Hivi Nape anayo pumzi ya kuzifuta NGOs.......................


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
624,763
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 624,763 280
Nape azionya NGOs
Friday, 10 December 2010 20:58

Abdallah Bakari,
Masasi.


UONGOZI wa serikali katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara umesema hautasita kuyafuta mashirika yasiyo ya kiserikali yatakayobainika kuwa yanafuja fedha zinazotolewa na wafadhili, kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii wilayani humo.


Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa wilaya hiyo, Nape Mnauye, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku kumi kwa wawezashaji wa Benki za Jamii Vijijini (Vicoba) ngazi ya kijiji.

Mafunzo hayo yalikuwa yameandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Saidia Watoto (Sawa) na kufanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha mjini Masasi.

Mnauye alisema mashirika yasiyo ya kiserikli ni wadau muhimu katika kuharakisha maendeleo, lakini kama viongozi wake watatawaliwa na tamaa ya kujinufaisha, hayatakuwa na tija kwa jamii.

Alisema kwa msingi huo, uongozi wa serikali katika wilaya yake, hautasita kuyachukulia hatua kali mashiria hayo ikiwa pamoja na kuyafuta.

"Mashirika yasiyo ya kiserikali ni nyenzo na wadau muhimu hasa kama yatafanya kazi na kutumia fedha za wafadhili kama ilivyokusudiwa," alisema Mkuu wa wilaya.

wasiendelee kutoa fedha

Hata hivyo Mnauye, aliisifu Sawa kwa ubunifu na utekelezaji wa miradi inayolenga mahitaji ya jamii.

"Nimemsikia hapa Mkurugenzi wa Sawa amesema wanakusudia kuunda shirikisho la Vicoba la wilaya lakini wanashaka watapaje jengo kwa ajili ya ofisi… serikali itatoa ofisi bure na kila aina ya msaada utakaohitajika," alisema.
 
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
624,763
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 624,763 280

Nape awaonya wanaojitajirisha kwa fedha za NGOs


Imeandikwa na Hassan Simba, Masasi; Tarehe: 10th December 2010 @ 23:15

MKUU wa Wilaya ya Masasi, Nape Nnauye ameyaonya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wilayani humo kutumia fedha za wafadhili kwa malengo yalikusudiwa na kwamba hatasita kuwachukulia hatua viongozi wa mashirika yatakayobainika kufuja fedha kwa maslahi binafsi.

Nnauye ambaye yuko katika miezi yake ya mwanzo ya wadhifa huo, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifungua mafunzo ya siku kumi kwa wawezeshaji wa Benki za Jamii Vijijini (VICOBA) ngazi ya kijiji yaliyoandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya

Saidia Watoto (SAWA) na kufanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii mjini Masasi.

Alisema kuwa, mashirika yasiyo ya kiserikali ni wadau muhimu katika kuharakisha maendeleo, lakini kama viongozi wake watatawaliwa na tamaa ya kujinufaisha wao kwanza hayatakuwa na tija kwa jamii na kwamba wilaya yake haitakuwa na mzaha na mashirika yenye viongozi wenye mtazamo wa namna hiyo.

“Mashirika haya ni nyenzo muhimu ya maendeleo iwapo yatafanya kazi na kutumia fedha za wafadhili kwa malengo yaliyokusudiwa …nataka mjue katika hili sitakuwa na utani kabisa, ukienda kinyume hutufai…..maana NGO moja itakapotumia rasilimali vibaya itasababisha
wafadhili wasiendelee kutoa fedha…hii haitakubalika”, alisema Nape.

Aidha mkuu huyo wa wilaya aliisifu SAWA kwa kuwa wabunifu na wakweli katika utendaji, jambo aliloshauri linafaa kuigwa na mashirika mengine ili kuharakisha maendeleo ya jamii wilayani humo na kwamba serikali itatoa ushirikiano mkubwa kwa asasi hiyo ili iweze kutimiza malengo yake kama ilivyokusudiwa.

“Nimesikia hapa Mkurugenzi wa SAWA amesema wanakusudia kuunda shirikisho la VICOBA la wilaya, lakini wanashaka watapataje jengo kwa ajili ya ofisi…..nataka niwahakikishie Serikali itatoa ofisi bure na kila aina ya msaada utakaohitajika ili lengo hili zuri lifanikiwe…,”
alisema Nnauye.

