Hivi mwajiri wako akisema lipa hili usilipe lile sio sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mwajiri wako akisema lipa hili usilipe lile sio sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Sep 29, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Salamu sana
  Nimejaribu kupitia magazeti yetu ya leo na karibu kila gazeti na "Dowans yaibwaga Tanesco", "Mahakama yaridhia Tanesco iilipe Dowans" and the same alike. Ukifuatilia sana unakuta utata unagubika sana suala hili hasa hata pale kiongozi wa nchi anakiri kuwa hawamjui mwenye hii Dowans. Mahakama zetu nazo (Ingawa pia nawaheshimu sana wanasheria wetu) bila kuweka maslahi ya nchi hii mbele nao wanaridhia kuwa HIKI KIVULI KILIPWE! Kama hakuna mtu ajulikanaye kwa nini nikiite kivuli ndicho chenye haki ya kulipwa! Kama kweli viongozi wa nchi hii wanadai kuwa Watanzania ndio waliowaajiri na wako pale kwa dhamana ya wanachi waliowchagua, na kuwa wanaitumikia katiba ya nchi hii ambayo inampa nguvu kila Mtanzania kwa nini wanachelea kutoa tamko! Msimamo wa Watanzania waliowengi ninaamini ni kutolipwa kwa Dowan! Kama ni kweli ninavyoamini, NI UKWELI KUWA TUNAWAAMBIA HAWA WAFANYAKAZI WETU KUWA HAKUNA KUWALIPA HAWA DOWANS! Hii ni amri halali ya WAAJIRI WAO!
  Bila hata haya wanakamua ngombe maziwa yameisha na sasa wanakamua damu!
   
Loading...