Hivi ndivyo nimjuavyo Mwigulu Nchemba

Hivi ndivyo nimjuavyo Mwigulu Nchemba

huyu hana tofauti na pilato, na adhabu ni kusulubiwa kwenye mti mrefu kwa mnyororo wa moto
 
Mleta mada kaka umeandika hivi sababu ya njaa, basi mwenzetu njaa yako imezidi, sifa gani za kumsifia mwanaume mwenzako kiasi hicho.........tena unamsifia mtu anayenyooshewa vidole na kila mkataa maovu katika Nchi hii.
 
Mbona unatumia avatar ya kike wakati tunajua Iliboru wanasoma wanaume tuu au sikuhizi umekuwa mambo swafi mombasa utaenda lini?
 
Wahi kupanga foleni hapo mjengoni upate malipo yako!
 
sasa tunataka ukweli uwekwe hadharani, JAMANI NAOMBA MTU YEYOTE MWENYE CV YENYE TABIA HALISI ZA MTU HUYU AIWEKE HADHARANI, MAANA TABIA YAKE NA HAIBA YAKE MBELE YA WATANZANIA SIO NZURI. LAKINI PIA KAMA INAWEZEKANA NA PICHA ZAKE ZIWEKWE HADHARANI.
 
Hamad Mohamed! Mbona imani yetu haituruhusu kukaa uchi. Ni kwa nini unatumia picha ya mwanamke kaacha maziwa nje kama avatar?

Note: Sio kila mzungu ni mkristo, si kila mwarabu ni muislam......!
 
Nilianza kujua umahiri wa Mwigulu kuongoza pale alipoongoza kama kaka mkuu wa shule yenye kidato cha 5&6 huku akiwa kidato cha tatu. Wanafunzi walimkubali kwani alikuwa akiona hitilafu kwenye masilahi ya wanafunzi anamwita mkuu wa shule na kumwambia makosa ya utawala black and white.

Huyu bwana Hamad Mohamed nadhani haijui vizuri historia ya usimikwaji wa viongozi pale Ilboru Sekondari hususani kipindi Mwl Kitemango akiwa mkuu wa shule.

Utaratibu wa shule ya Ilboru ulikuwa ni kusimika viongozi ambao ni mapandikizi ya waalimu haswa mkuu wa shule.

Huyu Mwigulu alikuwa ni pandikizi la mkuu wa shule ambaye asili yake ni Mnyaturu wa Singida na aliwekwa madarakani kama kibaraka tu kwa maslahi ya Kite.

Kwa kuwa Nchemba ni mwenyeji wa Singida, suala la kuwa kibaraka wa mkuu wa shule watokaye mkoa mmoja lilikuwa dhahiri.

Baadaye pale Ilboru walikuja viongozi(makaka wakuu) kama kina Gaki, Migiro (huyu alikuwa makamu), kuna mnyaturu mwingine namkumbuka kwa jina la Suleiman(pia alikuwa mnyaturu) wote hawa walikuwa vibaraka waliopenyezwa tu.

Naamini hata huku mbele alikoendelea atakuwa ni kibaraka na mtu wa kubebwa tu ili kufanikisha adhma za wakubwa zake.
 
Story za chuo kikuu ni za uongo, Mwigulu hakuwahi kuitisha mkutano Wowote kwani hakuwa kiongozi japo aligombea tangu akiwa mwaka wa kwanza mwaka 2001 ila alikosa, alikuwa mtu wa kujipendekeza sana kwa Luhanga, mwaka 2002 wakati wanafunzi 800 waliponyimwa mikopo alikuwa akiwa spy wakina Novatus Akondowe, Paul mnashauri na wengine ambao walikuwa waki organize wenzao , kazi hiyo alikuwa akiifanyayeye , Kelvin ambaye yuko mzumbe sasa na Nawanda ambaye ni kuu w Wilaya yake .....

Hamad, umesimuliwa uongo nawe Ukija kuuandika hapa, wewe ulimaliza UDSM tawi la Duce mwaka 2010 miaka mitano baada ya Mwigulu kumalizika UDSM ......WEWE NI MWALIMU ila ulipopangiwa kwenda kufundisha Misungwi ulienda kuwachukulia fedha zao na ukarejea Dar.......Acha uongo.......
 
Huyu mleta maada cjui ni mchumba wake, nafikiri aliwahi kutoka nae,
Mwigulu popote ulipo nakuhakikishia utakufa kifo kibaya ukitoa macho kama ndulele na mdomo wazi,
Hili lijamaa cjui kama linamjua mungu,
Mwigulu kuwa na cheo madarakan na kuwanyanyasa masikin si mwisho wa maisha,
Unatumia jeshi, police na usalama wataifa kuua watu na kuteka,
Cheo ulichonacho unajiona ww ndo mungu na hutokufa,
Kumbuka vyeo vinapita tu na kwa mungu cheo chako hakitambuliki,
Umeua watu wasiokuwa na hatia,
Umewang'oa kucha ww ndo mratibu wa mambo yote,
Kama unakumbuka arusha uliwahi kusema kuwa Dam lazima imwagike arusha,
Kwenye zile kata 4 za udiwan,
Ulikodisha police kutoka moro wakaja kurusha bom kwenye uwanja wa soweto na likauwa watu wasiokuwa na hatia,
Na hotel uliyofikia mwigulu chemba ni Stereo Hotel iliyoko maeneo ya makao mapya karibu na stand ndogo,
Cku ulipolipua bomu jion kbs, vijana wa arusha walikuja kuzingira hotel hiyo bahat ukijifungia hotelin, ilipofika saa 9 ucku police walikuja na magar yao 3
Na wakaamuru hotelin hapo wazime taa za nje,
Walipozima ulitoka saa 9 ucku ukasafirishwa kuja dar,
Baadae ukatangaza kwenye vyombo vya habar kuwa chadema ndo imejilipuwa,
Kwa kutafuta huruma ya wapiga kura haingii akili hata kidogo
Walitumia kila silaha ila mungu ni mkubwa sn,
Ww chemba utakufa kifo kibaya sn cku ukifa
Arusha tufanya sherehe kubwa sn ya kushangilia,
Kufa utakufa tu huwez kukwepa kufa,
Utakufa mwenyewe na si cheo chako,
Ukifa mm nitakuombea ULAZWE MAHAL PEMA MOTONI,
NA ADHABU IWE MOTO WA JAHANAM!! Inauma sana
 
mabaya yanapokuwa mengi kuliko mazuri hata Yale mazuri hufichwa na mabaya!
bahati mbaya kwa upofu na Mahaba kwake hilo hutokaa ulione!
 
Eti kwa sifa hizi ndio chaguo la CCM kwenye kiti cha Urais 2015. Ni wakati sasa na huyu akaitwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya CCM kwani yeyote anayejisifiasifia anaonyesha nia ya kujitangaza kugombea Urais.
 
hamad mohamed! Mbona imani yetu haituruhusu kukaa uchi. Ni kwa nini unatumia picha ya mwanamke kaacha maziwa nje kama avatar?
mkuu,hilo ni jina tu.hana imani yetu.angekuwa muislam asingeweka hiyo picha.ni mroho wa madaraka
 
tuna safari ndefu, bila kueliminate wapuuzi kama huyu alepost utumbo hatatafika
 
Hapo kwenye namba 2, Tema Mate sikubaliani na wewe, hasa kuhusu mwalimu Msasa, hakuwa Mazengo miaka hiyo ya 1998-2000, Msasa alihama Mazengo miaka ya 1987. Mengine sijui ila chembe ya uongo huondoa ukweli.
FAHAMU,UJASIRI NA MSIMAMO WA MH:MWIGULU NCHEMBA HAUJAOTA KAMA UYOGA,NILIPATA KUSOMA NAYE NA HUYU NDIYE MWIGULU NCHEMBA NINAYEMFAHAMU MIMI NA WATANZANIA WENYE UWEZO WA KUCHAMBUA UWEZO WA VIONGOZI WETU.


1798508_499004793537271_1354415385_n.jpg


NDG zangu nilipata bahati kusoma shule moja na kiongozi huyu kidato cha 1-4 Ilboru (1994-97) na kidato cha 5-6 (1998-2000) Mazengo na chuo kikuu UDSM na sasa ni mwl niko Dodoma naitwa Hamad.

(1) Nilianza kujua umahiri wa Mwigulu kuongoza pale alipoongoza kama kaka mkuu wa shule yenye kidato cha 5&6 huku akiwa kidato cha tatu. Wanafunzi walimkubali kwani alikuwa akiona hitilafu kwenye masilahi ya wanafunzi anamwita mkuu wa shule na kumwambia makosa ya utawala black and white. Nakumbuka siku moja chakula kilikuwa kibaya akaita wanafunzi tukaenda na sahani akatwambia chakula leo kibaya naomba tusile mpaka nimlete mkuu nimwambie arekebishe. Tukasubiru akajanae akamwambia, nanukuu, mkuu chakula leo ni kibaya hakifai kwa afya ya binadam. Hivyo nimewambia wanafunzi wenzangu tusile mpaka kitakapopikwa kingine. Wakapika "KITEI"

(2) Tukiwa Mazengo kulikuwa na tabia ya


walimu wote kutembeza bakora kila jumatatu. Mwigulu alipochaguliwa kuwa katibu mkuu akamwambia headmaster mwl Msasa aliyekuwa anaogopeka mpk kwa walimu kuwa hataki walimu waje na viboko kuchapa wanafunzi kwa vikosa vidogovidogo kwamba kuna serikali ya wanafunzi na kazi ya kusimamia wanafunzi ni kazi yao wawaache wafanye kazi yao. Alibadili tabia ya wanafunzi kukimbilia kujificha "sudani"


(3) Mwigulu alikuwa akiwambia black&white ma profesa wa chuo kikuu, alipokuwa akipigania upatikanaji wa viti vya kusomea mabibo hostels. Nanukuu, Maprofesa wazima mnatuletea baa humu hostel huku mkijua hatua pakusomea. Hivi ni kweli hamjui tumefuata nini hapa? Sasa wanafunzi wenzangu tutachukua viti vya baa tuvifanye vya kusomea, baa itarejea tukishamaliza shule na kufaulu au watakapotuletea viti.

Wanafunzi zaidi ya 4000 walichukua viti huku wakiimba wanaimani na Chifu jina alilokuwa akifahamika nalo chuoni. Kitendo hicho kilimfanya asimamishwe, wiki 2. Aliporudi akakuta viti hakuna akaita mkutano tena, akasimamishwa wiki 3 akarudishwa baada ya chuo kuweka viti chini ya kila bweni mabibo.

(4)Akiwa BOT nilipata taarifa tokea kwa classmate wetu kuwa Mwigulu alihoji kwa GOV kwanini wakurugenzi wamekopeshwa magari mapya tena bila kodi, wanapewa mafuta yakutosha wala hawaishi mbali lakini wanatumia magari ya pool ya ofisi? Hii ni ukosefu wa uadilifu. Wafanyakazi wakampenda wakurugenzi baadhi wakamchukia baada ya wiki mbili akapewa uhamisho tokea makao makuu kwenda Arusha.

