Utapeli mpya kwa wafanyabiashara

danhoport

JF-Expert Member
May 20, 2020
1,607
3,194
Habari ndugu zangu,

Huu utapeli unaweza ukawa ni mpya kwangu ila kwa wengine ni wa kizamani. Ipo hivi jana kuna mteja alipiga simu dukani anataka betri za gari(N150 mbili na N70 moja) tukakubaliana apelekewe Masaki, tukamtafuta bodaboda wetu mwaminifu tukampa mzigo.

Yeye(tapeli) alichofanya hapo Masaki alitafuta sehemu akawaomba wenyeji kuwa kuna mzigo wake kuna mtu anamletea alikuwa anaomba amkabidhi then atakuja kuuchukua baada ya mda. Bodaboda alivyofika walipokubaliana akampigia simu huyo tapeli ila jamaa(tapeli) akamwabia kuna mlinzi hapo amkabidhi afu pesa ya betri pamoja na ya usafiri aje achukue Mikocheni mana amepata emergency kidogo(kumbe kuna sehemu kajibanza anamchungulia)

Bodaboda akauacha mzigo kwa walinzi akijua ndo nyumbani kwa jamaa kisha akaanza safari kuelekea Mikocheni, na yule jamaa baada ya kuona boda kasepa akaja na bajaji akapakia mzigo akaondoka zake. Boda kufika kule simu haipatikani, kurudi alipoacha mzigo wale walinzi wakamwambia jamaa kashachukua mzigo wake.

Boda inabidi arudi dukani kutupa taarifa, boss akamwambia ampeleke alipouacha mzigo walivyofika pale kwa bahati nzuri kulikuwa na CCTV camera, jamaa akaonekana na bahari nzuri tena jamaa tunamjua ni jirani yetu(tupo ghorofa moja) akapigiwa simu kwa no yake ya kawaida akasema atarudisha betri ila mpaka naandika hapa bado betri hazijarudi.

Mnisamehee kwa uandishi mbovu
 
Habari ndugu zangu, huu utapeli unaweza ukawa ni mpya kwangu ila kwa wengine ni wa kizamani. Ipo hivi jana kuna mteja alipiga simu dukani anataka betri za gari(N150 mbili na N70 moja) tukakubaliana apelekewe Masaki, tukamtafuta bodaboda wetu mwaminifu tukampa mzigo. Yeye(tapeli) alichofanya hapo Masaki alitafuta sehemu akawaomba wenyeji
Kwa mwandiko mbovu , utasamehewa Ila kwa kutapeliwa kirahisi sio kabisa,! Boda angepiga simu kwa bosi kabla ya kuacha mzigo! Mtazamo wangu!
 
Back
Top Bottom