Awali, akitoa taarifa ya mafunzo hayo kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Nurdin Mhuva, alisema mafunzo hayo ya siku kumi yanahusisha washiriki 16 kutoka vijiji 14 vya Kata ya Lisekese, mafunzo ambayo yatawajengea uwezo wa kwenda kuwafundisha wenzao kwenye vijiji wanakotoka juu ya namna ya kuanzisha na kuendesha benki za vijiji.

Mkurugenzi huyo alisema mbali na mafunzo hayo asasi yake itatoa vifaa muhimu katika uendeshaji wa benki hizo ikiwa ni pamoja na masanduku ya kuhifadhia fedha na nyaraka nyingine muhimu ambazo zinahitajika katika kuanzisha na kuendesha benki hizo.

Alisema mradi huo uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa One UN na kusimamiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), utagharimu zaidi ya Sh milioni 27 na kwamba
wanatarajia kuanzisha Vicoba zaidi ya 16 na baadaye wataviunganisha na vingine ili kuunda shirikisho.
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,562
Likes
1,583
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,562 1,583 280
hajui anaongea nini huyu mtoto
 
Keynes

Keynes

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
501
Likes
24
Points
35
Keynes

Keynes

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
501 24 35
SIYO kila jambo wanalofanya ccm ni baya maana humu naona wengi wanaweka maslahi ya chama fulani mbele zaidi....So mlitaka aziambie NGOs ziendelee kutumia hela vibaya??
FAIR PLAY PLEASE.!!!
 
Nzi

Nzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
13,664
Likes
5,635
Points
280
Nzi

Nzi

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2010
13,664 5,635 280
Nape kama DC hawezi kufuta NGO. Registar wa NGOs ndie mwenye mamlaka ya kufuta NGO kutokana na NGO Act.
 
Mallaba

Mallaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2008
Messages
2,560
Likes
4
Points
133
Mallaba

Mallaba

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2008
2,560 4 133
hawezi kuzifuta, lakini kama DC anauwezo wa kuziwajibisha kama kuna makosa yeyote na pia anaweza akatoa pendekezo kwa register kuzifuta kama ni lazima, hivyo kwa njia moja ama nyingine anaweza akawa part of it.
pili tusiwe washabiki sana kwa kila kitu, hapa sawala linaloongelewa ni matumizi mabaya ya baadhi ya NGO's swala ambalo watu wengi wanalijua, sasa yeye kama kiongozi tena DC anakiongelea kunatatizo gani jamani? kama mtu anafanya mabaya lazima awe criticized na anapofanya mazuri pia awe praised ,not just blamming for everything.be logic please..
 
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Messages
2,263
Likes
270
Points
180
Mtego wa Noti

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2010
2,263 270 180
safi sana Nape...keep it up.
 
Jembe Ulaya

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2008
Messages
456
Likes
1
Points
0
Jembe Ulaya

Jembe Ulaya

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2008
456 1 0
Anachofanya ni kizuri lakini asiishie hapo. Awafukuze pia wale ndani ya serikali yake wanaofuja pesa.
 
M

mams

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2009
Messages
616
Likes
8
Points
35
M

mams

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2009
616 8 35
Huyu dogo anatengeneza jina, mwacheni kwa kuwa ni mpambanaji mwenzetu
 
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2009
Messages
352
Likes
1
Points
33
K

KunjyGroup

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2009
352 1 33
SIYO kila jambo wanalofanya ccm ni baya maana humu naona wengi wanaweka maslahi ya chama fulani mbele zaidi....So mlitaka aziambie NGOs ziendelee kutumia hela vibaya??
FAIR PLAY PLEASE.!!!
Umetaja ccm nimefurahi. Niambie wanalipi lakujivunia kuhusu swala la ufujaji wa pesa za umma? Mfano. EPA. Richmond. Deep Green. Radar. Pesa za halimashauri. Tanroads etc
 
sensa

sensa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
398
Likes
0
Points
33
sensa

sensa

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
398 0 33
Hivi nyie mnafikiri mamlaka ya DC ni madogo? hamjui anamwakilisha nani pale? ndio boss wa eneo husika akitaka uondoke unaondoka
 

Forum statistics

Threads 1,235,629
Members 474,678
Posts 29,229,077