(5) Akiwa kwenye chama rafiki yangu aliyeko Lumumba aliniambia huyu jamaa ana ujasiri wa wapigania uhuru alisema kama ambavyo huwakemea wapinzani akitolea mfano wa mbowe aliyedanganya umma kuwa hataki gari ili kupunguza mzigo ila baadae akachukua jipya kimyakimya na alivyo mlipua mbowe alivyokwenda na kimada wake dubai kwa gharama za bunge (kodi za watanzania), alisema jamaa huyu hamwogopi hata mwenyekiti wake kwenye vikao. Alitilea mfano swala la loliondo.
Mwigulu alipowasikiliza wananchi nakuelewa hoja yao, aliwambia nimewasikia na nimewaelewa. Katika kikao alichoitisha Rais akiwepo mwigulu na badhi ya mawaziri. Mwigulu alisema bila ardhi wananchi wa loliondo hawana maisha hivyo serikali aangalie upya msimamo wake. Ndipo waziri mmoja akasema kuliko kufuata ushauri wa mwigulu bora aache uwaziri. Mwigulu alichofanya alichana karatasi akampa waziri huyo na kumwambia Rais mpe kalamu waziri wako ajihudhuru sasa hivi aende nje halafu sisi tuendelee kujadili maisha ya watu wa loliondo. Waziri akaomba radhi na jambo hilo likaisha mpk leo Loliondo walituma ujumbe wa watu 80 wakimwomba mwigulu akagombee ubunge loliondo au aombe nafasi ya kitaifa ili nao wampigie kura.

(6) Sasa baada ya kuwa Serikalini ameendelea kuweka msimamo kwenye mambo yenye tija kwa watanzania
(A) Kulipokuwa na mjadala wa wabunge wa bunge maalumu kutaka waongezewe posho tokea laki 3 hadi saba, mwigulu alijitokeza nakusema, nanukuu watanzania wanashida sana. Kuna wanaokula mlo mmoja, kuna wazabuni wanadai, walimu wanadai, huduma bado duni hosipitalini. Wabunge hawa wamebajatika kuteuliwa na jambo la katiba ni sehemu tu ya wajibu wao. Hatujawakodi tokea kenya, uganda au ulaya kama consultants.

Anayedhani hapa anapata hela kidogo kuliko alikokuwa kwa heshima zote na afunge virago aondoke zake. Baada ya kauli yake mjadala huu ukafa. Huu ni ujasiri wa aina yake. Taarifa zilisema kuwa wabunge hao walipangiwa laki 8 kwa siku mwigulu akazikataa baada tu ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

(7) Sasa hivi majuzi ameweza kuwambia ukweli wazungu. Hotuba kama hii wazungu walizoea kuona kwa Mwl Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Nelson Mandela na Patrice Emery Lumumba.
MWIGULU NCHEMBA AHUTUBIA BUNGE LA ACP NA EU,APINGA WAZI WAZI MAPENZI YA JINSIA
Sehemu ya Majibu yake ni haya hapa.
As I have just said, the ACP Council recognizes the strategic importance of access of sexual and reproductive health care including family planning. To our values, tradition and beliefs sexual and reproductive health and rights includes pre-and post natal care and safe delivery, prevention and treatment of infertility and STDs including HIV and AIDS, access to contraceptives, reducing the recourse to unsafe abortions and comprehensive sexual education. The matters related to homosexuality are strictly out of contexts. I would argue the international community with due respect to refrain from linking the development assistances with the specific country stand on homosexual policies. Just like there was colonization, and it come to pass, and we have passed through various periods of Development Assistances with various conditionality’s but if we are told to choose between our Values without assistance or Assistance tied with homosexual conditions, we will in top of our voices and in confidence remain with our Values without an assistance in dishonour of homosexual policies.

(8) Zipo taarifa pia kuwa Mwigulu alikataa kupangishiwa hotel baada ya kuteuliwa kuwa naibu waziri kwa madai kuwa watanzania wanashida nyingi hawezi kwenda kuishi hotelini.Walipomwambia ndio utaratibu mwigulu alisema hapendi kwenenda kwa mazoea bali anaenenda kwa uhalisia. Alisema zaidi ya robo tatu ya ndg zake wanaishi nyumba za tembe na nyasi. Hawezi kufanya hotel ndio nyumba yake ya kuishi.

Nisiwachoche, in short Najivunia kumjua kiongozi huyu maarufu aliyevuma kwa kasi zaidi katika siasa za Tanzania. He is Bold, Firm, Visioned and Consistent, ana Sifa za kiongozi anayetakiwa kuongoza Taifa hili tunakoelekea.
Wenu,

Hamad Mohamed
hamadmohamed23@gmail.com
Dodoma
Tanzania



 
Back
Top Bottom