitumie.
 
Back
Top Bottom