Hivi ndivyo nilivyoibiwa kirahisi

Hivi ndivyo nilivyoibiwa kirahisi

Ilikua Siku ya Jumapili,
Kaja kijana Dukani kwangu ambako ninauza mitungi ya gesi ya kupikia majumbani.
yule kijana alifika dukani hana mtungi wala hela ya gesi.

akamwambia kijana wangu wa dukani ampe mtungi mkubwa wa gesi na kama kuna boda boda anayemfahamu waende na huyu mteja ili ampe hela na Mtungi empty,

Kijana bila kujiuliza akamuita boda boda akampa mteja gesi na akamlipa boda boda basi wakaondoka na mteja.

walipofika njiani akatokea mtu kama anatoka kwenye makazi ya watu ili kupokea ule mtungi wa gesi,
Alipoupokea yule mteja akamwambia boda boda ampeleke sokoni akanunue viazi akirudi ndio ampe pesa ya gesi na mtungi.

walipofika sokoni kwakua boda boda haziruhusiwi kuingia sokoni jamaa akaingia sokoni. Boda boda akasubiri mteja wake pale masaa yakawa yanakwenda tu. kumbe ndio alishapigwa
Kama wewe ni CCM endelea tu kuibiwa
 
pole sana mkuuu...mimi alikuja MAMA mtu mzima kiasi kwamba huwezi fikiri au waza anaweza kuwa tapeli...Akanambia kijana hujambo nikamjibu sijambo nikamsalimia akaitika.

Akawa anataka vitu tofauti tofauti Hesabu ya vitu vyote alivyotaka ikafika kama 35,000 akatoa pochi yake anilipe mda huo namfanyia kazi yake alikua analalamika miguu inamuuma so nimpe kiti akae,nikampa.

Baada ya kutoa pochi kuangalia ndani akajikuta ana hela pungufu,basi akaniomba "mwanangu nimepungukiwa na hela naomba nikutumie hela yako MPESA" Nikamwambia TUMA mama nikampa namba yangu akanitumia mpaka na yakutolea.

Akachukua mazaga yake akasepa..mimi hua ikiingia hela MPESA siitoi kwa wakala huwa na recharge mashine ya maxmalipo so aliniekea kama 38 mimi nikaihamishia 38 yote kwenye mashine ya maxmalipo.

Baadae siku hiyo hiyo kuna mtu nilikua namdai kama 50,000 akanambia anipe nikamwambia TUMA MPESA alipotuma tu nikapokea msg ya muamala wa kuingia hyo 50k then dakika hiyo hiyo ikaja msg inasema "muamala uliokosewa kutumwa kwako kimakosa wa sh.38,000 umerudishwa kwenye akaunti ya mtumaji"

Hapo ndio nikashtuka yule bi mkubwa baada ya kutoka hapa dukani aliende kupiga simu VODA kuwambia ametuma pesa kimakosa tena na hivi ni mama nadhani wakat anaongea na customer care aliweka sauti ya kibibi kabisa Hela yake ikarudishwa kwake.

Napiga simu voda eti nao wanasema mtu alikosea kutuma,nkawaelezea situation ila hamna walichonsaidia Aseee ikaenda hivyooo ndio ikawa mwanzo na mwisho mtu kunilipa hela kwa Mpesa yani sasa hivi kama nakudai au unahela yangu hata kama upo TUKUYU ntakusubiri urudi unipe hela yangu.

Nakubali kulipwa mpesa kwa ninao wajua TU ila hawa wateja asee nmekoma.
 
Halafu sikuhizi ndio mana vijana tunaonekana hatuheshimu wazeee,maana wanaofanya haya matukio saivi ni wababa/wamama/wababu/wabibi vijana wa siku hizi hawatapeli kizembe labda wajiridhishe kweli huyu katoka CHATO leo leo..

Ila wanaotupiga hapa town saivi ni washua kabisa,ndio mana nikipandaga dala dala staki kusogelewa na mzeee kabisa mimi,asimame hukoooo maana ndio wapiga watu Fingers🤞
 
Ilikua Siku ya Jumapili,
Kaja kijana Dukani kwangu ambako ninauza mitungi ya gesi ya kupikia majumbani.
yule kijana alifika dukani hana mtungi wala hela ya gesi.

akamwambia kijana wangu wa dukani ampe mtungi mkubwa wa gesi na kama kuna boda boda anayemfahamu waende na huyu mteja ili ampe hela na Mtungi empty,

Kijana bila kujiuliza akamuita boda boda akampa mteja gesi na akamlipa boda boda basi wakaondoka na mteja.

walipofika njiani akatokea mtu kama anatoka kwenye makazi ya watu ili kupokea ule mtungi wa gesi,
Alipoupokea yule mteja akamwambia boda boda ampeleke sokoni akanunue viazi akirudi ndio ampe pesa ya gesi na mtungi.

walipofika sokoni kwakua boda boda haziruhusiwi kuingia sokoni jamaa akaingia sokoni. Boda boda akasubiri mteja wake pale masaa yakawa yanakwenda tu. kumbe ndio alishapigwa
pole mkuu
 
ila huyo mwizi alitumia akili sana
 
Back
Top Bottom