Hivi ndivyo Google wanavyo endelea kuitajirisha Apple

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,622
Reaction score
8,427
Kampuni ya Apple Inc ambao ni watengenezaji wa vifaa vya mawasiliano kama iPhone, iPads, iPods na MacBooks wameendelea kufanya vizuri kwenye makusanyo ya fedha na kama unadhani kuna siku watafanya vibaya basi fikiri upya!

Apple mbali na kukusanya fedha kupitia mauzo ya vifaa vyake, pia wanakusanya pesa za kutosha sana kutoka Google, katika mkataba mpya ambao wameingia na Google sasa watalipwa dola za kimarekani bilioni 3 kwa mwaka, kwa kuwa tu Google wanataka Apple waendelee kutumia kisakuzi chao kama cha lazima (Default Browser) kwenye vifaa vyao.

Dili hii imepanda ndani ya miaka 3 ambapo mwanzo Google walikuwa wanailipa Apple kiasi cha dola bilioni 1.

Ukasanyaji wa pesa hizo unachangia asilimia 5 ya mapato ya kibiashara ambayo Apple wanaingiza kwa mwaka.

Mchambuzi Bernstein ameeleza kuwa mpango huo wa kulipa kiasi hicho kuna mazuri na mabaya yake kwani Google wanaweza kuona wanatoa kiasi kikubwa cha pesa kuilipa Apple huku wakifahamu Apple hawana Search Engine hivyo watalazimika kutumia Google, ila wakati huo huo ifahamike kuwa Apple inachangia asilimia 50 ya mapato kwa vifaa vyake kwenye ku-search kwenye Google hivyo wafikiri upya.

Chanzo: DIBUTE
 
Badala Apple ndo itoe malipo kwa kwa hao GOOGLE sababu haina google search Engine. Iweje tena apple ndo walipe? Huu ni wizi.
 
Kumbuka ule msemo ukitaka kula lazima uliwe... na Mla huliwa
 
Badala Apple ndo itoe malipo kwa kwa hao GOOGLE sababu haina google search Engine. Iweje tena apple ndo walipe? Huu ni wizi.
Apple wana nyodo sana mkuu, mfano mozilla aliacha tengeneza browser yake kwa ajili ya ios kwakuwa apple waligoma kuweka option ya mtu kuchagua default browser ndani ya lifaa chake jambo linalomlazimisha mtuniaji atumie safari browser kam default browser.
Wakizingua google anaweza tumia hata bing kitu ambacho kinaweza shusha watumiaji wa google search
 
Google wako vizuri sana
 
sio Apple tu opera, mozilla, na wengine wengi wanalipwa na google kwa kuieka kama default search engine
 
Kampuni ya Apple Inc ambao ni watengenezaji wa vifaa vya mawasiliano kama iPhone, iPads, iPods na MacBooks wameendelea kufanya vizuri kwenye makusanyo ya fedha na kama unadhani kuna siku watafanya vibaya basi fikiri upya!

Apple mbali na kukusanya fedha kupitia mauzo ya vifaa vyake, pia wanakusanya pesa za kutosha sana kutoka Google, katika mkataba mpya ambao wameingia na Google sasa watalipwa dola za kimarekani bilioni 3 kwa mwaka, kwa kuwa tu Google wanataka Apple waendelee kutumia kisakuzi chao kama cha lazima (Default Browser) kwenye vifaa vyao.

Dili hii imepanda ndani ya miaka 3 ambapo mwanzo Google walikuwa wanailipa Apple kiasi cha dola bilioni 1.

Ukasanyaji wa pesa hizo unachangia asilimia 5 ya mapato ya kibiashara ambayo Apple wanaingiza kwa mwaka.

Mchambuzi Bernstein ameeleza kuwa mpango huo wa kulipa kiasi hicho kuna mazuri na mabaya yake kwani Google wanaweza kuona wanatoa kiasi kikubwa cha pesa kuilipa Apple huku wakifahamu Apple hawana Search Engine hivyo watalazimika kutumia Google, ila wakati huo huo ifahamike kuwa Apple inachangia asilimia 50 ya mapato kwa vifaa vyake kwenye ku-search kwenye Google hivyo wafikiri upya.

Chanzo: DIBUTE
Fact:- Apple ndio kampuni tajiri namba moja duniani inayotengeneza pesa nyingi kuliko kampuni yoyote unayoifahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni kampuni ya 9 sio ya kwanza, tumia tu akili za haraka haraka Apple vs toyota, iphone za mtaani vs cruiser za serikali
Titicomb hii niliisikia kupitia

Clouds FM na Millard ayo kipindi cha Amplifier.

Na walitaja kampuni 5 kubwa tajiri zinazoingiza pesa ndefu duniani.

Nafikiri Cocacola ilikua namba 3 katika ile listi pia Google ,microsoft, nao walikuwemo ndani ila hawakufua dafu kwa apple.

Hizo Toyota ,shell nk sikuzisikia hata kidogo.

then bila kutoa source hata hao amplifier hawawezi badilisha ukweli.

hii hapa list ya ukubwa wa kampuni kwa mapato

List of largest companies by revenue - Wikipedia

hapo utaona watu kama toyota, volkswagen, walmart, shell, china petroleum wapo juu ya Apple, na Huko USA ni lini Apple kafikia hata nusu ya Utajiri wa walmart?
 
c97dd4e1d0771c68cbe0791480522d79.jpg
afu apple naskia wana hela kuzidi had I serikali ya uingereza uk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom